Updates za Uzini, vitimbi kuharibu uchaguzi vimeanza kwa kuwatumia masheha

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,070
Kwa ujumla kampeni za CHADEMA zinakwenda vyema. Kampeni zetu si za siri. CCM ambao ndiyo hasa tunapambana nao hapa Uzini wanahangaika kweli. Wameshikwa pabaya. CUF wanajaribu kufurukuta, kwa nia tu ya kutaka kuiharibia CHADEMA si kushinda. Maana wanasema itakuwa iabu kubwa kama yaliyowatokea Igunga, yatawatokea pia hapa Zanzibar. Kwa sababu dalili za hali hiyo zinaonekana wazi. CHADEMA wamekuja kunashindana. Uzini wanajua hivyo. Zanzibar mjini wanajua hivyo.

Kudhihirisha kuwa hali ni mbaya kwa CCM, sasa wameanza kuwatisha wananchi. Majuzi CCM wamepiga gari la CHADEMA mawe. Wameanza mtindo wa kuwakusanya wananchi mahali kwa nia ya kuwashawishi lakini pia wanawatisha. Wale wasiokuwa wenyeji, wameambiwa watahamishwa iwapo watapigia kura CHADEMA. Jimbo la Uzini lina mchanganayiko mzuri sana wa watu wa Visiwani na Bara. Waluguru, Wanyamwezi, Wasukuma na wengine kibao.

Kuna taarifa zimepatikana pia kuwa yameanza kutolewa maelekezo kwa askari wa moja ya vikosi vya ulinzi Zanzibar (kama mmekuwa mkifuatilia siasa za Visiwani, mtajua ni vikosi gani hutumika sana) kuwafuatilia vijana, kuwatisha, kuwapiga na kuvamia kaya kwa ajili ya kuchukua vitambulisho vya kupigia kura.

Masheha wamepewa amri kuandika majina ya vijana, akina mama na wazee wanaoonekana wazi kabisa kusapoti mabadiliko na kuelekeza kura zao CHADEMA. Baadhi wameanza kutekeleza maagizo hayo.

Mmoja aliyefuatwa na makamanda wetu maeneo ya Miwani, baada ya wananchi kulalamika kwetu kuwa wananyang'anywa vitambulisho vya kupigia kura na sheha wao, Sheha huyo amekir akisema kuwa mwananchi aliyemyang'anya ni mlevi. Sheria ya wapi inamruhusu Sheha kuchukua kitambulisho cha mpiga kura cha 'mlevi'. Ili iweje? Anataka kukifanyia nini? Akina mama wengine nao pia wamekwenda kwa makamanda wetu maeneo ya Ghana, wakilalamika kuwa wamefuatwa na Sheha akitaka vitambulisho vyao. Akavichukua.

Kwa Zanzibar, Sheha ni mtu anayepewa zaidi ya heshima. Anaogopwa. Nafikiri ni sawa na Katibu Kata hivi kwa huko bara. Wameamua pia kuwatumia wazee ili wawatishe vijana. Hili halijafanikiwa sana. Maana wazee nao, with exceptionals, wamepigwa nondo kali, hasa kusalitiwa kwa shabaha na malengo ya mapinduzi, wameitikia mwito wa kusimamia haki na uwajibikaji wa watawala.

Haya tuliyatarajia mapema. Tunayajua. Tunapambana nayo kuyadhibiti. Maana ni moja ya dalili kila CCM wanapozidiwa na CHADEMA. Intimidations. Tumewapiga jukwaani big time brothers. Tumewapiga kwa hoja. Tumewapiga kwa sera, kuanzia masuala ya Muungano, Katiba mpya, hali ngumu ya maisha waliyonayo Watz, kushindwa kwa chama hiki ambako sasa kunadhihirika wazi kabisa na kuwa kiko kufani, kufa kwa upinzabi Zanzibar na ombwe la sauti za utetezi wa wananchi. Wananchi wametukubali. Wenzetu wameumia sana.

Wamedanganya kwa kusomba na kubeba watu kutoka mjini na maeneo mengine ya Uzini kila wanapofanya mkutano, haijasaidia. Matokeo yake wamekuwa wakihutubia watu wale wale tu, kila siku. Wakati CHADEMA wanakutana na watu tofauti kila siku, katika mikutano yao, maana hawana haja ya kubeba watu, wanakuja wenyewe kusikiliza nondo zinazopenya masikioni na kuburudisha ubongo. Kuhanikiza na kuhamasisha mabadiliko. Wanafurahi kuwasikiliza na kuwaangalia makamanda.

Kama mjuavyo tunapambana na CCM na wafuasi wake wengine kibao, vikiwemo baadhi ya vyama vya siasa, ukiwemo mfumo unaotegemewa kuwa katikati na kutenda haki. CHADEMA inawekeza kwa watu. Daima inajivunia nguvu ya umma, maana ukiamua kubadilika na kudai haki, hakuna anayeweza kusimama mbele kuzuia.

