Upendo wa Wamama kwa Watoto ni wa Kinafiki??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upendo wa Wamama kwa Watoto ni wa Kinafiki???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SnowBall, Aug 30, 2012.

 1. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wanajamvi salaam!
  Ni kawaida sana kwa wanawake walioko kwenye NDOA kuwa na mapenzi makubwa na watoto wao. Wengine hudai kibaolojia urafiki wa mama na mtoto uko 'strongly linked' kuliko ule wa baba..husema wamama wana stake kubwa sana kwa watoto kuanzia mimba, ulezi na pengine hata ukuaji wa watoto wenyewe...Lakini hii pia haiondoi dhana ya uwepo wa mama wakatili kwa watoto. Mfano tumeona wanawake wengi tu wakitupa watoto wao wa kuzaa wenyewe majalalani au pia wanawake kutesa watoto wao wa kambo. Kiufupi yote yanawezekana..i mean mwanamke kuwa mkatili au mpole katika nature yake.

  Kutokana na jamii kuwa na mentality ya namna hii ndio maana tunasikia 'slogan' kama 'hakuna kama mama' na nyingine zinazofanana na hizo. Lakini hali ikiwa hivyo kwa kina mama sidhani pia kama ni sahihi kusema wababa hawana mapenzi kwa watoto wao as walivyo wamama..Manake pia tunaona katika baadhi ya familia watoto wakiwa wanawapenda wababa zao kuliko pengine mama zao..Vyovyote iwavyo inawezekana katika mazingira flani upendo wa baba ukawa mkubwa kwa watoto kuliko wa mama au saa zingine kinyume chake.

  Lakini hali ikiwa hvi ni mara nyingi utasikia kwenye mahusiano yanayolegalega wanawake wakisema 'Yaani naishi naye kwa ajili ya watoto tu'?..It means upendo unakuwa umekufa ila kwa vile kuna watoto wamama wanakuwa wanaishi na wenzi wao alimradi tu siku ziende..It means wapo tayari ku'sacrife' anything kwa ajili ya watoto. Kwa wababa ni nadra kusikia hili..pengine nalo lipo hapa sina uhakika sana..

  Hebu sasa niwaulize wamama/wababa kama mko tayari kuishi na wenzi wenu kwa maisha ya kuungaunga yasiyo na furaha kisa mnalea watoto...JE? KWA NINI MNASHINDWA KULEA WATOTO WA KAMBO???..Au nyie ni wabinafsi na wanafiki tu kwa watoto mliowazaa wenyewe???..Kumbukeni uchungu uliokushika wewe ndio uliomshika mwanamke mwenzio!!!Ukiwa na upendo kwa watoto kwa nini ubague labda tujiulize upendo wa mama kwa watoto ni wa kinafiki???

  Nawasilisha!
   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Yaani heading na content ni tofauti sana, sijui lengo lako hasa ni nini?
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni sawa na kushangaa kwanini mtu anamdhulumu mwenzake mali zake, kwani jinsi alivyozihangaikia ni sawa na wewe ambavyo unahangaikia za kwako.

  Kitendo cha mwanamke kuzaa na kupata uchungu hakihusiani na uzuri au ubaya wa roho yake; hata kama tukipenda iwe hivyo.

  Binadamu ni binadamu ana both good and evil side, with help of imani (dini) one can supress evil side.
   
 4. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kaunga sio kweli ....heading na content ni sawa kabisa.....

  Kwa kuongezea kuhusu unafiki wa hawa wamama....huwa wanapenda watoto wao wenye pesa tu...Na huwachukia wasio na pesa....
   
 5. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  pacha please edit hiyo title !kama kaunga hapo juu mi wala siiungi mkono title hiyo na kilichomo ndani twinie!!
   
 6. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  una lako jambo....
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Kusuhu kulea watoto wa kambo si rahisi kama unavyoliona.

  Kwa mtizamo wangu, baadhi ya watu wanashindwa kulea watoto wa kambo kutokana na mazingira waliyokulia na kitu kilichojengeka akilini mwao.

  Nitarudi hapa sababu mie, sina tatizo na kulea mtoto wa kambo niliyemkuta kabla ya ndoa na aliyenikuta baada ya ndoa.
   
 8. steveslove

  steveslove Senior Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nashkuru sana mtoa mada, mada yako nzuri sana though uliyoongea ni maswali na majibu kabisa.
  kama ulisema kuhusu wa mama kulea wana wa kambo baba unahusika kwa kiasi kikubwa kama wewe ulizaa mtoto na mtu mwingine ukaamua kumleta alelewe na mtu mwingine hilo ni dhahiri ushamchunguza mkeo na kujua anafaa kwa mtoto si wake. Hapa umejicommit kwakutaka kuwa baba bora na unayempenda mwanao asipate tabu ukamleta kwa family unatakiwa kuhakikisha yule mtoto anastahili kupata kila kitu kama watoto wako wengine ukifail akiteswa ni wewe ndio sababu ni ukamwacha kwa mama yake ukapeleka huduma huko mtotot akaishi kwa amani.

  Nakuja kwenye mada, mwanamke kumpenda au kuchukia mtoto wa kambo hii inatokana na hulka au situation unayoishi na mkeo. U cant change ndio maana ww baba uwe makini kuhakikisha mtoto wa kambo analelewa vizuri as mnakua mshaongea na mwenzio mkakubaliana na umeona ndio sahihi endapo utajiamulia ndio matatizo yanaaanza mwanamke hasira zake kwako zooote anamimina kwako, utakuta mkeo umemletea yule mtoto we unatesa na mama yake huyo mtoto unatarajia nn lazima amtese coz ww ndio utaumia huko au ndgu wa mama wa mtoto wa kambo wanakuja kumsumbua mkeo lazima iwe problems

  So hata nyie wanaume mnasababisha watoto wa kambo kuteseka hampo makini
  Pia usisahau hata wa baba wa kambo wapo wa roho mbaya naona umesisitiza sana kwa wanawake wapo baba kibao wanabaka na kulawiti watoto wa kambo so hii bwana inahitaji mazungumzo kati ya wazazi watatu mkubaliane mpeane masharti then ndio mumlee mtoto wa kambo tena kama bababa u v to be very careful kuhakikisha mwanao analelewa vyema
   
 9. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  mie sioni tabu kulea mtoto wakambo as long s anafata sheria kama watoto wenzie nyumbani...
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wa mama wa Kileo mapasua wa zamani siyo wana.... now days vururuvururu tu
   
 11. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kaunga sidhani kama nimeshindwa ku'convince'..
  Jaribu kusoma between lines utaelewa namaanisha nini..
   
 12. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nashukuru umenisoma japo kwa upande huu..
   
 13. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ahsante Boflo naona wewe umenisoma..
  Kuna kaunafiki flani kwa wamama bana kuhusu upendo kwa watoto..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Pacha hebu irekebishe tu title kwa mtazamo wako na uchangie kwa vile unavyoona wewe ni sahihi..
  Binafsi naona kama ukinisoma taratibu utanielewa nilikuwa namaanisha nini..
   
 15. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Rudi bana Kongosho useme kitu..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Vipi kwa kina baba ambao wanatembea na mabinti sawa na age ya watoto zao? Tena wengine hawaendi mbali, wanakula mabinti wa wake zao au hata mahouse maids wao?

  Ubaya hauna jinsia, na mtu akichagua wa kumtendea wema si kwamba ni mnafiki.

  Wanaotesa watoto wao ni wabaya fulstop!
   
 17. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  steveslove nimefanya msisitizo kwa wamama kwa sababu inasemekana wamama ni wapenzi sana wa watoto..
  Na pia inasemekana wamama wanaweza kubaki kwenye ndoa hata kama ya mateso kwa ajili ya watoto..
  Sasa kwa kuangalia huo upendo mkubwa walionao wa wamama kwa watoto ndio nikawa najiuliza mbona kwa kiasi kikubwa ndio wanaoongoza kuwatenda vibaya watoto wa kambo...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe Kaunga kuwa ubaya hauna kwao..Ila inaweza kuwa inasikitisha sana pale mama mwenye watoto nyumbani kubagua katika malezi kisa watoto wengine sio wa kwake..i mean hakuwazaa yeye. Na hapo ndio mimi nauita unafiki. Nina mifano mingi ambayo nimeiona na mimi mwenyewe ni mwathirka wa mfumo wa malezi ya mamawakambo. She mistreated me in a way hata watoto wake wakawa wanamuambia kwamba she was not fair..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. steveslove

  steveslove Senior Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yap nimekuelewa yan bwana mwanamke ukisha mtreat vibaya kwakweli hawezi lea mwanao kwa upendo hata kidogo kwa hili baba unatakiwa kuonyesha appreciation kwa mkeo ukileta mambo asiyoyapenda baaasi so wengi wanawake wanaowatesa watoto wa kambo chanzo ni baba, mama mzaz wa mtoto wa kambo au ndugu na majirani pia. but mwanamke kama mwanamke sidhani. me ninaproof ya baba alioa mke wakaachana walizaaa mtoto mmoja,mtoto akakua akafikia kupata komunio (kikatoliki) bas yule mama akamualika baba mtoto yule bbaa mtoto alikuja na mwanae ambae amezaa na mwanamke wa sasa lakini mke wake wazamani alimpa mahali pakulala ila tule baba alimhudumia mwanae aliyekuja nae mwanzo mwisho as ni mdogo yupo kama 4yrs so huu baba me nlimpenda alijua wht is best for his son kwa mama wa kambo.

  so kina baba wasifikiri ukimshamletea mkeo mtoto wa kambo basi ndio umemaliza noooo lazima uhakikishe usalama wake
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sababu ni 1 tu kwamba KWANINI ULIMWACHA MKEO UKAMFATA MWANAMKE MWINGINE,MKAFANYA MAPENZI MPAKA MKAPATA MTOTO,hii ndo chanzo cha manyanyaso kwa watoto wa kambo walozaliwa wakati tayari unamke na watoto,Mara nyingi wanawake hawanyanyasi watoto wa kambo waliowakuta wamezaliwa kabla wao hawajaolewa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...