Upendeleo wa kijinsia kwenye makuzi ya watoto unachangia tabia ya wanawake kufanyiwa ukatili

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
414
1,027
Katika maisha yetu ya kawaida hasa sisi watu wa kipato cha chini, nasema hivyo kwa kuwa nimetokea kwene mazingira hayo, japokuwa najua hawa wale wa hadhi ya juu nao wanaweza kuwa wanahusika.

Kibongobongo maisha kwenye familia nyingi wazazi wengi na wale wamekuwa na tabia ya kutengeneza mazingira ya kuwafanya watoto wakike waonekane wao hawana thamani kubwa mbele ya wale wenzao wa kiume, hali hiyo imekuwa ikitokea katika familia nyingi.

Uhalisia huo ndiyo ambao unasababisha vijana wengi kuwa na dhana wao ni bora kuliko wanawake pindi wanapokuwa wakubwa.

Niwaambie tu wazazi na walezi kuwa hiyo siyo sawa na inachangia sana kuwaangusha wanawake kisaikolojia.

Sasa hivi watu wakiwa wakubwa, wanaume wengi wanaishia kufanya ukatili kwa wanawake na kusababisha madhara kimwili, kisaikolojia, kiafya na kiuchumi ambapo hali hiyo inasababisha wengi wao kushindwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali.

Jamii ibadilike iachane na dhana ya mtoto wa jinsia fulani ni bora kuliko mwingine.
 
Binti anafanya kazi zote nyumbani wa kiume amekaa tu wazazi wa zamani hovyo sana ndio wamekuza huo mfumo dume.
 
hamuwezi kushindana na asili ya uumbaji

cha msingi rudini kwenye mstari
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom