Upendo wa MAMA kwa WANAE

Nilipokuwa mdogo nilikuwa naona kila kitu ni rahisi maana kitu pekee nilichohitajika kusema ni mama naomba hiki; mama nataka kile na mama sitaki hiki. Kama mfalme yote nilitimiziwa. Leo nimebahatika kuwa mtu mzima na kuweza kuyafahamu maisha kwa jinsi yalivyo; ni kitu kimoja ambacho kila siku huwa nakiongea katika sala zangu na katika maongezi ya kawaida: Namshukuru Mama yangu kwa upendo wa kweli na kwa kujitolea kwake kutulea sisi. Leo tumekuwa watu wazima na katika umri alio nao ni faraja sana kwetu kwa kuwa tumekuwa na uwezo wa kumwangalia na kumtunza.

Shukurani kwa Mama nimekulia katika malezi bora na mema nikimjua Mungu na kufahamu thamani ya utu. Nampenda.
 
nampenda sana mama yangu zaidi ya sana ni mwanamke jasiri sana. Baada ya baba kufariki miaka 18 iliyopita alimwachia watoto sita na wamwisho akiwa na 2month, alinyang'anywa kila kitu had kad zetu za clinic, hakuwa na elimu so kazi pekee aloweza kuimudu ni uhudumu wa baa yan baamed amefanya hyo kazi kwa miaka 15 tukisoma, kula, kuvaa kwa taabu sana, had leo hii mm ndo nimekuja kumpumzisha na hyo kazi, lastborn wetu anaingia 4rm 4 mwakani,

Naheshm sana mabaamed coz ndo kaz iliyonikuza na kunisomesha,, nampenda sana mama yan sana nashndwa hata kujielezea..
Kwa wale wanaodharau hawa mabaamed sio wote walipenda ama kujitakia kufanya hyo kazi wengne nishda 2.
 
ni kiumbe pekee anayeweza kusacrifise na kusafa kwa ajili ya watoto wake, i love u mom
 
Kwangu mama ndo shujaa wangu wa kwanza katika dunia hii,,, hao wengine ndo wanaofata
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom