UPENDO... Hivi umepotea kiasi hiki????

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,190
18,076
Leo nimeumia mno na tukio moja la kusikitisha.... Roho imeniuma mno....

Kijana mmoja anaeishi na babake kafariki kwa mda wa sikut zaidi ya tisa ndani bila kutambulika... In brief huyo kijana anaishi hapo na babake...
inasemekana kua alikua anajisikia vibaya hivo akaenda hospitali... siku ya mwisho kuonana na babake alikua kamuaga babake kua anaenda kuchukua majibu (lab results) hospitali....

From assumption inaelekea siku hio kijana alirudi akajiliza na kufariki siku hio hio... Amegundulika baada ya babake kumgongea chumbani kwake ili eti aazime dish lililokua chumbani mwa huyo kijana - only to find hakuna response na harufu kali.. In short.. kafariki ana siku tisa... Huyo baba katiwa ndani....

MASWALI NINAYO JIULIZA....

  1. Jamani tumefika hatua ya kusema hatuonani na mtu wa nyumba moja zaidi ya week na wala usifuatilie huyo mtu anaendelea vipi?
  2. Huyo kijana alikua na hali gani??.... inasikitisha mno kufikiria labda alikua na kiu... maybe njaa.... Mpaka anafariki...Dah!
  3. Huyo anae ishi nae ni babake mzazi... Huyo baba ni mtu wa dini saaana... na anajulikana kwa ushirikiano mzuri na watu.... Sasa ina maana gani ya huo ushirikiano IF YOU CAN NOT SPEAD THE SAME LOVE katika watu wako wa karibu na familia.....
  4. Hivi UPENDO umepotea to this extent???

Yaani nimeona nitoe hii story itusaidie turafakari sie twaishi vipi na watu wetu wa karibu hasa familia... Are we responsible kama tulivo kwa watu baki??? Je are spreading UPENDO vile ipasavo?? Na ni vitu gani vya ziada tunafanya kujenga ukaribu ndani na kati ya familia zeetu?? Hii habari imeniumiiiiiza mno.... I am so Sad... Dah!

AshaDii.
 
kuna kiwango cha frustration watu hufikia na kuwa kama wehu hivi
inatia simanzi......
 
I think inategemea na lifestyle yao huyo baba na mwana wanavyoishi. Kuna wengine wanakaa hata 3 days bila kujuliana hali kutokana na mihangaiko ya maisha. Huyu akiingia huyu katoka. Lakini kama ni 9 days, yes, hapo kuna utata. Itakuwaje mzazi akae asimwone wala kumsikia mwanae kwa 9 days then asishtuke hata kumjulia hali?
Dunia ina mambo
 
kuna mmoja namfahamu,alifariki ndani ya nyumba waligundua baada ya siku 5.huyo kijana alikuwa anaishi nyumba za uwani,alikuwa anaishi na mama wakambo,hakuwa akim treat vizuri huyo kijana na baba mtu nae alikuwa hamjali kabisa mtoto wake.hiyo issue ilitokea dar
 
Hii imetokea wapi hapa ulimwenguni?

Imetokea hapa hapa Tanzania... Southern Highlands....

I think inategemea na lifestyle yao huyo baba na mwana wanavyoishi. Kuna wengine wanakaa hata 3 days bila kujuliana hali kutokana na mihangaiko ya maisha. Huyu akiingia huyu katoka. Lakini kama ni 9 days, yes, hapo kuna utata. Itakuwaje mzazi akae asimwone wala kumsikia mwanae kwa 9 days then asishtuke hata kumjulia hali?
Dunia ina mambo

Dah! hata kama kweli mpo busy... ina maana mnaridhia kua mtu anaumwa usimjulie hali ili/imekuaje?? Katika hali ya uzima maybe kutoonana a day ni acceptable.. lakini personally hata tu ile ya siku mbili naona kama nikuvuka mpaka... Sijui lakini...
 
isije kuwa watoto wenyewe mateja???

kama ni mateja sishangai.....wazazi wengine huomba tu siku ya kufa ifike yaishe.......
 
kuna mmoja namfahamu,alifariki ndani ya nyumba waligundua baada ya siku 5.huyo kijana alikuwa anaishi nyumba za uwani,alikuwa anaishi na mama wakambo,hakuwa akim treat vizuri huyo kijana na baba mtu nae alikuwa hamjali kabisa mtoto wake.hiyo issue ilitokea dar

Sad. Na hili kaka/baba zetu inabidi waliangalie saana.
 
isije kuwa watoto wenyewe mateja???

kama ni mateja sishangai.....wazazi wengine huomba tu siku ya kufa ifike yaishe.......

Sielewi... ila nobody deserves kufa kifo cha kikiwa hivo ndani ya familia husika... angekua anaishi peke yake sawa...
 
hayo mauaji mbona ni kama yamepangwa wakuu?
pia inadhihirisha wazi kabisa pamoja na kuwa kiongozi wa dini lakini mmmbaba huyo ni mnafiki wa kupindukia
dini imekuwa kama eneo la watu kujificha na kupretend wana love kumbe ufedhuli wa ajabu
in fact ni kwa vile tu dhambi zetu hazijichori migongoni mwetu,, nahisi watu wasingetembea hata barabarani

inahuzunisha sana!!!
 
Inasemekana kawahi tiwa ndani for seven years (kama sikosei) baada ya
kumpiga mkewe na kusababishia kifo.. INAUMA... sina hata la kusema hapa.
 
dadangu na mamangu, maisha ck hizi yamebadilika mpaka basi. Kila mtu akiamka asubuhi ni kutoka spidi kwenda kuganga njaa na kurudi ni usiku umechoka hadi mkia. Familia nyingi ziko hivi na unaweza kuta hata baba mtu hajaonana na mwanaye wiki hadi jumamosi na j2. Twaweza kumlaumu huyo babake ila tuangalie na upande halisi wa familia tunazoishi. Mbaya zaidi itokee kuwa hiyo familia haina mama basi ni kama jehanamu. Yote tisa, kumi amekaa siku TISA unalala nyumba moja na hujastukia harufu? Yawezekana kuna kitu zaidi!

Tumwombee kijana mwenzetu apumzike kwa amani, "In God We Trust"
 
I Love this post.... ila familia inabidi tujiangalie saana... kama taratibu zetu za kusema

mwaishi nyumba moja hamuonani to that extent... then it is really bad... Inabidi tubadilike, and make an effort...
 
AshaDii,

Hii dunia imegeuka kuwa kama uwanja wa fisi...Hata sishangai ingawa huo ni unyama wa kutisha sana.

Kwa uzoefu wangu..watu wengi tunapenda sana kuonekana wema sana nje ya familia zetu.
 
AshaDii,

Hii dunia imegeuka kuwa kama uwanja wa fisi...Hata sishangai ingawa huo ni unyama wa kutisha sana.

Kwa uzoefu wangu..watu wengi tunapenda sana kuonekana wema sana nje ya familia zetu.

DC.. Asante kwa maneno yako... Moja ya my weaknesses ni kuongelea issues depressing... Sipendi maana kind of sensitive saa ingine... But niliona bora niiweka hapa kwamba walau sie at a personal level tutafakari ni jinsi gani tunaishi na familia zetu.... na wale wetu wa karibu pia...
 
Tatizo ni hali ya nchi ivyo sasa.. usione watu wanatembea .. wote wana stresses
 
Tatizo ni hali ya nchi ivyo sasa.. usione watu wanatembea .. wote wana stresses

Hii habari imeni stress mpaka inanitia uvivu... lakini hata hivo data... hilo ni mambo ya family values sio serkali...
 
Wakati mwingine ndio kuwa na baba ambae ni mzee kijana. Baba huyo hajali kama kijana wake amerudi ama amelala, matoke yake ndio hayo mzazi ana-assume kuwa kila kitu kiko ok. Lakini mzazi responsible anaekaa na mwanae ikipita 24 hrs bila kumwona basi lazima antenna zitasimama kichwani na ataanza kumwuulizia. huyu baba ni mzembe na anatakiwa na polisi awe the person of interest in this case.
Dunita siku hizi ni tafran tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom