Upendeleo wa wazi TBC Habari

Mkuu umenena vema kabisa hata mimi wamenikera,hata kipande cha Lisu kuzungumzia yaliotokea hawajaonyesha chote na maneno niliyoyasikia tu ni "ilikuwa usiku wa saa,,,,"wakakata wakaweka ya Zitto na hawakuipa hata muda wakaikata pia sasa sijui wamelazimishwa kuonyesha taarifa za Chadema!!!?.Siku Kikinuka kituo cha kwanza kukichoma moto kiungue chote ni TBC1 na ole wao

Hawa watu hawajifunzi, wind of change haiwezi kubadilishwa na uchakachuaji, tena kwa namna nyingine ndiyo kwaanza wanazidi kuwapandisha hasira wananchi na kuiongezea umaarufu.
 
Unajua naidaka TBC kupitia decoder ya dstv so nkikumbuka home huwa naweka tbc ndo nkakutana na iyo dhahma!
Unajua huwa napenda kupata updates za home siku unaweza sikia taarifa nzuri hasa pale CCM watakapotoa speech kama ya Banda/Zambia
 
Huyo MSHANA ameshindwa kazi yani siku ya ajali ya meli ndo nlihakikisha kweli TBC ni UOZO na PUMBA yani CHANEL 10(TV BINAFSI) ilikuwa bize kutuonyesha yanayojili zanzbar lakini TBC ndio kwanza wanaonyesha taarabu na MAUNO.... kazi wanayoijua ni kuRUSHA harusi na Matangazo ya Biashara kushindana na tv binafsi utadhani hawapati ruzuku..... toka nizaliwe sijawahi kuona TV ya taifa ya ajabu kama TBC (kichefuchefu)
 
TBC hawana kitu tangu Tido aondoke,yaani staff wanashida kama nini.Mishahara inachelewa ,magari ni ya kusukuma na staff wanakimbia


Nahisi kuna siku ntaenda TBC pale kudai Kodi yangu nnayolipa kwenye PAYE maana naona haitumiki kama inavyostahili!
 
Marine Hasan atasaidiwa na Efreim kiboga Kibonde

Hivi watajionaje siku watakapokuwa wanarusha matangazo ya moja kwa moja ya kuapishwa raisi anayetoka CHADEMA? Wakamuone mtu anayeitwa L. M. Mbotela wa Kenya aliyekuwa anajifanya kimbelembele kuipigie debe KANU na kuponda upinzani. Kuna wakati alihojiwa ni kwa nini KBC haitangazi habari za wapinzani (akina Kibaki wakati huo), kwa kujiamini kabisa akajibu kuwa hawajaona lolote la maana linaloongelewa au kufanywa na wapinzani, lenye hadhi ya kutangazwa. Ilipofika siku upinzani ukachukua nchi, alikumbwa na aibu kubwa kwani yeye ndiye aliyetakiwa kutangaza tukio la kuapishwa Kibaki, hivyo ilibidi awe anatoa wasifu wa raisi mara kwa mara. Yalimshuka.

Natamani hapa Tz siku raisi toka CDM anachukua nchi, Marine H. Marine apewe jukumu la kutangaza.
 
TBC bora ibadili jina na kuitwa TVCCM tujue moja,ndio sababu walimuondoa Tiddo mapema maana alikua haendani na sera zao. Habari za uhakika juu ya matukio ya campaign yanayoendelea uko igunga ni CHADEMATV tu, yani kwa hili nawasifu chadema, wako very creative, otherwise tungebaki gizani bila kujua ukweli wa yanayojiri
 
Kwani mnajua kilichomuonda Tido Mhando kwenye TN hiyo? Alitaka kufanya kazi kwa kufuata professionalism lakini Magamba wakaona itakula kwao.

Natamani ChademaTV iende public ili uozo uonyeshwe.
 
TBC wanapendelea ccm, kwa mfano wameripoti kwamba wafuasi wachadema wamevamia wabunge wawili wakat ukweli ni wabunge wa ccm pamoja na green gurd aka makomandoo koko wa ccm walitaka kuchoma magari ya matangazo ya chadema lakini jaribio lao halikufanikiwa. TBC imekua UONGO na UPENDELEO badala ukweli na uwazi. wana JF acheni kutazama habari za TBC1. ITV ndio kituo pekee kwa habari za uhakika

TBC Ilikua ya TIDO bana.Cku hizi hakuna kitu
 
Wakati wa Tido TBC iliku poa na mwonekano mzuri, lakini mambo sasa si shwari nasema haya si kwa sababu ya ushabiki, mimi nilikuwa mmoja wa wapenzi wazuri sana wa TBC1, sisi tunaotumia satelite dish pande hizi za nyanda za juu kusini kila wakati ni "signal weak" wakati mwanzo ilikuwa poa lakini sasa Ovyo na ukizingatia ni TV ya taifa yani ni Aibu tu.
 
Truly speaking TBC wanaboa. Sina imani sana kwamba ni television ya Taifa au ya serikali iliyoko madarakani. Kuhusu maandalizi ya vipindi labda tuwaundie tume. Infact wanaogopa yaliyomkuta Tido.
 
Truly speaking TBC wanaboa. Sina imani sana kwamba ni television ya Taifa au ya serikali iliyoko madarakani. Kuhusu maandalizi ya vipindi labda tuwaundie tume. Infact wanaogopa yaliyomkuta Tido.
 
Tbc- tido ndo ilikua tv station ya kuangalia,walivyoichakachua na kumpa mshana ndo yakatokea yote mnayoyaona. Nafikir itakufa pamoja na serikali yake,kwakweli napata shida sana siku hizi kuangalia tbc
 
Usiwatetee mkuu mbona taarifa za mwanzo hazikukatwa!,Kama ni tatizo la kiufundi hiyo taarifa isingeonekana kbs.Nnasikitika ITV siwapati huku Arusha.
Mshukuru mungu kwa kutowapata itv kwasababu hao ndo wamekua kichefuchefu kabisa. Jitahidi uipate startv vinginevyo ni bora kuangalia cartoon network
 
Te te te. Hivi bado unatumia TBC! Chombo hiki kinafanya kazi kwa maslahi ya 'CCM' na si 'taifa'.TBC wanachefua sana kwa mtanzania yeyote anayependa haki na usawa.Big up Tido kwani ulijaribu kuonyesha njia,Mungu akujalie maisha marefu na yenye baraka tele.
 
Acheni kulalama.mbona tbc huwaonesha sana cdm?.ingawa igunga hakuna chenu ndio maana mnaanzisha fujo.tbc habari kwa uhakika.
Twahili hivi ndo wewe mjukuu wa mvumo, unaona vibaya, tbc wanachemka waziwazi. Isaidie TBC kukua, mkurugenzi wake anaogopa kuondolewa madarakani kama aliyemtangulia. TBC ipo weak, imepoteza mvuto, mchanganya picha anachemka kila siku, mpangilio wa habari na maandishi yapitayo pale chini ni kama wanajifunza, hovyo kabisa
TBC wajipange na kuleta ubunifu, janja ya kutafuta huruma ya watawala inawaharibia wasifu wa kupata kazi za maana, msipoangalia mtaendelea kusota kwenye kuombaomba vinauli mnapohudhuria mikutano
 
Hawasomi alama za nyakati, nafikili hawana taarifa kwamba hapo kwa jirani zetu Zambia serekali imekataliwa, our days are coming. Leo jumapili wameonesha taarifa za Igunga za CCM A na CCM B tu, CDM leo haikupewa nafasi kabisa, ole wao!!
 
TBC hakuna kitu pale upendeleo wa wazi yaani TBC ni magamba machafu!
 
Back
Top Bottom