real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,287
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jana iliambiwa kesi ya Aliyekuwa Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu ya kutakatisha dola za Kimarekani 300,000 umekamilika
Hata hivyo, Aveva alishindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake hiyo kwa kuwa bado amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Madai hayo yalitolewa na upande wa Jamhuri jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Alidai kuwa mshtakiwa wa kwanza bado mgonjwa akiendelea na matibabu Muhimbili.
Hakimu alisema kesi hiyo itasikilizwa maelezo ya awali Aprili 5, mwaka huu.
Katika kesi ya msingi, vigogo hao wa Simba wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 674.8 kwa kiwango cha ubadilishaji fedha cha jana).
Katika shtaka la kwanza ilidaiwa mahakamani hapo walipopanda kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29, mwaka jana kuwa Machi 15, 2016 washtakiwa wote kwa pamoja walighushi fomu ya kuhamisha fedha ya tarehe hiyo wakionyesha kwamba klabu ya Simba inalipa deni la dola za Marekani 300,000 kwa rais wake Aveva.
HAMISHA FEDHAKatika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Machi 15, 2016 katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe lililopo Ilala, jijini Dar es Salaam, Aveva aliwasilisha fomu ya kuhamisha fedha zilizoghushiwa ya terehe hiyo akinyesha kwamba Klabu ya Simba imemlipa dola za Marekani 300,000 huku akijua sio kweli.
Msigwa alidai katika shtaka la tatu, kati ya Machi 15 na Julai 29, 2016, washtakiwa wote wawili walikula njama ya kutakatisha fedha hizo huku wakijua zimetokana na nyaraka za kughushi.
Upande wa Jamhuri ulidai katika shtaka la nne, Machi 15, 2016 katika benki ya Barclays Tanzania Limited, tawi la Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni Aveva alihamisha dola za Marekani 300,000.
Shtaka la tano, ilidaiwa kuwa Machi 15, mwaka 2016 katika benki ya Baclays tawi la Mikocheni, Kaburu alimsaidia Aveva kupata dola za Marekani 300,000 wakati akijua zimetokana na zao la uhalifu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka yao lakini kwa kuwa mashtaka ya kutakatisha fedha hayana dhamana kwa mujibu wa sheria, walinyimwa.
Chanzo: Nipashe