Upendeleo unaofanywa na Polisi kwenye foleni makutano ya Ali Hassan Mwinyi

Jadi

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
1,494
860
Jamani hii ni kero kupita kiasi pale Polisi wanapoona njia fulani ndio zina watu muhimu wa kuwahi kazini na wengine wachelewe.

Makutano ya Alhasan Mwinyi, toka Kinondoni na Coco ni balaa usipopita upande wa panapoitwa kwa wakubwa. Yaani ni waoo tuuu muda wote nyie wa kutokea Morocco na Kinondoni labda awepo mkubwa wao wa Polisi upande wenu ndio mtaitwa au mpaka waishe wote wa huko Coco.

Na inasemekana Polisi wengine huwafanyia favor marafiki zao wanaowapigia. Kwa ufupi ni kwamba Polisi wanatumia vibaya fursa hii kwa kupendelea upande mmoja au wafanyajazi wenzao au marafiki zao, taa ziliwekwa kubalance bila kujali huku kuna rafiki au la, hatusemi kuongoza magari hakusaidii ila sio siri ni kero sana hasa kwa upande usiokuwa na mvuto kwa Polisi anayeongoza.

Sijui nani huangalia uadilifu wa anayeongoza kama hatoi upendeleo, wote hatujui ila Polisi mnaboa sana kutuona wengine hatustahili kuwahi kazini bali ni wengine walioamka saa moja wawahi kisa wanakaa Masaki na sie tulioamka saa kumi na moja mnatupotezea kisa tunatoka Kimara au Mbezi beach via Kinondoni road.

Yote kutaka kuwahi halafu unamkuta mtu pale kona anakukalisha hata nusu saa eti wa Coco waishe!!!
 
Nipo ubalozi wa ufaranca hapa nina 45mins sijasogea hatua,
Jamaa wa coco beach wanapendelewa sana
 
coco beach ni wapi huko? na kwanini kuko very special namna hiyo? ukitaka kufika huko kutembelea ramani yake ipoje? natamani sana nipajue mkuu.
 
mi nilikua namtym kova mida ya saa mbili ndo hua anapita njia ya kinondon na hapo ndo wanaruhusiwa.sijui sasa iu alafu mbna hlo tatizo la zamani sana
 
coco beach ni wapi huko? na kwanini kuko very special namna hiyo? ukitaka kufika huko kutembelea ramani yake ipoje? natamani sana nipajue mkuu.
Nadhani atakuwa anazungumzia wanapendelewa watumiaji wa Barabara za Toure/Kaunda Drive na wale wa Haile Sellassie ambao ni wakazi wa Oysterbay na Masaki-- na bila shaka umeshafahamu ni kwanini ni hizo barabara!!!
 
mm mwenzio na viziaga gar za wagonjwa mkuu...nafuatilia kwa nyuma ..au ya police zile..nikibanwa sana natanua na trafic akinisimamisha sisimam...
 
Nadhani atakuwa anazungumzia wanapendelewa watumiaji wa Barabara za Toure/Kaunda Drive na wale wa Haile Sellassie ambao ni wakazi wa Oysterbay na Masaki-- na bila shaka umeshafahamu ni kwanini ni hizo barabara!!!

naomba uzidi kunifafanulia mkuu huko toure / kaunda sijui haile sellasie, oysterbay na masaki ni wapi? nipo mbali na huko dar es salaam. nitakushukuru!
 
Google Earth itakusaidia. Kenyatta Drive/Toure Drive utaziona.
 
Nipo ubalozi wa ufaranca hapa nina 45mins sijasogea hatua,
Jamaa wa coco beach wanapendelewa sana
Hiyo barabara ni kero aisee
Hio njia ilikuwa unakula timing 7.30am to 8am anapita Kova inavutwa balaa.....sasa hivi Kova hayupo! Kuna traffic niliwahi kumkomalia mbona mnapendelea njia zingine ila sio kinondoni road akaniambia 'huko mnawahi samaki feri tu acha tuwawahishe wakubwa na wenye kuwahi shughuli za maana mjini'.....
 
Nipo ubalozi wa ufaranca hapa nina 45mins sijasogea hatua,
Jamaa wa coco beach wanapendelewa sana
Pita hiyo Barabara. Kuishi mjini ni pamoja na kujua wapi wanavutwa haraka. Unaitafuta hiyo barabara though ni ndefu sana
 
Ni kweli hata mimi yamenikuta hilo eneo, kukalishwa nusu saa ni kawaida, hadi hao wa upande Wa coco wapite wote. Ndio maana wanajeshi hukosa uvumilivu na kuwalabua vibao
 
