mnyikungu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2009
- 1,960
- 2,464
kweli tuwape fursa na sio upendeleoMajaribio ni kitu kizuri lakini kuna vitu havihitaji majaribio kama uongozi wa nchi. Tukiamuwa kuwapa uongozi kundi fulani eti kubadili mindset nahofu tutakuwa nyuma siku zote. Uwezo wa mwanamke au mtu mwengine yeyote hauji kwa kupewa upendeleo kwani upendeleo ni kuonyesha kasoro ya anaependelewa. Wanawake wetu wa Tanzania hawahitaji kupendelewa bali ni kupewa fursa sawa na wenzao wanaume. Tumeshuhudia huko nyuma wanawake ambao walionyesha uwezo wao si kwa upendeleo. Tulikuwa na wanawake kama Bi tit, Julie Manning na wengineo na kwa wa karibuni ni wanawake kama Mongella.
Okay na tutowe upendeleo kama sera yetu, sasa kwanini katila Baraza la Mawaziri wako wachache? Ni kiini macho kujidai kuwa tuwe sawa huku tukidharau hilo kwenye nafasi zilizo nyeti kama uwaziri, na vyombo vikuu vya utawala.