Updates za kikao cha Wakuu wa Idara za Rasilimali watu Dodoma

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
1. Serikali imetoa Waraka mpya wa posho za kujikimu ndani ya nchi utakaoanza kutumika tarehe 01.07.2022. Posho husika zimepanda kwa majiji/manispaa kuwa hadi 150,000 na Makao makuu ya Mikoa na Wilaya na sehemu zingine ulingana na scale za Mishahara.

2. Serikali imetoa Waraka mpya wa posho za masaa ya ziada extra duty allowance utakaoanza kutumika 01.07.2022. Maafisa 60,000/= kwa siku, Watumishi ngazi ya kati kama PS, makarani na madereva ni 40,000/= kwa siku na Operational service kama Walinzi na Wahudumu ni 30,000/= kwa siku.

3. Serikali imefuta mfumo wa OPRAS katika kupima utendaji kazi watumishi. Umeanzishwa mfumo mpya wa Online unaoitwa PEPMIS ambao kila mtumishi ataujaza na atapimwa kulingana na mahitaji ya kazi ya kada yake kuanzia tarehe 01.07.2022
 
Posho za walimu walio mazingira magumu na wanaofanyishwa kazi kila siku mpaka jioni na jumamosi= HAKUNA
 
Hii nzuri sana Zile karatasi zilikuwa zinachosha na katika ujazaji na ufatiliaji naimani utaleta matunda zaid kuliko opras kama elimu ya utumiaji itatolewa kwa watumishi walio na umri mkubwa na mazingira ya vijijini
 
Back
Top Bottom