Polisi waenda kupekua nyumbani kwa Mbunge Tundu Lissu

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Polisi wameenda kupekua nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu , wakiongozana na mwanasheria huyo.

Tundu Lissu alikamatwa na Polisi akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na anakabiliwa na tuhuma za Uchochezi na Kumkashifu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


UPDATE 1
Jeshi la Polisi limemaliza upekuzi waliokuwa wanafanya nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu wanaelekea Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Taarifa ya msemaji wa Chadema Tumaini Makene amesema Lissu anapelekwa polisi kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria kuendelea ikiwa ni pamoja na dhamana yake ambayo kisheria iko wazi.

Amesema upekuzi uliofanyika ulihusu makosa mawili anayotuhumiwa nayo ya kumkashifu rais na Uchochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 huko nchini Canada.
 
Polisi wameenda kupekua nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu , wakiongozana na mwanasheria huyo.

Tundu Lissu ambaye anawadhulumu wapiga kura wake kwa kutumia mda mwingi akiwa Vizimbani anakabiliwa na Kosa la Uchochezi na Kumkashifu Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Labda wanaenda kutafuta mkojo wa nyumbani
 
Kama wanashtaki kuwa kamkashifu raisi na nyumbani wapi na wapi, wakifika afungue friji awape juice wanywe manake washakuona kama kawaida, ila ananiacha hoi, utakuta yeye na tabasamu lake utadhani sio mtu wa kulipua makombora, kilichotakiwa hao polisi au serikali wangemjibu kwa hoja tu lakini kimabavu namna hiyo, muafaka hautakuwepo
 
Back
Top Bottom