naomba uzidi kunifafanulia mkuu huko toure / kaunda sijui haile sellasie, oysterbay na masaki ni wapi? nipo mbali na huko dar es salaam. nitakushukuru!
I hope upo serious na maswali yako!!
  • Ukitoka City Center (sio Kariakoo) kwenda Mwenge unatumia Ali Hassan Mwinyi Rd!
  • About 2 km from City Center unafika eneo moja linaitwa Mbuyuni!
  • Hapa Mbuyuni, kushoto kuna pacha kuelekea Kinondoni (depending unaenda Kinondoni ipi).Aidha, watu wanaoenda/kutoka Mwananyamala wanatumia hiyo pacha.
  • Ukiingia kulia (hapo hapo maeneo ya Mbuyuni) ni Barabara ya Kenyatta ambayo ukishika, mbele kidogo inaungana na Toure Drive.
  • Hii Toure inapita pembeni mwa Bahari ya Hindi (to the north) hadi Masaki na moja ya sehemu maarufu inakopita ndo hapo Coco Beach!
  • Coco Beach ndio ufukwe maarufu zaidi kv ni open public beach-- hadi mihogo ya kukaanga yenye hadhi ya Uswahilini utaikuta!!! Hata hivyo si kwamba Coco Beach nayo ipo Uswahilini-- ipo Oyster Bay.
  • Likewise, hapo kulia ambapo Kenyatta inaungana na Ali Hassani Mwinyi ni Oyester Bay... hii Oyster Bay inaendelea na huko mbele inaungana na Masaki!
  • Vilevile kutoka hapo Mbuyuni, ukienda mbele zaidi/ukinyoosha along Ali Hassan Mwinyi (just short distance) unakuta barabara kubwa inaingia kulia ambayo ndiyo hiyo Haile Sellassie.
  • Kama ilivyo Kenyatta/Toure, hii nayo inapitia vitongoji kadhaa vya Oystebay na Masaki lakini sio along Indian Ocean kama ilivyo Toure ingawaje along Haile Sellassie kuna barabara kibao unazoweza kushika na kutokea Toure/along the Indian ocean na sio mbali.
  • Sasa why Oyster Bay & Masaki-- ni kwa sababu ndiko wanakoishi asilimia kubwa ya wafilisi wa nchi hii!!! Kimsingi majority, ukiondoa watoto wao; si watu wa kwamba huenda wakafokewa endapo wanachelewa kazini!! Huko Mwenge ni moja ya maeneo wanakoishi wavuja jasho wa nchi hii! Majority ni wale ambao wakichelewa kazini wanaweza kufokewa na hata kutiwa mangumi na mabosi wao!!! Hata hivyo, si kwamba ni moja ya maeneo yanayokuwa categorized kwamba uishi watu masikini bali ni watu wa kawaida huku ndani yake kukiwa pia na maskini wa kutosha!!!!
 
asante japo sababu yako hiyo ya mwisho imenipa uhalisia wako wa wewe ni mtu wa aina gani mkuu. kifupi acha kuwa stereotype na epuka sana fallacies of generalization na badala yake pambana ili kufikia malengo yako ya kimaisha na jipange tu utatoka.
 
Si useme tu asante yaishe.
Yaani kachukua muda wake wote kukujibu
Ka kupa details zote ulizokuwa unahitaji.

Sasa hivi unajifanya psychic.
Shukran kama yako bora usitoe.
Ya nini kujifanya unajua maisha ya mtu ?
 
subiri yataisha manake wao wanataka kujijengea daraja wawe wanapita juu ya bahari
 
asante japo sababu yako hiyo ya mwisho imenipa uhalisia wako wa wewe ni mtu wa aina gani mkuu. kifupi acha kuwa stereotype na epuka sana fallacies of generalization na badala yake pambana ili kufikia malengo yako ya kimaisha na jipange tu utatoka.
Unaweza kufafanua? Ndo maana nikaweka angalizo mapema kwamba "I hope upo serious na maswali yako manake nahisi kama haukuwa serious coz' kama unakumbuka, swali lako lilikuwa hili:
coco beach ni wapi huko? na kwanini kuko very special namna hiyo? ukitaka kufika huko kutembelea ramani yake ipoje? natamani sana nipajue mkuu.
Na ndio maana nikakupa aina ya watu wanaoishi huko ulikohoji why wapo special! Kama hoja yako ni kwenye neno "wafilisi" basi ulitakiwa kufahamu matumizi ya lugha na mapana yake coz' utake usitake, kwenye nchi masikini wanaozifilisi nchi ni viongozi na watendaji wengine wa idara mbalimbali-- ziwe za umma au binafsi! There's no way mtu anayeishi Tandika, Mwananyamala, Temeke, Ubungo, Mwenge, Magomeni, Ilala and the like wakawa ni miongoni mwa wafilisi wa nchi hii-- no way na hata kama wapo basi idadi yao ni negligible.

Si kwamba wote wanaoishi maeneo hayo hapo juu ni maskini lakini ukikuta wana pesa basi majority ni pesa zinazotokana na kutumia jasho lao hata kama ni kwa kulala makaburini au kufanya illegal sio through signatures haiwezi kuwa zile ambazo zilitakiwa kujenga hospitali au madarasa!!!

Tukija eneo la Oyster Bay kwa mfano (for that case na Masaki and the like), sidhani kama unaweza kupata kiwanja cha 36*36 (robo ekari) kwa bei chini ya sh.500M... kwanza viwanja vyenyewe hakuna; labda uuziwe nyuma na bila kujali nyumba yenyewe ni mbaya namna gani, I doubt kama unaweza kuuziwa chini ya hiyo bei! Lakini wakati hali ndo hiyo, only few years ago, huko huko Oyster Bay waliuziana hizo nyumba kwa bei chini ya 100M (majority ni chini ya 50M) lakini baadae tena wakalazimika kujenga nyumba zingine kwa billions of T Shillings maeneo hayo hayo ili wakae wale wale ambao waliwauzia nyumba kwa bei chee!! Sasa kama sio kufilisi nchi utaita nini hiyo?

Nndugu yangu, inaweza ikawa kweli huyafahamu maeneo uliyotaja lakini usiniambie kwamba huifahamu Tanzania!
 
Back
Top Bottom