Upeo wa Prof J.Magembe ndo umefika mwisho? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upeo wa Prof J.Magembe ndo umefika mwisho?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kisoda2, Feb 4, 2010.

 1. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,251
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Naja kwenu ndugu zangu hapa jamvini mnijuze juu ya hii hoja ya huyu waziri kusema kwamba vijana wetu wamefeli 2009 kutokana na kutumia vitabu vingi kwenye somo moja,na kutoa kauli hizi:
  -Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi isiendelee kutumia vitabu hivyo mashuleni.
  -Serikali itaanzisha mfumo wa matumizi ya kitabu kimoja kwa somo katika kila daraja kote nchini.
  -mtihani ni mmoja kwa chi nzima kwa hiyo kitabu kiwe kimoja tu.
  -Shule zisijishughulishe na ununuzi wa vitabu.

  Sasa hapa napata kizunguzungu kuhusu upeo wa huyu waziri na hatma ya elimu ya mtanzania.
  Najaribu kujiuliza alipokua akisoma yeye ni vitabu vingapi alitumia mpaka akaupata huo uprofesa ama hata kufika chuo kikuu.
  Kuna mengi ya kumuuliza huyu bwana atupatie majawabu ya kina ni wapi anatupeleka katika hili.

  Naomba kuwasilisha,..
   
 2. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Matatizo la elimu Tanzania hayatokani na kitabu kimoja, mfumo mzima unahitaji ukarabati mkubwa. Kwa mtazamo wangu Profesa Maghembe ameshindwa kusimamia marekebisho haya.
   
 3. s

  smalnama Member

  #3
  Feb 4, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kwenye kiwango cha uprofressor bado watanganyika tunashindwa kutofautisha kufaulu na kuelimika. kitabu kimoja kitasaidia kufaulu, ili uelimike unatakiwa pamoja na mambo mengine usome widely.
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  mimi nina pande mbili katika swala hili.
  1. Maghembe kwangu siamini kama anahadhi hata ya kuwa kiongozi wa mtaa kwa maana ya hekima na busara na uwezo wake katika kuyatazama mambo.

  2. kuhusu kitabu kimoja mimi ninaunga mkono, kwa maana katika nnchi yenye tabia za kupenda kitu kidogo kama hii, ni hatari...nimewahi kuzungumza na mmoja kati ya waandishi wakongwe wa vitabu mzee Yusuph Halimoja, alinipa ushuhuda wa ajabu juu ya ubora wa hovyo wa nakala kadhaa za vitabu vya kiada ambavyo vilipitishwa na mamlaka husika na kuruhusiwa kutumika, sasa kwa sababu fursa ya kutumia vitabu lukuki iipatikana na ikatumika hovyo basi na turejee tulikotoka ili vijana wetu waongee lugha moja kitaaluma toka Kigoma hadi Mtwara, toka Rukwa hadi DSM.
   
 5. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #5
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimemuona wakati akijikanyanga kwenye kipindi cha Tuongee ASsubuhi cha Star TV na bahati yake kwa sababu hakuulizwa maswali magumu \
   
 6. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,251
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Naona ameshindwa/kaona aibu kutwambia kuwa tz tunasomea mitihani na sikupata elimu ya kutusaidia katika kuleta maendeleo.
  Na hii ndo maana hata wakurugenzi,wabunge na ma CEO kama wapo hawatupeleki kule tunakopaswa kwenda badala yake wanaishia kwenye michakatozz isokuwa na tija pale walipo.

  Ama kweli MMK uliposema watz tunapenda vyepesi vyepesi,hapa ndo inadhihirika wazi kabisaaa.Bravoo mkuu
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Feb 5, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 13,577
  Likes Received: 6,714
  Trophy Points: 280
  ..hoja ya kutumia kitabu kimoja cha kiada nchi nzima ni agizo la Raisi Kikwete wakati alipotembelea wizara ya elimu. suala hili baadhi yetu tulishalisemea hapa jamii forums.

  ..hoja za Prof.Maghembe alipokuwa backbencher ni tofauti kabisa na sasa kama Waziri wa Elimu. huyu Mzee kasoma na amefanya kazi nchi nyingi tu kwa ufanisi mkubwa tu.

  ..nadhani tatizo ni Raisi tuliyenaye. kila msomi aliyekaribu naye mfano Dr.Kawambwa,Prof.Msolla, Prof.Maghembe, wote wanashindwa kumsaidia.
   
 8. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,778
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 180
  ukitaka kujua huyu waziri ni kichwa maji,ungeona jibu lake kuhusu suala la prof Baregu leo asubuhi..
   
 9. m

  miner Member

  #9
  Feb 5, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu si kitabu kimoja yamekuwepo malalamiko mengi kuhusu mfumo wetu wa elimu na suluhu ni kuwa na mjadala wa kitaifa wa namna bora ya kutoa elimu. Mfumo wa elimu umeoza na Maghembe hawezi kuleta mabadiliko. Vitabu ni tatizo Walimu wetu jee? Wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ni wale ambao hawakufaulu vizuri ni tatizo na matokeo ni kufeli mitihani ifike mahali tuseme inatosha kwa watawala wa leo.
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,147
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Mimi sioni tatizo kabisa, na wala hatukupaswa kumtusi kiasi hicho Prof. Maghembe kuhusu uwezo wake wa kufikiria. Hajasema kitabu kimoja tu ndo kitatumika mashuleni, bali anaongelea kitabu cha kiada. vitabu vya ziada vinaweza kuwa vingi tu lakini hivi vyote vitakuwa vinaongeza ujuzi kwenye kile kimoja cha kiada.
  Lakini pia kumbukeni kwamba mfumo wetu wa elimu ni centralized. katika centralized system of education, tunatarajia kwamba watoto wote katika nchi nzima wajifunze kitu kinachofanana, wasome kitabu kinachofanana, na katika mazingira ya kujifunzia yanayofanana, kwa kuwa wanafanya wote mtihani mmoja/unaofanana. Japokuwa mazingira ya kujifunzia hayafanani kwa kiasi kikubwa sana, lakini bado naona umhimu wa kuwa na kitabu kimoja cha kiada. Vinginevyo watoto wa masikini kule vijijini, wanaosoma katika shule zetu za kata zisizo na uwezo wa kununua vitabu vingi mbalimbali wanaweza kujikuta ni wa kufeli kila siku na wengine wanafaulu.
  Kwa mtazamo wangu, ni vizuri tuwe na standards zinazofanana. Binafsi nampongeza kwa mtazamo huu, ameanza vema na ningependa sasa aandae mazingira ya kujifunzia sawa kwa watoto wote nchini.
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Feb 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  sasa katika kuthibitisha hekima na busara yake ni ndogo kiasi gani , jana kaleta kituko cha mwaka, akiongea kwa jiamini bungeni, mara akafyatuka na majibu ya hovyo zaidi juu ya sakata la proF Baregu.....akidai kuwa BAREGU HAKUPEWA MKATABA MPYA KWASABABU KUMEPATIKANA MWALIMU MWINGINE WAKUFUNDISHA SOMO HILO... kwa kauli hiyo alikuwa akipingana na Waziri wa ofisi ya Rais Utumishi juu ya sababu za Baregu kunyimwa mkataba.
  na zaidi nammbishia mkuu wa Idara ya sayansi ya siasa UDSM kua Baregu hana mbadala labda mpaka hapo watakapo pata mwalimu mwingine....
  Elimu na ufahamu wa Maghembe utatia shaka, kiwango chake cha kuchakata mambo kiko too low, kweli ameingia darasani lakini hajaelimika.
   
 12. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 8,013
  Trophy Points: 280
  Alitoa jibu gani?
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,455
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Alisema Prof Baregu anang'ang'ania UDSM kwa kuwa malipo pale ni mazuri, eti vinginevyo angetimkia nje. Huyu ndiye msomi wetu Maghembe!
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Feb 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  bado namtizama Maghembe kama matunda ya wanafunzi wanaokariri sana darasani, hawezi kuongea vitu vyenye mtiririko. hawezi kuchangia hoja kama waziri msomi...hana hata hadhi ya kuwa katibu kata.
   
 15. B

  Bumela Senior Member

  #15
  Feb 6, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nami katika hili la kitabu kimoja naliunga mkono kwa sana, labda iwe mantiki hatujailewa hapa.Kitabu cha kujibia mitihani kiwe ni kimoja lakini kwa kuelewa mwanafunzi hazuiliwi kusoma na vitabu vingine. Hapa Mkuu naungana na wewe wanafunzi wote tuongee lugha moja tz nzima. Lakini vikiwa multiple Ufisadi huooooooooo.
   
 16. w

  warea JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri aliyeleta mada hii ni mdau wa wale jamaa wanaotuuzia vitabu visivyokidhi mahitaji ya watoto wetu. Sasa baada ya kuona biashara yake inaelekea kubuma anaanza kumsakama profesa. Profesa ni mtu aliyepitia changamoto nyingi sana katika fani yake kuanzia huko tulikoanzia shule za kijijini hadi chuo kikuu na kuzidi. sisemi kuwa hana mapungufu kama binadamu, ila si kwamba hajui anachokisema. Mtihani ni kama mashindano, au kama biashara - kuamua nani aitwe mshindi lazima uweke mazingira sawa kwa kila mshindani. la sivyo kila shule iwe na mtihani wake wa kumaliza shule.
  Huwezi kumfundishia mtoto kwa kitabu ulichotunga wewe, na mwingine akafundishiwa na kitabu alichotunga profesa Maghembe, halafu wote uwape hao watoto mtihani mmoja ambao huenda utakuwa na maswali mengi ya kitabu chako, ukategemea wale wanafunzi watalingana katika kuelewa mazingira na maswali ya mtihani.
  Kama unaona maprofesa hawatusaidii ni kwa sababu hatuwasikilizi ushauri wao. Mara ngapi tunaamua kuanzisha miradi bila kuwauliza maprofesa. Mara nyingi wakijadili vitu wanatazamwa kwa jicho la kuwanyamazisha.
  Sasa kwa suala hili sijui kama wamejadili kwenye paneli za wadau wa kufundisha. Lakini mimi naona ni zuri. Namuunga mkono profesa
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,973
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 145
  Alikuwepo Mungai kavuruga weee mitaala mashuleni.
  Kaja huyu nae anavuruga weeeee Elimu sielewi jamaa elimu yake Prof. ni kama akina Prof. Maji marefu?
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,734
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hapana Mkuu. Tatizo ni mataalamu kama hawa ambao badala ya kushauri wao wanatekeleza tu. Kama anaona agizo ni la kipuuzi kwa nini basi asilipinge au ali-ignore? Yakimzidi si achie ngazi angalau heshima yake ikiwa hai? Mimi naanza kuwa na mashaka na hayo mataasisi ya kimataifa ambayo hawa wasomi wetu wanasifiwa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa! Haiwezekani ufanisi huo ukapotea wakija bongo tu. Pengine kule nako walikuwa wanabebwa.

  Sasa huyu msomi atawazuia wanafunzi ku-google? Kama alivyoulizwa, hivi elimu ni kupasi mitihani tu? Ikiwa mitihani inatungwa kutokana na kitabu basi ajuaye maswali yote yaliyomo kwenye kitabu si atapasi bila hata kujua yanapatikana vipi? Inaelekea tunataka taifa la 'crammers' si walioelimika.

  Amandla......
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Feb 6, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,524
  Trophy Points: 280
  Huko kwenye mataasisi ya kimataifa hawa wasomi wetu wa Kiafrika mara nyingi hufanya kazi chini ya wazungu. Kama hawako chini ya wazungu basi huwa wanazungukwa na wazungu wengi sana. Wakirudi Afrika inakuwa an all African affair na matokeo tunayajua. Kwa mfano yule Balali tuliambiwa eti alifanya kazi kwenye shirika moja kubwa la kifedha duniani huko Marekani. Lakini aliporudi bongo kuwa gavana wa benki kuu tuliuona huo ufanisi wake jinsi ulivyokuwa maridadi.
   
 20. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanx brother,labda mtoa maada hakumuelewa professor alikuwa anamaanisha nini anaposema kitabu kimoja nchi nzima.
  Mimi naunga mkono hoja ya kutumia kitabu kimoja (kwa vitabu vya kiada) ila pasiwe na restriction kwa vitabu vya ziada(broad learning).
  Enzi zetu za juma na roza,mussa na neema,mr&mrs daudi,kibanga kampiga mkoloni,manenge na mandawa n.k. nchi nzima ilikuwa inaimba wimbo mmoja kitaaluma.Na yule mwenye uwezo mkubwa kiakili aliweza kudhihirisha uwezo wake hata kama anasomea kijiji cha kumpekenyela.Na ni wazi,mianya ya rushwa katika sector ya elimu ilizibwa kwa kiasi kikubwa.
  Wafuasi wa mkapa, tambueni huu mparanganyiko wa elimu ya tanzania uliletwa kwa makusudi na MUNGAI kwa maelekezo ya bwana wake Mkapa.Leo tutamlaumu Kikwete na Maghembe.
  Naunga mkono kuhusu uwezo wa prof. Maghembe.
  Hastahili kuitwa proffesor kwani hajaelimika na hana uwezo wa kuchanganua mambo...
  But i dont know what is he proffessing,,may be antques
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...