UPDP kujadili katiba mpya mwezi ujao

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
UPDP kujadili katiba mpya mwezi ujao


Na Rabia Bakari

CHAMA Cha siasa cha UPDP kinatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka mapema mwezi Februari kwa ajili ya kufanya tathmini ya uchaguzi na kujadili ajenda mbalimbali kwa maendeleo ya chama hicho.Akizungumza na
waandishi wa habari, Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Fahmi Dovutwa, alisema moja ya ajenda zitakazojadiliwa na chama hicho ni pamoja na kukipa uhai chama kwa mikakati mbalimbali ikiwemo kuzunguka mikoani, sanjari na kujadili mabadiliko ya katiba wakiwa kama wadau.

Alisema baada ya mapendekezo ya wajumbe wa mkutano, chama kitaandaa ziara za mikoani, zitakazohusisha jimbo kwa jimbo, matawi na mashina kwa ajili ya kuweka mizizi ya uongozi kuanzia ngazi za chini.

Alisema baada ya mkutano huo, UPDP, ikiwa ni wadau wa katiba, itatoa rasimu ya mapendekezo ya katiba, na kushauri vitu muhimu kwa ajili ya maslahi ya wananchi.

"Rasimu hiyo itakuwa na maslahi na umma zaidi, tofauti na mapendekezo yanayotolewa sasa na wanasiasa ambayo yamelenga kuingia ikulu pekee.

"Kwanza kabisa lazima katiba iseme kuwa Tanzania iwe taifa la kujitegemea,lakini hakuna anayeweka kipaumbele katika suala hilo.

"Sehemu ya utangulizi katika katiba, kwenye misingi ya katiba inasema 'kwa kuwa sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga jamii yetu, jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki na udugu na amani.' Lakini sehemu hii haijataja tafita huru,"aliongeza.

Alisema kuwa ni lazima suala la kujitegemea litajwe katika katiba, lakini badala yake wanasiasa wanatoa mapendekezo kwa uchu wao wa kisiasa, na kusahahu masuala ya msingi kama hayo.

"Tupo mbioni kutoa rasimu ya mapendekezo ya katika mpya ambayo itakuwa na maslahi zaidi na wananchi kuliko uchu wa kuingia madarakani,"alisema.

Aliongeza wanamalizia kukamilisha taratibu za kuiandaa na baada ya mkutano mkuu wa chama hicho, rasimu itakuwa tayari kwa wadau na wanaharakati wote wanaodai katiba mpya.
 
jithada zote za kupata katiba mpya zinakaribishwa kwa mikono yote miwili...................
 
Hivi ni ya Rev Chris au Bw. Mapesa?????????? Mimi hawa I don't trust them-ni watafuta maslahi binafsi!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom