Upelelezi kesi ya dada wa Balali upo hatua za mwisho

mkara mshamba

Senior Member
Jan 15, 2020
106
250
Nimesoma habari hizi kwenye chanzo hiki. Banki Kuu, marehemu Daudi Balali, Elizabeth Balali (54) anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, anaendelea kusota rumande huku ikielezwa upelelezi uko katika hatua za mwisho.

Kesi hiyo ilikuja jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutajwa. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo, alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kwamba kesi ilikuja kwa kutajwa na upelelezi unaendelea katika hatua za mwisho.

Alidai Hakimu Mfawidhi, Godfrey Isaya anayesikiliza kesi hiyo ana udhuru, hivyo aliomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu Mwaikambo aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 26, kwa kutajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017, Dar es Salaam, alijipatia Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Roderick Kisenge kwa ulaghai. Inadaiwa alijipatia fedha hizo baada ya kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambazo halijapimwa lililopo Boko Dovya, Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa katika kipindi hicho mshitakiwa huyo alipokea kiasi hicho cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

KWA UELEWA WANGU MDOGO SIJAONA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI WALA UTAKATISHAJI PESA. LAKINI WAHENGA WALISEMA ELIMU NI BAHARI KARIBUNI MNIPE DARASA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,402
2,000
Nimesoma habari hizi kwente chanzo hiki. Banki Kuu, marehemu Daudi Balali, Elizabeth Balali (54) anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, anaendelea kusota rumande huku ikielezwa upelelezi uko katika hatua za mwisho.

Kesi hiyo ilikuja jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutajwa. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo, alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kwamba kesi ilikuja kwa kutajwa na upelelezi unaendelea katika hatua za mwisho.

Alidai Hakimu Mfawidhi, Godfrey Isaya anayesikiliza kesi hiyo ana udhuru, hivyo aliomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu Mwaikambo aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 26, kwa kutajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017, Dar es Salaam, alijipatia Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Roderick Kisenge kwa ulaghai. Inadaiwa alijipatia fedha hizo baada ya kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambazo halijapimwa lililopo Boko Dovya, Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa katika kipindi hicho mshitakiwa huyo alipokea kiasi hicho cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

KWA UELEWA WANGU MDOGO SIJAONA KOLA LA UHUJUMU UCHUMI WALA UTAKATISHAJI PESA. LAKINI WAHENGA WALISEMA ELIMU NI BAHARI KARIBUNI MNIPE DARASA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nikishaona tu Habari fulani chanzo chake ni Udaku Special huwa naziamini kwa 1% tu lakini 99% zilizobakia nakuwa siziamini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom