Upelelezi kesi ya Wema Sepetu wakamilika, kuanza kusomewa mashtaka

Fang

Content Manager
Nov 5, 2008
509
322
Mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu anatarajiwa kuanza kusomewa maelezo ya awali kufuatia kukamilika kwa ushahidi upande wa Jamhuri juu ya kesi ya kusambaza picha za ngono inayomkabili.

Wema Sepetu anatuhumiwa kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wake wa kijamiii ambapo kupitia hatua hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 21, 2019 kumsomea maelezo ya awali.

Akiwa mahakamani hapo Mwanasheria wa Serikali, Glori Mwenda amesema, "shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na taarifa njema ni kwamba upelelezi wa shauri hili umekamilika, hivyo tunaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali, mshtakiwa huyu"

Wema anatetewa na wakili, Ruben Simwanza, alifikishwa na katika kesi ya msingi anashtakiwa Oktoba 15, 2018 jijini Dar es Salaam alichapisha video ya ngono.
 
Nilijua ya kukutwa na PULI aka MSOKOTO aka MNERI aka MJANI aka KIJITI aka Msumali aka SHADA aka ganja aka bangi kumbe ya kusambaza picha? Hii kesi DIPIPI hana nia ya kuendelea nayo.
 
Hii video inayosemwa sio ile inayomwonesha akilana denda na mpenzi wake? Hiyo ndio ngono? Embu wajuzi watufafanulie,
 
Back
Top Bottom