upendeleo kwa wanawake ni njia sahihi ya kuleta usawa na wanaume? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

upendeleo kwa wanawake ni njia sahihi ya kuleta usawa na wanaume?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchakamchaka, Mar 10, 2010.

 1. m

  mchakamchaka Member

  #1
  Mar 10, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  leo hii ni kawaida kusikia wanawake wakipewa upendeleo maalumu katika vyeo vya kisiasa eti kwa minajili ya kuwa na usawa wa kijinsia katika uwakilishi,cha kujiuliza je hii ni njia sahihi ya kuwa na usawa wa kijinsia ktk uwakilishi?binafsi siamini kabisa katika mawazo haya, huwezi kumpa nguvu mtu ambaye kifikra tu tayari anajiona mwenyewe hana nguvu, kwa kufanya hivi mi naamini tunazidi kuwadhoofisha kwani hawatakaa hata siku moja waamini wanaweza kusimama wenyewe mbele ya wanaume.jana india wamepitisha mswada wa kuwapa wanawake uwakilishi wa theluthi nzima katika bunge lao la congress...mnaonaje hili wanaforum wenzangu?
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hata mie nakubaliana na wewe......huwezi kumpa mwanamke cheo kwa minajili ya kuwa sawa na mwanamme japo kama hana sifa za kuwa na cheo hicho.

  nafikiri wangeweka milango wazi ya wanawake wenye uwezo kugombea sawa na wanaume pangepatikana usawa naturally, lakini usawa huu wa kulazimishia huu hamna kitu
   
 3. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  usawa wa namna hiyo si njia sahihi daima,lakini hayo yote ni amri kutoka kwa mashetani wanaoitwa wahisani,wao hawayatekelezi haya ila wanalazimisha nchi changa zitekeleze ujinga hou.
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Mbona hata wao wameshindwa kubadilisha wimbo wa Taifa wa Canada? Wanatuburuza tu na sisi tunachekelea. Pemye demokrasia kiongozi anapatikana kwa uchaguzi wa wengi na sio kupendeleana.
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Tunapojadili juu ya wanawake ni vema tukajua tunajadili juu ya mama zetu, dada zetu, shangazi zetu, mabinti zetu nk na si watu baki. Je tungependa kuendelea kuona watu hao niliowataja wakipata haki sawa na wanaume?
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Well kwa mantiki ya kuweka mbele uhusiano basi sisi ni haki yetu kujipendelea. Hata hivyo kwa kuangalia mjadala ni kuwa haki sawa maanaayake ni kusimama sawa pahala popote sio kupendelewa. Hilo la kupendelewa ndio linalodaiwa kufanyika katika mfumo unaoitwa dume. Sasa tukisema kuwa tunawapendelea jamii fulani kwa makusudi ndio tunatatuwa tatizo? Na in application,huu utaratibu wa viti vya upendeleo jee umesaidia kiasi gani kuwafanya wanawake wajinasuwe na kuchaguliwa wengi badala ya kukimbilia upendeleo?
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ngekewa,

  Unajua tatizo tulilonalo kwenye mfumo dume ni mindset. Tukiweza kubadilisha mindset za watu (wanawake na wanaume), kwa hakika tutapiga hatua katika suala hili. Kinachoendelea sasa ni kujaribu kubadili mitizamo ya watu juu ya mwanamke.

  Kwa kuwapendelea (systematically), kunabadili mindset za watu - kwa mfano waliokuwa wanadhani/amini mwanamke hawezi kuwa mbunge, waziri au spika nk pengine kwa sasa wanaweza kuwa na mtizamo tofauti. Kwa maoni yangu, utaratibu huu unafanikiwa na watu wameanza kubadilika.

  Kumbuka huu mfumo dume umekuwepo kwa muda mrefu na huwezi kubadili ndani ya usiku moja. Upendeleo kwa wanawake kama intervention tool naamini is justifiable.
   
 8. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mi naona huo upendeleo haujawasaidia kitu zaidi unawafanya wazidi kuonekana ni viumbe duni yaani wao ni watu wa kubebwa siku zote na ndio maana inayowapigia kampeni ya huo usawa mingi ni midume
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  I real hate that word...
  kwa nini unipendeleee?? sina uwezo bali naonewa tu huruma
  ili statistics ziende sawa....that uwakilishi wa wanawake umekuwa 30%
  wat is it for real???
   
 10. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  huu ni ujinga na upungufu wa akili, hii awamu ya nne kweli ni ya wanwake( au ya kike) kama alivotabiri sheikh yahya, tunajaza madudu tu katika system itakuja kutucost kama vile kuungoa ukoloni, jamani hata vitabu vitakatifu havikulivalia njuga hili jambo, why twampa Mwenyezi Mungu masahihisho? Mwanamke kazi zake zipo wazi, kutokana na nyakati basi kama anaweza apambane, so muhimu ni kujitahidi kuchange mindset za watu na si kumzuia mwanaume mwenye uwezo asipande ili mwanamke apande, at the end of the day mwnamke hata kama ana uwezo zaidi ya mwanamme wake, mme ndo provider siku zote, its nature! lazma ukojoe, ule, uwe na love feeling, upige chafya hizi ni nature tulivoumbwa!si issues za siasa na kutafuta ujiko kwa mademu, viongozi wetu pambaf kabisa!!
   
