Upendo umepungua kwa wanandoa wa siku hizi au ugumu wa maisha unachangia?

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,014
12,278
Asalam alaykum warahmatullah wabarakatu

Ndugu zangu hongereni kwa kumaliza mwezi mtukufu wa ramadhan na kusherehekea sikukuu kuanzia juzi Jana na leo yote tunasema mungu ndo mjuzi wa yote.

Katika kusherehekea sikukuu kuna kitu nimeona hakipo sawa hasa kwa wakazi wa Dar es Salaam,

Zamani kipindi tunakuwa sikukuu ilikuwa inaheshimika na siku kubwa sana kwa familia na kwa watu wote kwa ujumla japokuwa siku hizi mambo yapo tofauti kidogo.

Hali ya mtaani inaonyesha ndoa nyingi watu wanaishi kwa mazoea kuna matukio yanafikirisha sana wana ndoa wanaenda kutembea ila kila mtu, ni kama amelazimishwa kutoka vile maana unakuta mmoja yupo mbali sana na mwenzake kama hawaendi safari moja mpaka kwenye kuvuka barabarani hakuna hata anayemuangalia mwenzake.

Barabarani sasa utakuta mama ana watoto watatu au wanne anahangaika mwenyewe kuwavusha na hili kundi wapo wengi sana mpaka mama unamuonea huruma unaamua tu kumsaidia kuwavusha wengine, kwenye usafiri sasa ndo shida kabisa yaani mama anagombania gari huku ana watoto watatu au wanne kina baba hawaonekani kabisa.

Hata kama hali ni ngumu na wanaume wapo bize kutafuta hela lakini siku ya sikukuu wakulungwa tujitahidi kuonyesha uwepo wetu kwa familia, maana haya matukio kwa mwaka yanatokea mara moja tu tusiwaachie kina mama watoke na watoto peke yao hata kama hujisikii kutoka au huna ratiba hyo ila fanya kwa ajili ya familia.

NB: Mlio kwenye ndoa wapendeni wake zenu msiwaache watoke wenyewe siku za sikukuu kwani mateso wanayopata na watoto ni makubwa sana.
 
Kichwa cha mada ni kizuri ila content sasa, bandiko lako nafananisha na kitabu chenye jina zuri kwa nje ila ndani ya kitabu muandishi hajalitendea haki jina la kitabu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom