Upendeleo wa Pinda Rukwa, Jenister Mhagama amtolea uvivu Lukuvi

Jenista Muhagama unaposema, " NADHANI WALIOUNGA MKONO HOJA (KUPITISHA BAJETI) WAMESHINDA", una maana gani?
Kama unadhani je huna uhakika?
Kama huna uhakika ni kanuni gani ya Bunge inakuruhusu upendeleo upande unaohisi umeshinda?

Umeongoza vyema bunge leo lakini hitimisho la kudhania limetibua shughuli yote na hii iko kwenye record!

N.B: kumradhi sana Mh.Mwenyekiti Bungeni leo 10/07/2012, Mh. J. Mhagama kwa kukosea kulitamka jina lako linavyopaswa!

Mkuu, kanuni za bunge ndivyo zinavyosema kuwa spika, naibu spika ama wenyeviti watasema "NADHANI waliosninda....." sababu hana uhakika wa asilimia 100 isipokuwa anahisi kwa upeo wake binafsi kama binadamu na ndivyo na kanuni zinasema hivyo hivyo wala haijakosewa. Fuatilia siku zote utaona ndivyo wanavyotamka
 
Nikawaida serikali zaifu na viongozi dhaifu kufanya upendeleo kwakuwa viongozi nao wamepatikana kwa upendeleo na Rushwa na dhuluma
 
Jenista yuko sawa kabisa hivi wakuu hamfahamu kilicho mpa ulaji ni nini au mnataka magamba wamkolimbe.
 
Mazee, kama unataka kutujengea hospitali karibu sana. Marehemu Joseph Nyerere alikuwa na mpango wa kujenga modern hospital lakini alipofariki mipango yote ikaparaganyika. Hata uwanja wa ndege ni wa 1952.

Umatonya! No wonder.
 
Ni dhahiri mapungufu yaliyopo na Bunge lenyewe linayafahamu, tatizo lililopo ni kuwa watu ni wagumu kwenda na wakati kwa kuwa kuna wasisi wa kuumbuliwa kila mara. Mfumo uliopo unawabeba baadhi na hivyo wanaufurahia kuendelea uwepo wake ili maslahi yao yasiharibike.Kuna ukweli mkubwa kama utaratibu wa kupiga kura kwa kubonyeza utawekwa mijadala itakuwa moto na watu wengi watakuwa wazi kupiga kura zao kwa uwazi kuliko ilivyo sasa usipopiga kura unaulizwa.

Ifike tu wakati tukubaliane na ukweli na hiyo ndiyo demokrasia ya kweli, watu wawe huru katika fikra na maamuzi yao bila kushinikizwa na kikundi au itikadi za vyama bali maslahi ya taifa.
 
Jenista Muhagama unaposema, " NADHANI WALIOUNGA MKONO HOJA (KUPITISHA BAJETI) WAMESHINDA", una maana gani?
Kama unadhani je huna uhakika!

Ndugu ndivyo ilivyo siku zote. Huwezi kuwa na uhakika. Anaposema anadhani hatoi conclusion maana mbunge yeyote anaweza kusimama na kusema hapana. Ikitokea hali hiyo ndipo kura za ukweli hupigwa na kuhesabiwa ili kuwa na 100% uhakika kwamba wapi wameshinda
 
Mtoa mada, watu wote ndani ya nchi hii wana haki ya kupata huduma kutoka serikalini na sidhani kama hao wa kimara au Dar kwa ujumla wake, wana haki zaidi kuliko wale wa Namanyere. Huu ni ubinafsi wa ajabu kabisa kufikiri hivyo! Wale watanzania wa Namanyere wana shida mkuu kwani nayafahamu hayo maeneo, maji ni janga. Na wao pia walistahili kupata huduma hiyo siku nyingi hata kabla ya Pinda kuwa PM na kwa sababu hiyo sidhani kama ni sahihi kufikiri kwamba wamependelewa! Namanyere ni makao makuu ya wilaya ya Nkasi na kwa kukujulisha tu, ni kwamba hata umeme ambao nyie watu wa Dar mmekuwa mkiufurahia kila siku, wao hawana, ni giza totoro na vibatari mwanzo mwisho! Unataka kuniambia siku wakipelekewa umeme watakuwa wamependelewa na Pinda? Naamini wanastahili kikubwa zaidi kuliko hata hiyo bilioni 2 kwa vile wana haki ya kupata pia kama walivyo hao wa Dar.
 
Watu wote wana haki ya maji hamna anayekataa, sasa je ukiwa na pesa ya maji kwa sehemu moja tu, utachagua uyapeleke wapi? Nikiwa mimi ntachagua Namanyere walie tu ama wachimbe visima maana kuna sehemu muhimu kama Dar ambapo ni uso wa nchi yetu na hamna maji.
 
Hii ni nyuzi yangu ya pili kuhusu hili. Nakubaliana kuwa Rukwa imekuwa nyuma lkn kuisogeza sio kwa speed hii Mh. Pinda.

Leo kwenye kupitisha bajeti ya maji kama mtakumbuka Mbunge wa Namanyere wkt akichangia aliahidi kuleta basi lenye wapiga kura wake wamama ambao hawajaoga bungeni kwa siku 3. ....

My take:
Tuacheni siasa za upendeleo, ni aibu kwa jiji kuu la Dsm kila nyumba watu wamejaza madumu ya maji ndani halafu kumbe serikali overnight ina uwezo wa kupeleka maji wilaya kama ya Namanyere, sio dharau ila tuwe wakweli btn Dar eg Kimara na Namanyere kwa akili za

Acha ujinga! kwani watu wa Namanyere hawana hadhi ya ubinadamu na hivyo kutostahili kupata huduma ya maji? Umewahi kufika Namanyere na ukaona adha ya maji ilivyo! Ubaguzi gani huu! Ni vizuri ukaanza kutumia ubongo kufikiri badala ya kamasi!
 
Watu wote wana haki ya maji hamna anayekataa, sasa je ukiwa na pesa ya maji kwa sehemu moja tu, utachagua uyapeleke wapi? Nikiwa mimi ntachagua Namanyere walie tu ama wachimbe visima maana kuna sehemu muhimu kama Dar ambapo ni uso wa nchi yetu na hamna maji.
Mtoa mada ulikuwa na point..Lakn unaposema watu wa Dar ni wa maana zaidi kuliko Namanyere hapo ndio umeharibu kabisaa.Huna maana.
 
Honestly huwaga siangalii Bunge maana ni aibu tu, full of very incompetent individuals...bure kabisa...huwaga naapiga biere zangu...wacha maisha yaende..yaani mtu anafanya kitu kwa hisia badala ya taratibu na kanuni??? HOVYO...
 
Sio kwamba serikali ya CCM inashindwa kuweka VITUFE kwa kupigia kura NDIYO na HAPANA katika viti vya wabunge kama afanyavyo Oprah Show. CCM wamezoa kuchakachua kura, hivyo wanapendelea hizo kura za ku SHOUT! Ninashngaa kwanini wanawake na walemavu wa kusema/kusikia (mabubu/viziwi) hawaja lalamikia huu unyanyapaa wa waziwazi, maana madume tuna BASS. Sauti ya dume mmoja ni sawa na sauti za wanawake watatu.

But hang on little bit, kwakuwa huu unyanyapaa unafanywa na CCM na wabunge wengi wanawake ni wa VITU MAALUMU, hawawezi kusema kitu. TUnaomba wabunge wa CDM mlisema hili, muwekewe VITUFE vya kupigia kura, tuanchane na huu mtindo wa STONE AGE wa ku SHOUT as if ni MAZUZU, No wonder Dr. Mgimwa anasoma bajeti yake kwa kulamba makaratasi(lambalamba), lakini Uhuru Kenyetta anasoma bajeti yake kwa kutumia iPAD, halafu leo eti tunataka kujilinganisha na Kenya, THUBUTU!
 
Watu wote wana haki ya maji hamna anayekataa, sasa je ukiwa na pesa ya maji kwa sehemu moja tu, utachagua uyapeleke wapi? Nikiwa mimi ntachagua Namanyere walie tu ama wachimbe visima maana kuna sehemu muhimu kama Dar ambapo ni uso wa nchi yetu na hamna maji.

Hebu jaribu kufikiri tena juu ya haya unayoyaandika. Kwani pesa za maji kwenye bajeti zote zilizopita zilikuwa zinapelekwa wapi? Na hao ambao wamekuwa wanapata huo mgao katika bajeti hizo nao walikuwa wanapendelewa? Hatuhitaji kuwa wabinafsi kiasi hiki, Tanzania ni zaidi ya Dar ndugu yangu!
 
Back
Top Bottom