Upeo Mdogo wa Wajumbe CUF ndio Tatizo- Profesa Safari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upeo Mdogo wa Wajumbe CUF ndio Tatizo- Profesa Safari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Babuji, Mar 4, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Mar 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAPINZANI wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni Profesa Abdallah Safari na Koplo Stephen Masanja wamesema kushindwa kwao katika uchaguzi huo kumechangiwa na upeo mdogo wa wajumbe.

  Wakiongea kwa nyakati tofauti na Nifahamishe walisema kuwa wamesikitishwa na aina ya wajumbe ambao wanawakilisha wanachama kwani wanaonekana watu wa kupikwa kwa ajili
  ya kutetea mtu fulani na kukashfu wengine.

  Profesa Abdallah Safari alisema ni vigumu vyama vya upinzani kuchukua Serikali kama aina ya wanachama ni kama hao ambao wapo chama cha CUF ambapo amewaelezea kuwa wanahitaji kupatiwa elimu ya urai kwa maslahi ya chama na Taifa.

  Safari alisema alikuwa akidhania kuwa uelewa wa wanachama wa vyama vya upinzani mdogo hali ambayo imedhihirika katika uchaguzi uliomalizika ambapo
  walishindwa kuuliza maswali ya msingi kwa maslahi ya chama na kujikuta waletakejeli.

  Profesa Safari alisema wajumbe wengi wa mkutano mkuu wa CUF wameonekana kama mamluki hivyo kushindwa kusimamia misimamo yao na kujikuta wakiwa watumwa bila kujitambua.

  Alisema katika mkutano huo wajumbe walionekana kukosa ubunifu na uamuzi makini hivyo kujikuta wakibakia katika mfumo wa baadhi ya vyama ambavyo havitaki mabadiliko.

  Safari alisema ni jambo la ajabu katika ulimwengu huu wa sasa kukuta uchaguzi unafanyika na kuwarejesha viongozi wote ambao wanamaliza muda wao huku chama kikiwa hakina mwelekeo.

  "Nilikuwa nafikiri kuwa chama chenye watu wanaotaka kukaa madarakani hata kama hawajafanya lolote ni CCM lakini hata huku CUF wapo wengi," alisema.

  Kwa upande wa mgombea mwingine katika nafasi hiyo ambaye alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 10 Koplo Stephen Masanja alisema ili kuleta mabadiliko ya kweli ni vema katiba ianishe kipindi cha viongozi wa ngazi za juu ili kuchangia mafanikio na kuleta mabadiliko.

  Alisema kutokana na mfumo huo na ulewa mdogo wajumbe unaweza kuchangia watu wengi kuongoza kwa muda mrefu bila kufanya chochote hivyo kukigharimu chama.

  Mkutano huo ulimalizika mwishoni mwa wiki kwa Profesa Ibrahimu Lipumba kuibuka mshindi kwa kupata kura 646, Koplo Masanja kura 10 na Profesa Safari kura sita


  Source: Nifahamishe.com
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kheeeee heeeeee heeee! Habari ndio hiyo!
   
 3. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ha,ha,ha, maskini Profesa hakujua kwamba hii ni SI HASA
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  sasa nini kifanyike kuongeza upeo wajumbe wa CUF?
   
 5. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Profesa angeshinda, angetoa hii kauli ya dharau kwa wajumbe wa chama chake?

  Duh! wasomi wetu bana..
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Sio wa CUF tu...ni kambi yote ya upinzani...
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yaani sizitaki mbichi hizi , halafu hajayasema yote kama Blue gurdz wamemshitukia ni pandikizi la CCM ,na ndio maana yake ,huwezi kuwa mwanasiasa ukikosa ukaanza kulalamika ,hivi aulizwe hilo analolisema hakulifanyia uchunguzi kabla ya kuomba kugombea eti wajumbe wana upeo finyu ,upeo finyu kwa kuwa hakuchaguliwa ,pole sana ,yaani mtu wenyewe ameibuka tu kama uyoga hana hajulikani ,mimi sikuwahi kumsikia hapo kale ,kwa kweli kama wagombeaji basi wapo ambao wangejitokeza wangeliweza kutoa ushindani lakini si kwa mtu ambae wacha wajumbe wananchi hawamjui wala hawajamsikia au kumuona kwenye majukwaa na umaarufu labda angetokea katika uongozi fulani au akiongoza jambo fulani na kuvuma hapa Tz ,ili watu wamuelewe.
  Pia kama yeye alikuwa ni mkereketwa wa CUF au anaipenda Chama ya CUF rohoni mwake asingeweza kutoa na kusema utumbo kama anaoongea hivi sasa zaidi anajishusha hadhi na asifikiri kuwa ataiathiri na kuisababishia CUF kutoeleweka zaidi ,kwa hapo alipofikia kila mtu anamuona ni mtu wa ajabu ,wale waliojitokeza kumpa sapoti au kumshangilia kila anaponafasika na kurapu ni kama wanamshangilia mwendawazimu.
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  CUF wanaojulikana ni Seif na Limpumba wengine hapana..ni hii ndo demokrasia ya CUF!

  Kwa hili tu CUF kupewa tiketi kuongoza nchi basi tusahau! Afadhali CCM na CHADEMA wana desturi kubadili viongozi wa juu!
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ni bahati mbaya sana kuwa Prof Safari ndiye mwenye upeo mdogo. Kama ameshindwa kusoma upeo wa wajumbe wa kamati kuu ya CUF, ataweza vipi kusoma upeo wa wakazi wa Dar es salaam au wa Tanzania ka ujumla? Anapaswa kukaa kimya kwanza ajifunze hayo ndio agombee tena!!
   
 10. B

  Babuji Senior Member

  #10
  Mar 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Profesa Ibrahimu Lipumba - Elimu - Phd Uchumi - kura 646,
  Koplo Masanja - Elimu - Kidato cha nne - kura 10
  Profesa Safari -Elimu - Phd Sheria - kura 6
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio matatizo ya Sultan CCM hayo kutaka mambo ya wengine yasijulikane ,maana hata Tanganyika kuna watu hawajui kama Nyerere ameshafariki kitambo. :D Kiasi munaiona bora CCM kwa sera za ajabu za kuwataja majambazi katika kisanduku cha kura :D ,jamaa katika kura yake kaandika Mzalendohalisi ni mwizi na anaua maalbino. serikali ya Sultani CCM itakuwa imeshapata ushahidi :D
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Unajua hata wewe ni miongoni ya wale waliokandiwa na Profesa Safari...:D
  Pole Yakhe!!!
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  Nilisema ni uchaguzi zuga. Prof. Safari ana ulimi wa upanga wa makali kuwili. Atatema cheche zitalipua moto utakao iunguza CUF.
  Tayari Maalim keshatangaza nia ya kugombea ZnZ. Bado Li- Pumba. Hadithi itakuwa ni ile ile, mwafaka ujao ni 2015.
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa huyo sio jambo la kushangaza, ana deni la kulipa, hivyo piga ua lazima agombee tu!
   
 15. C

  Chuma JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwiba kujulikana sio sifa makini...Mkapa hakuwa anajulikana....Sumaye hakuwa anajulikana "kwa mtazamo wako"...ulitaka Safari aimbe taarabu...?

  Akina Lipumba na Seif wanajua who is Safari na ndio maana wakapitisha Jina lake liwepo ktk Mkutano Mkuu...Safari kasulubiwa kwa kuwa tu alikwenda kuwatetea akina Lipumba...Leo hii unamwita pandikizi!!!....Bwana Mdogo acha dharau...au ndio wale walio na upeo Mdogo...? u need to grow kaka!!!!

  Kesi ambazo tunazo kwa viongozi wetu hatutaki kuambiana ukweli na tunaoena Aibu...anachosema safari ni Jambo Sahihi...

  kama CUF mpo serious Gazeti lenu lipo wapi....?...Website yenu inakaa hadi kujaa pono...? unataka nani aje akufanyie kazi hizo...? yaani kumlipa hata web Admin pekee hamuwezi...?...Vipi unaweza kuja kuongoza siasa wakati Tools za propaganda huna...? Wenzenu wameweka hadi vyuo kufundisha watu namna ya kuhubiri siasa yao...!!!

  What i can see ktk vyama vyetu vya siasa vyote...kumejaa watu ambao tunasema materialist au ma-oppurtunist...!!!
   
 16. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2009
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Jamani kuna umuhimu wa kujifunza upya kuandika report, sasa muandishi unapoandika quote after quote si bora ungetuwekea script ya interview au recorded tape. Huu ni uandishi wa kina chilambo wa miaka ya 60s, "muheshimiwa raisi alisisitiza watu waendeleze kilimo cha mkono, akizungumza na wananchi wa kata ya sikonge".

  Unapoandika habari unatakiwa kufanya analysis, kuchukua data ambazo umepokea then una develop information kutoka kwenye hizo data kwa kutumia analysis. Na sio kutuandikia quote mpaka quote.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hata kama aliwatetea ,haina maana kuwa akubalike katika kuiongoza CUF,unaweza ukajikaribisha na kuonekana mwema sana pingine kushinda mitume lakini ukawa una agenda za siri kuliko firauni ,hivyo ndivyo ilivyo na ushahidi ndio unaoonekana kuwa jamaa siku ya pili tu baada ya kukurupushwa anapanga siku ya kuzingua kitabu,hivyo alikuwa tayari ameshajua matokeo na ameshajua kitakachotokea hivyo hakujitayarisha kugombea tu bali kutafuita sababu ya kupakazia na sababu ndio hiyo ameshaipta mwache atimize azimio la kitabu chake ila sidhani kama atapata wasikilizaji na wasomaji zaidi ya Wafuasi wa Sultani CCM :D sasa mnaonaje mkampa kazi ya uenezi wa propaganda za Sultani CCM kama Tambwe hiza !
   
 18. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Mhmh haya sasa .unajua wapinzani si lolote si chochote.Wakishika nchi tutajuta na kusema aheri SISIM
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nilazima ujute maana itakuwa hakuna tena chauchau ,na kila kitu kitafuata mkondo wa sheria ,rushwa za mabilioni zitakuwa na grade ya uhaini ,polisi atakaejulikana kabambikiza kesi ataenda jela ,yaani kutakuwa na sheria uchwara kibao ambazo zitakufanya uogope hata kutupa karatasi,hapo ndipo utakapoona kuwa bora utawala wa Sultani CCM ukiweza kufungua dirisha kumwaga machicha.
   
 20. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hoja ya Prof.yafaa kujadiliwa kuwa upeo mdogo wa wajumbe wa Mkutano Mkuu ndio ulikuwa kikwazo kwake , je? upeo huo ndio ulikuwa mtaji kwa Prof.Lipumba?
   
Loading...