Kwa ujumla tayari tumeingia katika vichwa na akili za akina mama, vijana, wazee na watoto wa shule. Sasa si ajabu tena unapita hapa mjini Zanzibar na gari lenye picha za mgombea au bendera, unanyooshewa vidole viwili, alama ya V. Ushindi, amani na upendo. Unaambiwa pipooooooo's... Kwa Uzini ndiyo balaa zaidi watoto, vijana, akina mama hawaogopi tena kujitanabaisha na CHADEMA wazi wazi. Wapo wengine bado wanaogopa. Wanaogopa masheha, wanaogopa wazee wao. Kisa! Kusapoti mageuzi!

Uwanja wa mapambano ukiwekwa sawa, CCM ni weupe mno brothers. Asubuhi tu biashara inafungwa. Tunaelekea Arumeru Mashariki. Lakini swali la muhimu, hivi kama hata Zanzibar hawa jamaa wameshindwa kujiamini, watajiamini wapi sasa?
 
Kinachoonekana sasa ni kwamba CUF imekosa mvuto, kwakweli wajipange upya vinginevyo nafasi yao itachukuliwa na CHADEMA huko Zanzibar, nashuri pia kwa CCM kuacha siasa za vitisho, hayo mambo yamepitwa na wakati, tukubali kuwa Tanzania ya sasa sio ile ya zamani kwamba watu wataogopa vitisho. Tunashukuru kwa kutuhabarisha kinachoendelea Uzini
 
Sisi yetu macho.

Kwani siku zote debe tupu haliachi kuvuma. kazi kwenu.

msiogope ni vivuli vyenu wenyewe hivyo
. Msilete sababu kwa kuona mnashindwa
 
Sisi yetu macho.

Kwani siku zote debe tupu haliachi kuvuma. kazi kwenu.

msiogope ni vivuli vyenu wenyewe hivyo
. Msilete sababu kwa kuona mnashindwa
I can see this coming out in your back!!!
images
 
Sisi yetu macho.

Kwani siku zote debe tupu haliachi kuvuma. kazi kwenu.

msiogope ni vivuli vyenu wenyewe hivyo
. Msilete sababu kwa kuona mnashindwa

Kwenye uchaguzi kuna vitu viwili, Kushinda na kushindwa. Sasa inategemea, unmeshindaje au umeshindwaje? Si suala la debe tupu. Mbona Igunga CHADEMA wamekubali.
 
Kwenye uchaguzi kuna vitu viwili, Kushinda na kushindwa. Sasa inategemea, unmeshindaje au umeshindwaje? Si suala la debe tupu. Mbona Igunga CHADEMA wamekubali.
Si kukubali tu bali pia kujivunia kile tulichopata pamoja na rafu kidoogo tulizochezewa yeye mwenyewe huyo ni shahidi
 
Baada ya Uzini, Arumeru nayo iko kwenye ramani. Nchi hii ya ajabu! Kila mwaka ni uchaguzi!!
 
Baada ya Uzini, Arumeru nayo iko kwenye ramani. Nchi hii ya ajabu! Kila mwaka ni uchaguzi!!

Ofcourse ni suala ambalo linahitaji kuchambuliwa na kufanyiwa kazi. Ukilingalia kwa macho mawili, bila makengeza ya na namna yoyote ile utaona implications zake!
 
Sisi yetu macho. Kwani siku zote debe tupu haliachi kuvuma. kazi kwenu. Msiogope ni vivuli vyenu wenyewe hivyo. Msilete sababu kwa kuona mnashindwa

Kwa maneno yako hayo na namna Uzini kwa sasa palivyo, umewachambua vizuri sana CCM au magamba. Asante.
 
Finally tutadai uchaguzi haukuwa huru,chadema too much possesion lakini kuscore tabu,mbwembwe kibao,mwende nanyi ukapige kura,viongozi hawachaguliwi kupitia humu
 
Kila la kheri makamanda,mie nimefunga sili wala sinywi ili mfanikiwe na ninaimani Mungu atajibu maombi yangu,vipi Kamanda Zito kishatia timu huko??
 
Wazenj kwa kujaa tele mikutanoni na kusikiliza ni wazuri sana lakini kazi ipo kwenye kisanduku Johmbaaaaaaaa (HAWADANGANYIKIIII)! Labda mupate kura za hao Wanyamwezi, Waruguru na Wakurya ambao walipewa vitambulisho vya Uzanzibapri na CCM ijapokua hawakustahiki! Nawashauri CHADEMA muanze kutafuta LESSO za kujifutia machozi mapema siku inakaribia hiyooooo.
 
Back
Top Bottom