Upendeleo mwingine ukoo wa Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upendeleo mwingine ukoo wa Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen, width: 728"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][​IMG][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][​IMG][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen, width: 728"]
  [TR]
  [TD]Imeandikwa na Waandishi Wetu, Dar , Bagamoyo
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Jumanne, Oktoba 09, 2012 09:37

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Fukuto kubwa limeanza ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo, kutokana na baadhi ya wanachama kuhoji uhalali wa ukoo wa Kikwete kushika nafasi nyeti karibu zote katika Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo.

  Ukoo huo umehakikisha unashika nafasi zote za juu, ikiwamo ya Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo iliyokwenda kwa Shaibu Mtawa.
  Mtawa alipata kura 811 na kumshinda Mohamed Mrisho Kikwete aliyepata kura 613. Mtawa na Mohamed wote ni ndugu wa damu wa Rais Kikwete.

  Habari za uhakika kutoka miongoni mwa wanachama, zinasema majina ya wanandugu hao yalipendekezwa kutoka miongoni mwa wanachama 13. Wengi wao walikatwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na kuhitimishwa kwenye vikao vya kitaifa ambavyo Mwenyekiti wake ni Rais Kikwete.

  Katika ngazi hiyo ya Taifa, Mwenyekiti Kikwete alihakikisha majina matatu yanarejeshwa. Mawili - Shaibu na Mohamed - yakiwa ni ya ndugu zake, na mwingine Omar Mhando.
  “Mhando hapa aliwekwa kama msindikizaji kwa sababu kwenye raundi ya kwanza aliangushwa. Kwa kuwa hakuna mgombea aliyepata nusu ya kura, ikabidi upigaji kura urudiwe. Ikawa hivyo kwa kupigia majina mawili ya ndugu.

  “Kilichofanyika kwenye uenyekiti ni kuhakikisha majina mawili ya wanandugu hawa yanaingia ili mmoja achaguliwe. Hilo limewezekana kwa kuchaguliwa Shaibu,” amesema mmoja wa wanachama.

  Habari za uhakika zinasema kwamba kwenye uchaguzi huo kulikuwa na mvutano mkali kati ya wanandugu, hasa kutokana na ukweli kwamba Shaibu ni mdogo wa Katibu Msaidizi wa Rais Kikwete, Alhaji Kassim Mtawa.


  “Mvutano ulikuwa mkali kweli kweli bila kujali kuwa waliokuwa wakigombea ni wanandugu, ulikuwa mchuano wa miamba,” kimesema chanzo chetu cha habari.


  Baada ya uchaguzi huo, siku iliyofuata wanandugu walikutana katika kikao cha ukoo, kwa ajili ya kuzika tofauti zilizojitokeza miongoni mwao wakati wa uchaguzi.


  Mohamed Kikwete anakaririwa kusema kwamba hakuwa na kinyongo kutokana na kushindwa na Mtawa.
  “Aliyeshinda ni mdogo wangu, sina kinyongo,” alikaririwa akisema.Baadaye kilifanyika kikao cha Halmashauri Kuu kwa ajili ya kumchagua Katibu Uenezi na Katibu wa Uchumi.

  “Kabla ya uchaguzi, wapigakura kadhaa waliwekwa sawa, kuna kina mama walipata khanga, kina baba wakapata misuli na fedha za usafiri. Wajumbe walikuwa kama 140. Sikusikia aliyenung’unika kuwa amekosa kitu,” kimesema chanzo chetu.


  Katika nafasi ya Katibu Uenezi, mshindi alikuwa ni ndugu mwingine kutoka ukoo huo huo wa Kikwete, aliyetajwa kwa jina la John Francis (Boli Zozo).


  Kana kwamba hiyo haikutosha, nafasi ya Katibu Uchumi Wilaya ya Bagamoyo akachaguliwa Iddi Swala. Huyu ni mjukuu wa Rais Kikwete kwani amezaliwa na mtoto wa dadake Rais.