 11. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Kweli hii ni awamu ya wanawake, lakini tunachokifanya kweli kitatughalimu, hawa wanamama wanamajukumu yao sasa tunapowapa majukumu yasiyo yao, yao nana atatekeleza? huko ulaya wenzetu wanajuta, wamewapa majukumu wanawake matokeo yake wanawake wa huko hawataki tena majukumu yao.Hawataki tena kuzaa, wanaona kuzaa kunawapotezea mda na kuwahatarishia ajira na masrahi yao.je na sisi tunataka kufika huko?
   
 12. K

  Kekuye Senior Member

  #12
  Mar 12, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Mkuu inaelekea athari za mfumo dume zimekufanya uwe na uwoga kuwa wanawake watakapokuwa na nafasi sawa na wanaume mambo yatakuwa hayaendi.
  2. Itakuwa vyema utofautishe mwanamke na mwanaume kibaiolojia/kiasili na jinsi jamii (hasa mfume dume) ilivyotengeneza majukumu ya mwanamke na mwanamume. Mfano, nani kwakwambia kuwa mwanamke atakapotimiza wajibu wake wa kuzaa hataweza kuwa kiongozi?
  3. Kinachofanyika (mfano viti maalum, upendeleo kwa wanawake kujiunga elimu ya juu) ni suluhisho la muda mfupi ili kuiwezesha jamii (wanawake na wanaume) kubadili mitizamo yao ambayo itapelekea mabadiliko na kutoa nafasi sawa ya ushindani kwa wote wawili.
   
 13. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ndugu wapi umeona huo ushindani? na kwanini tushindane?hapo ndipo sipataki,tutapoanza kushindana mambo hayataenda.
   
 14. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ugomvi wangu mimi ni hizi Yes Boss! za wa magharibi wanaojiita wahsani! Eti kwa sababu wahsani wanataka 30% Basi bila kujali anaweza hawezi lengo lazima lifikiwe! Kuna wanawake kweli wanaweza Mfano mke wangu (What.......? Lazima usifie chako Bwana) Sio dhambi kuwapa madaraka hata kama ingekuwa ni 100% ilimradi tu watanzania tumeamua kuwapa, Lakini pia hata tusipowapa tusiletewe pressure na hawa wahsani. Siku zote mwanamke atakuwa chini ya mwanaume (simaanishi mtumwa) namaanisha mshirika wa karibu! Historia inaonyesha kuwa Hakuna mwanamke aliyewahi kufanya a large scale Ufida kama uliofanywa na akina Richard wa Monduli. Makofi tafadhali kwa wanawake!!!!!!!
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Mar 12, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani tatizo kubwa la swala hili ni hii tafsiri ya neno HAKI SAWA kwani imekuwa kaa vile kuna ushindani hapa. Na laukama tutatafsiri HAKI SAWA kwa mantiki ya kulingana ktk Idadi ya uwakilishi nadhani hilo swala tungelianza na kumuuliza Mungu ambaye ndiye muumba wetu aliyeshindwa kuweka usawa katika kizazi, usawa wa maumbile, usawa hadi ktk kazi zetu kiasi kwamba wanawake wanazaa wanaume wasizae, wanyonyeshe na sii wanaume na kadhalika...Yaani kazi zote ngumu kapewa mwanamke hali mwanamme anapeta pasipo hata kupata hedhi..Je, kuna haki sawa?... Hii ndio hofu yangu kubwa ya kule tunako elekea sisi ktk swala hili.

  Haki ya mwanamke, bora itambulike kutokana na kudidimizwa kwa mwanamke ktk mambo ambayo anatakiwa kupewa nafasi sawa na mwanamme, yaani ikiwa ni kuandikishwa shule mwanamke asikataliwe kuandikishwa kusoma kwa sababu tu ni mwanamke.. Mwanamke akigombea Ubunge asinyimwe nafasi hiyo kwa sababu tu ni mwanamke, hii ndio kinachozungumzwa kwani wanawake wamekuwa wakibaguliwa kwa muda mrefu kushiriki kikamilifu ktk ujenzi wa jamii na nchi zetu...lakini swala la KUWAPENDELEA wanawake haliwezi kuwa solution ya kusimamisha HAKI hii, bali ni kuweka uuwiano baina ya jinsia mbili ili kutimiza malengo fulani....sasa watueleze hayo malengo tutaelewa vizuri kuliko utumia hii lugha ya kutafuta haki.

  Hivyo isomeke kwamba kasi ya kuwapendelea wanawake iwe bungeni ama katika Utawala haitokani na kunyimwa kwa haki hiyo wanawake ila ni ktk kuweka uuwiano baina ya jinsia hizi mbili. Na kama tukianza na hivyo kesho itakuwa swala la makabila, kesho kutwa dini zitaingia na haya maswala ya Uuwiano kuwa ndiyo haki inayogombea..

