Upelekwe Muswada Bungeni wa Kuunda Upya Jeshi la Polisi

Naunga mkono hoja...

Nakumbuka kuna kipindi ZITO akiwa mbunge alishaanzishaga hii hoja...ikiwa pamoja na kubadili mtaala pale CCP uendane na mahitaji maana wengi bado wanaonekane wakizamani..
 
Hilo jeshi la polisi ndio linalowaweka viongozi wa CCM madarakani, na kwakuwa CCM ndio wako bungeni, hakuna uwezekano wowote hilo bunge lifanye mabadiliko ya hilo jeshi, kwani wao ni wafaidika wa moja kwa moja kwa huo uhalifu wa polisi.

Kwa katiba hii na namna viongozi wetu wanavyopatikana sasa, hakuna uwezekano wowote wa maboresho wa jeshi la polisi, kwani utawala uliopo na hiki chama tawala ni wafaidika wa dhahiri wa jeshi hili ovu. Kuna uhusiano wa wazi kabisa wa kihalifu baina ya polisi, na chama tawala kilichopoteza uhalali kwa umma.


Pamoja na hayo yote bado tunapaswa kupiga kelele kuliko kususbiri CCM itoke na Katiba ipatikane ilihali watu wanakufa daily..
 
Japo tuna bunge ambalo nalo kila mmoja anajua namna lilivyopatikana, je, haliwezi likatenda jambo jema kwa wananchi?

Jeshi la Polisi, kwa nyakati tofauti tofauti limethibitika kuwa halifai kabisa kusimamia sheria kwa sababu limetumika kama genge la uovu.

1) wafanyabiashara wa madini, bila hatia, polisi waliwapora fedha yao, kisha wakawaua, na baadaye kusingizia kuwa walikuwa majambazi. Waliyafanya hayo wakitumia gari la polisi, bunduki za polisi, na baadhi wakiwa wamevaa sare za polisi. Vifaa walivyopewa kuvitumia kuwalinda wananchi, wakavitumia kufanya ujambazi.

2) Polisi walimwua mwandishi wa habari Mwangosi, kisha kwenye taarifa ya mwanzo wakawasingizia watu waliokuwepo kuwa walimwua mwanahabari huyo kwa kitu chenye ncha kali. Picha za video zililiumbua jeshi la polisi.

3) Binti mwanachuo Akwilina aliuawa na Polisi, kesi wakabambikiwa viongozi wa CHADEMA. Mpaka leo, hakuna polisi aliyeshtakiwa kwa unyama ule.

4) Kuna kijana aliwahi kuaawa na polisi Morogoro siku CHADEMA wanafanya mkutano, polisi wakadai alikuwa anaandamana na alikuwa anawarushie mawe polisi. Mashuhuda waliwaumbua, kijana wala hakuwa mshiriki wa maandamano wala mkutano wa CHADEMA, alikuwa mfanyabiashara mdogo na alipigwa risasi akiwa kwenye biashara yake.

5) Leo mmeyasikia ya huko kusini, polisi maafisa, wengine wa ngazi ya mkoa ndio walimpora kijana pesa yake zaidi ya milioni 30, kisha wakamwua mwenye pesa, na kuitupa maiti yake. Kama viongozi wa polisi wanafanya haya, je, hao wa chini huko, si balaa?

Jeshi la polisi linajitambulisha kama alama ya uovu:
1) Kufuatana na tafiti mbalimbali za huko nyuma, polisi na mahakama ndio wanaoongoza kwa rushwa

2) Polisi wa Tanzania wanaua mahabusu, hata Rais Samia⅞ alilisemea na kukemea.

3) Polisi hubambikia watu kesi, hata Rais alilisemea

4) Polisi wanashiriki matukio ya ujambazi, kama ilivyoshuhudiwa hapo juu

Kwa ujumla, kwa sasa, kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha polisi na majambazi. Majambazi yanapora na kuua wenye pesa, polisi nao wanafanya hivyo.

Huku uraiani watu wanapeana tahadhari, ukiwa na pesa nyingi, ujihadhari na polisi kuliko unavyotakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya jambazi.

Hivi kweli:

1) Watanzania tunastahili kuwa na jeshi la nna hii?

2) Hawa watawala wetu wameridhika,ç Watanzania kuwa na Jeshi la Polisi ambalo ni hatari kiasi hiki?

3) Tutaendelea kuwa na jeshi la polisi la namna hii mpaka lini?
Nilikuwa nawaza kuandika kitu kama hiki mkuu,Ila nikaogopa jamaa wasije wakanishughulikia.Uliyoandika hapa ni kweli tupu na wao wenyewe wanakiri kwamba rushwa Polisi ni nje nje,wakisema Dar ndipo palipo kithiri.Wanakiri pia kwamba Polisi wanaua raia,na wanasema mara nyingi ukisikia Polisi wamerushiana risasi na majambazi na kuwaua,ujue hiyo ni ishu.Leo tu nimepata taarifa ya mwananchi aliyeporwa 70million na Polisi na hatimaye ili kuficha ushahidi wamemuua.

No,Ni kweli hali ya Jeshi letu la Polisi ni mbaya,kwa hiyo ni kweli kuna haja ya kulisuka upya Jeshi hili.Hili si Jeshi tena la kulinda Wananchi na mali zao,bali ni Jeshi la kupora wananchi mali zao.
 
Pia Usalama wa Taifa uko kulinda maslahi ya CCM na si raia. Wanao kamatwa na kushughulikiwa na Usalama wetu si wale wenye kuhatarisha usalama wa nchi bali ni wapinzani wenye hoja zilizoshindwa kujibiwa.
Hao ndio hamna kitu kabisa !
 
Kitu cha muhimu sana umeongea Jeshi limekosa weredi yaani polisi wenye dhamana ya kutunza mali zetu wao ndio wanaua Raia ili wapate pesa na kuuana wenyewe ili kupoteza ushahidi..RPC na RCO wake wa Mtwara wamesimamishwa kupisha uchunguzi kama walikua hawajui kitu na wapo ofisini walikua wanafanya nini?
 
Unaliundaje jeshi jipya? Hili la zamani unalifahamu vizuri?Kwani tatizo ni jeshi au members wa jeshi zima? Umefanya utafiti kujua tatizo zimeanzia wapi?

Mara nyingi tatizo siyo CCM tatizo ni watu waccm hata Polisi tatizo siyo Jeshi tatizo ni Askari mmoja mmoja ili kubadili fikra za hawa wenye maadili yaliyopinda inatakiwa utafiti uliotukuka ufanyike.

Hata kama hatutapata katiba mpya hii iliyopo iwekwe marekebisho ya kutosha kuhusu Jeshi la Polisi ambayo yatakuwa muongozo wa kuendesha jeshi kipengere cha kutojihusisha na siasa kiendane na uhalisia waondokane na uteuzi nafasi zijazwe kutokana na weledi wa KAZI na siyo uteuzi Kwa maslahi ya mteuaji.
 
Back
Top Bottom