  Ushindi wa Swala umezua gumzo kubwa hasa kutokana na namna alivyokuwa kiongozi ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Bagamoyo. Mgombea aliyetajwa kwa jina moja la Mtiga, aliyeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa uongozi, alishindwa.


  Awali, ndugu mwingine wa Rais Kikwete aitwaye Yusuf Mrisho Kikwete, alishinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Kata ya Dunda, Bagamoyo.


  Kuchaguliwa kwa wanaukoo hao, pamoja na kupita bila kupingwa kwa Ridhiwani Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete, kunaifanya Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Bagamoyo iwe na viongozi wakuu wanne ambao ni ndugu wa damu, pamoja na wajumbe wengine wa kawaida.

  Nafasi hizo ni Mwenyekiti, Mjumbe wa NEC Taifa, Katibu wa Uchumi na Katibu Uenezi.


  Hata hivyo, kuwapo kwa wanandugu hao kungeweza kupanuka zaidi endapo nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Bagamoyo, ingeshikwa na mwanaukoo mwingine wa Kikwete, Magreth Halfan Kikwete. Magreth kaolewa na mtoto wa Mzee Seleman Kikwete.


  “Huyu wanachama wakasema haiwezekani, wakaamua kumbwaga maana ilishaonekana sasa chama kinakuwa cha ukoo tu. Tukaamua kumpa Hapsa Kilingo,” amesema mwanachama mwingine.


  Kadhalika, ndugu mwingine wa Rais Kikwete, Mwanaisha Halfani Kikwete, alipitishwa kugombea Ujumbe Baraza Kuu/Halmashauri Kuu ya UWT Mkoa wa Pwani.
  Wakati hali ikiwa hivyo kwenye uchaguzi huu unaoelekea ukingoni, mtoto mwingine wa Rais Kikwete, Khalfan Kikwete ni Mjumbe wa Baraza Kuu Idara ya Chipukizi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Mwenyekiti wa Idara hiyo ni Gabriel Makalla - mtoto wa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.

  Ushindi wa Ridhiwani, Mama Salma
  Kitendo cha Ridhiwani kupita bila kupingwa kumeacha maswali mengi. Kuna habari kutoka kwa baadhi ya wanachama kwamba wale waliothubutu kujitokeza kuwania nafasi hiyo walitishwa, na wao wakatishika.

  Wapo wanaosema kwamba kupita kwake kwa mbinu hiyo kulitokana na hofu ya wajumbe kutokana na ukaribu alionao na mzazi wake, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.
  Ni woga kama huo uliowaingia pia wanachama na wapenzi wa CCM katika Wilaya ya Lindi Mjini, walioamua kusalimu amri na kushuhudia mke wa Rais Kikwete, Mama Salma, akipita bila kupingwa.Ridhiwani na ubunge 2015Watu walio karibu na kijana huyo wanasema kwamba anajiandaa kugombea ubunge Jimbo la Bagamoyo mwaka 2015.

  Wanaotoa madai hayo wanatetea hoja yao kwa kigezo cha namna Kamati ya Wilaya ilivyosukwa kwa kuwa na viongozi wakuu ambao karibu wote ni ukoo mmoja. Wachunguzi wa mambo wanasema matumaini ya Mbunge wa sasa wa Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa, kuwania nafasi hiyo mwaka 2015 yamefutwa kutokana na kundi lake kushindwa vibaya katika ngazi karibu zote.


  Kwa sasa Dk. Kawambwa ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
  Jambo jingine ambalo JAMHURI haijalithibitisha ni kwamba suala la ukabila nalo limekuwa likitawala kwenye uchaguzi wilayani Bagamoyo, kama ilivyo kwenye uchaguzi wa CCM katika maeneo mbalimbali nchini.

  Dhambi hiyo ndiyo inayomfanya Dk. Kawambwa sasa aonekane kuwa ‘wa kuja” asiyetakiwa na “wazawa”.
  Mbona hata Nyerere alipendelea?Kuna hoja zinazojadiliwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, naye alipendelea ndugu zake wakati akiwa katika uongozi.Anatajwa Joseph Warioba Butiku, aliyekuwa Katibu Myeka wa kiongozi huyo, kama kielelezo cha Mwalimu kuwabeba ndugu.

  Pia anatajwa Joseph Nyerere, ambaye ni tumbo moja na Mwalimu, aliyepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa muda usiozidi miaka miwili; na pia Katibu wa Umoja wa Vijana wa TANU.


  Baadaye, kuanzia miaka ya 1970 hadi kifo chake miaka ya 1990, Joseph alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Butiama.


  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali David Musuguri, naye anatajwa kama mmoja wa waliopendelewa na Mwalimu, ingawa kumbukumbu zinaonesha kuwa Janerali huyo alijiunga katika Jeshi la Kikoloni la KAR kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939-1945).

  Source; Gazeti la Jamhuri
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini CCM isivunje KATIBA yake? Na kuhakikisha KIKWETE anacheo kama ni SENATE au Mkurugenzi wa RAIS wa NCHI? Sababu bila yeye kuwa na CHEO ataimaliza hii nchi kwa VIDOLE VYAKE MWENYEWE...

  Labda, Ndio Maana naogopa SIASA, Ukishaanza kupata VYA BURE na kuanza kukupigia MAKOFI hata Ukitabasamu... That's the end of your HUMANITY; YOU BECOME an ANIMAL WITHIN...
   
 3. j

  johnjohn Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wilaya ya Bagamoyo ina majimbo mawili ambayo ni Bagamoyo na Chalinze. Nahisi RIZ 1 2015 ananyemelea jimbo la Chalinze na si la Bagamoyo la Shukuru Kawambwa
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  nngu007 Hizi thread zenye maneno "HABARI ZA UHAKIKA, ZA KUTOKA CHANZO CHETU CHA HABARI N.K" mara nyingi ni za kizushi sana. Hebu weka source kama Gazeti, TV, au Redio. Hata hivyo Kuwa Rais hakuwezi kumzuia ndugu yako kugombea nafasi ya uongozi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Riz1 hawezi shinda jimbo lolote hata akija na contena la pesa
   
 6. real thinker

  real thinker Senior Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Je kama anagombea kwa njia za kifisadi? Acha kutetea magamba wewe.
   
 7. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hizi ndizo siasa za dunia (ingawaje ni mbaya na hzifai), hata nchi zilizoendelea tumeona wake wa marais, watoto wao wakiwa na nyadhifa nyeti, sometimes ni ngumu kutenganisha tamaa ya ubinadamu na masua;la nyeti! Ila Kikwete kazidi, kha!
   
 8. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Badala ya kujiandalia makao mazuri mbinguni, watu wapo"busy" kujiandaa kwenda motoni!
   
 9. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  trash trash
   
 10. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60

  Hapa una hukumu, angalia nawe usije hukumiwa.
   
 11. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Sina wadhifa wa kuhukumu mtu. Mimi nimenukuu baadhi ya vitabu vya dini vinavyosisitiza binadamu kujiandaa na pepo!
   
 12. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kama ukoo umeonyesha uwezo wakuongoza tatizo wapi?
   
 13. MchukiaUonevu

  MchukiaUonevu JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu thatha,
  Hizi ndio fikra za Watanzania wa leo,wamekalia siasa majitaka na majungu badala ya kujikita kwenye siasa za kujenga nchi yetu. You can see hata mleta hoja amekuwa selective kwenye article ambayo anajua source ya gezetia (probably Tanzania Daima..),lakini kwa makusudi ame-delete jina la gazeti! Jiulize,kwa nini kafanya hivi.


  Kama mtoto au ndugu wa kiongozi kugombea nafasi ya siasa imekuwa issue,mbona hatuhoji kusikia Daktari fulani na watoto wake wote ni madaktari,Mwanasheria fulani na watoto wake wote wanasheria..hii inaonyesha akili ya kila Mtanzania na haswa vijana wengi wenye fikra mgando wanavyoabudu siasa. They dont see opportunities or any other worthy job nje ya siasa. Isitoshe,ukitazama kwenye upinzani,kuna uozo uliopitiliza kwenye nafasi za uongozi. Ukiwauliza hii field ya kugombea nafasi za uongozi,for instance Chadema,ni uozo!
   
 14. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Nashukuru kwa kulielewa hilo
   
 15. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi kweli mwandishi wa uzi huu ana akili? Yaani tuiache Tanzania iingie kwenye usultani kama Oman? Uliona lini Bush akiwa rais mkewe alikuwa kigogo ndani ya Repulican, au Clinton? Hata Moi au Mugabe pamoja na ubabe wao, hawakupata kufanya hivyo.
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Source na mwandishi wetu hahaha

  Lawama ziwaendee wana Bagamoyo sio JK mwenyewe.

  Mimi kama rais na mdogo wangu anataka kuwa mwanasiasa what has it got to do with me?
   
 17. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Ndiyo maana niliandika hivyo!
   
 18. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  HATARI: Angalieni watoto wa vigogo wa serikali ya Tanzania waliopita kwenye ngazi ya uchaguzi Taifa UVCCM
  Dickon Membe. Fready Lowasa, Ridhwan Kikwete, Ashura Hussein Mwinyi, Beny Samuel Sitta, Deborah Mwandosya, Irene Pinda, Felister Ndugai, Christopher Ndejembi, Sharifa Bilal, Hawa Kigoda, Judith Mukama na Jarome Msekwa
  Hu ndio utithi wa uongozi walipowa lakini la kushangaza sijamuona mtoto wa Rais Mstafu Dr Salmin Amour jee nawauliza yeye hana mtoto mwenye umri wa kupewa urithi wa uongozi?
  Lapili ambalo nimeliona ni kuwa viongozi wa Zanzibar ni wachoyo maana sio wengi waliowarithisha uongozi watoto wao
  Sasa watoto wa kimaskini wasahau kupata nafasi za uongozi kwa mfumo huu
  NIACHENI NIPUMUWE
   
 19. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Zanzibar na kabla ya Mapinduzi/mauwaji ya 1964. 1. Yalifanywa Mapinduzi kwasababu yakuondosha utawala wa *SULTAN* ambao baadhi yetu walikuwa wakinugunika kuwa wakifanya ‘UBAGUZI' na KURITHISHANA UTAWALA ndugu baada ya ndugu na watoto baada ya watoto, yaani utawala ulikuwa unakenda katika ukoo ((femiliya yao tuu)) Sasa haya tunayoyaona yanajiri siku hizi hapa Zanzibar na kule Tanganyika!! Jee si-mfano ule ule uliokuwa ukiendeshwa na utawala wa "KISULTAN/UFALME?? Au tuseme mkuki kwa nguruwe, kwa bin Adam ni mchungu??
  Kuna msemo unasema: USILAUMU YA WATU UKAJIFANYA NA KENGEZA!! VITIMBI VYAKO NI ASHADDI KUSHINDA MNGEREZA!!!!
   
 20. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata sura yako inafanana na Sheikh Farid, wale wale! Back to the point, umesoma hiyo article vizuri kweli, au Magamba yameziba hadi macho na kukufanya usione vizuri? Rudia tena kusoma, source ya habari hiyo imeandikwa aya ya tano kutoka mwisho! Pia nakushangaa kulinganisha namna daktari na mwanasheria wanavyopatikana na jinsi viongozi wa Magamba wanavyopatikana! Yaani hata hujui tofauti ya taaluma (profession) na siasa (kwa Tanzania ni SI HASA, yaani politicking). Yaani watu wanavyokamua MUCHAS kwa miaka zaidi ya mitano huku waki-sup na ku-pass kwa grade C tu wewe unakuja kulinganisha na jinsi ndugu wa M.k.w.e.r.e wanavyojiokotea uongozi kwenye Chama kinachokufa miaka mitatu ijayo? You are such an idiot! Too low to any matured and self-humbled person!
   
Loading...