  Wakuu zangu, wake kwa waume tuwe makini sana na maombi kama haya kwani tutakuja potea kabisa maana ya HAKI SAWA badala yake kuwa UUWIANO SAWA..Kinachotakiwa hapa ni wanawake kupewa haki sawa na wanaume tunapotoa nafasi za kazi ama uongozi na yule tu mwenye uwezo wa kuongoza ndiye atakayepewa kushika madaraka pasipo kutumia kigezo cha jinsia kuwa sababu..Hilo tutaliona hata tunaposema Binadamu wote ni sawa, usawa huu hauhusu maumbile yetu kutokuwa sawa hivyo tujaribu kuyarekebisha ili msemo huo ulete maana kamili wa usawa wa binadamu..

  Hivyo tuweni makini sana kwa matumizi ya lugha hizi kwani tunaweza poteza kabisa maana..Ni haki ya wanawake kushiriki ktk ujenzi wa nchi yetu wasibaguliwe kwa sababu tu wao ni wanawake, hali wana uwezo sawa au zaidi ya mwanamme aliyeitaka nafasi hiyo pia. Kama wanataka Ubunge watajiandikisha, watagombea na watashinda walioshinda.. isije hata siku moja tukawapa wanawake nafasi za uwakilishi bungeni kwa sababu ni wanawake ili kuweka uuwiano na kutumia dhamira hii kama ndio HAKI ya mwanamke....Na siwlewi kaa ni jambo zuri kwani miye hapa nina watoto wa kike watatu na mvulana mmoja, sijui nami nifanye nini kuleta haki ama uuwiano nyumbani kwangu..
   
 16. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  ....Na siwlewi kaa ni jambo zuri kwani miye hapa nina watoto wa kike watatu na mvulana mmoja, sijui nami nifanye nini kuleta haki ama uuwiano nyumbani kwangu..[/QUOTE]

  "Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee." Mithali 22:6
  Take heed! Dont turn your children into radical ferminist
   
 17. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Uwiano baina ya jinsia hii ulitakiwa uwe katika mtindo wa fair competition na sio kutunukiwa tu kisa kujaribu kuweka usawa. Wanawake wanatakiwa wastruggle wawe na vigezo sawa na wanaume katika sekta yoyote ile na kuwe na fair ground ya kupick watu katika ngazi na kazi mbalimbali
   
 18. F

  FM JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Akina mama wamevipiga vita na sasa kuna dalili za ushindi. Kwa muda mrefu wamefanya hila za kuwaaminisha akina baba kuwa wanawake wanateseka, wanaonewa, wanapuuzwa, wakoseshwa fursa na mambo kadha wa kadha. Mara nyingi utasikia katika kila janga waathirika wakubwa ni akina mama na watoto wadogo. Bahati mbaya sana katika majanga mengi wanaoplay role kubwa ya kupambana ni akina baba (wanaume) na katika mazingira hayo tu, ni wazi kuwa wao ndo wanakuwa katika mazingira hatarishi zaidi. Ukidhani kuwa hawawezi unajidanganya mzee, pamoja na mambo mengine, kuwaaminisha tu kuwa wanahitaji kupewa nafasi za upendeleo ni uwezo! My thinking!!!
   
 19. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #19
  Mar 12, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mimi naona inaweza ikawa njia sahihi kama tu hao wanawake wanaopewa "upendeleo" wako fit kwa nafasi walizopewa. kuna wanawake wengi wazuri (kichwani) ambao wangemudu nafasi nyingi sana lakini wanakosa sometimes sababu hawana connections. lakini ukweli ni kwamba huo upendeleo wanapewa wanawake ambao hawawezi hizo nafasi ndo maana inakuwa kama kero kwa watu wengi.
  Mfano zile nafasi za Ubunge za kupendelewa, mimi naona kama wangepewa wanawake ambao wanaweza kweli kwenda kutunga sheria ingesaidia sana maana contribution ya mwanamke pia ni muhimu sana kwenye utungaji wa sheria zetu
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Majaribio ni kitu kizuri lakini kuna vitu havihitaji majaribio kama uongozi wa nchi. Tukiamuwa kuwapa uongozi kundi fulani eti kubadili mindset nahofu tutakuwa nyuma siku zote. Uwezo wa mwanamke au mtu mwengine yeyote hauji kwa kupewa upendeleo kwani upendeleo ni kuonyesha kasoro ya anaependelewa. Wanawake wetu wa Tanzania hawahitaji kupendelewa bali ni kupewa fursa sawa na wenzao wanaume. Tumeshuhudia huko nyuma wanawake ambao walionyesha uwezo wao si kwa upendeleo. Tulikuwa na wanawake kama Bi tit, Julie Manning na wengineo na kwa wa karibuni ni wanawake kama Mongella.
  Okay na tutowe upendeleo kama sera yetu, sasa kwanini katila Baraza la Mawaziri wako wachache? Ni kiini macho kujidai kuwa tuwe sawa huku tukidharau hilo kwenye nafasi zilizo nyeti kama uwaziri, na vyombo vikuu vya utawala.
   
Loading...