Kabisaa.. Sijawahi kulala ndani kwa mafua ila haya yalinilaza ndani siku tano huku nikila mananasi na kunywa pepsi tu.Nadhani hii ilikuwa ndio Corona kibongo bongo!!View attachment 1394734
Kabisaa.. Sijawahi kulala ndani kwa mafua ila haya yalinilaza ndani siku tano huku nikila mananasi na kunywa pepsi tu.
Hii ilikuwa aina nyingine ya covid 19.. homa yake ilikuwa si mchezo.Mimi mchai mchai ndiyo ulioniokoa na vitunguu swaum.
Unakohoa mpaka damu, kifua kinabana balaa
Sent from my iPhone using Tapatalk
Ni doctor au mtabiri au ukiwa na hela unaweza kujua yajayoBill gate alisema huu ugonjwa utakuja kuua billions of people in Africa
Afrika tupo bilioni Moja ,ulisema billions of people unakua hujielewi na huyo aliyekudanganya nae hajielewiBill gate alisema huu ugonjwa utakuja kuua billions of people in Africa
Hamia Marekani Dada!Hili li nchi hili bure kabisa ngoja niishie hapo
Hii ndiyo mfano wa deficity and insufficience ya sheria tunazotunga zinakuwa rules and siyo sheria. Sheria lazima iwe ama iangalie exceptions. Magonjwa ya milipuko siyo magonjwa ya kufedhehesha wala kubeza na hivyo kutangaza ilipasa kwa kuwa inaweza kuponya kuanzia familia yake, jiarani yake, wafanyakazi wenzake ama watu wengine tu. Hii sheria inafanya kuwe na deficity ya benefit ya sheria yenyewe katika circumstance ya magonjwa ya milipuko. Magonjwa ya milipuko yana pattern mbaya sana na hayajali na mtu yeyote ni susceptible. Tumeona duniani jinsi hadi wataalamu wa afya wamekwenda tena waliobobea katika virology specifically huyu CORONA wamekwenda. Sasa tunaficha kwa faida ya kuzuia maambukizi au kwa faida ya wizara ya afya au kwa faida ya mgonjwa dhidi ya umati wa wananchi wote? From layman point of view hili haliko sawa hasa katika magonjwa ya milipuko...hii rule irekebishwe iwe sheria including exceptions hizi. Sheria without exception is a blind sheria na hivyo haiwezi kuona haki, ikiwa kipofu atatakiwa kuona dunia itapita na vitu vyake vyote. Sheria inakuwa sheria ikiwa na makali yake, considerate, covering exceptions ili iweze kutoa haki. Hapa kwenye magonjwa ya mlipuko ... hii sheria imetunyima haki watanzania .. hata hii ya kujua tu .. ili kuchukua tahadhari. Tahadhari ni pana na kwanza inahitaji habari kamili na sahihi.. mfano sasa tunaangalia sana na kusema mkuu umetoka nchi zenye mlipuko .. tukupime na tunakushuku kwa hali ya juu zaidi. Sasa hii ni habari inavyoweza kusaidia dhidi ya tahadhari.. pamoja na mambo mengine mfano umri, magonjwa mengine (pre-existing disease conditions) na habari zote zinazopasa kujumuishwa katika tahadhari. Hii ndiyo habari kamili na sahihi. Vinginevyo umri wa mgonjwa pia ni habari ila si kamili, jinale nani, kabila gani, anaishi wapi anafanya nini, amepataje uambukizo, alitembelea maeneo gani kabla na baada ya uambukizo. Nadhani hili lipitiwe upya na waziri mwenye dhamana na awatendee watanzania haki kupitia bunge tukufu?.
Common sense is not common anymore. Politics politics politics politics kwenye kilaaa jambo.Natambua umahiri wetu wa kuvifanya vitu serious kuwa mizaha. Natambua ujuzi wetu wa kuyageuza majanga kuwa manufaa ya kisiasa.
Hivi ni kipi kikubwa tumekifanya kama taifa cha serious kujikinga na hili gonjwa linalotaka kuwa janga la dunia?
Nimemsikia Waziri wa Afya akikutangazia umuhimu wa kutoshikana mikono wala kukumbatiana wakati wa kusalimiana kama ilivyo jadi yetu. Wanasiasa wakalibeba hili mzobe mzobe. Mengine yote sidhani kama yamepewa kipaumbele.
Waziri katangaza kila mkoa utenge maeneo maalum ya kuchunguza wenye dalili na viashiria vya huu ugonjwa.
Je, hili limetekelezwa?
Je, kuna vifaa ya kutosha kwenye hili?
Je, bajeti imetoka wapi?
Je, kuna wahudumu wa dharura wenye uelewa na huu ugonjwa wameandaliwa?
Je, sahihi ni kutenga vituo kila mkoa ama kila wilaya?
Je, mpaka sasa ni mikoa mingapi imelitekeleza hili?
Je, kuna changamoto yoyote?
Je, kuna kipindi maalum kwenye vyombo vya habari kutoa mapya ya kila siku kuhusiana na huu ugonjwa?
Hakika maswali ni mengi sana. Lakini nilichokiona kwenye huu ugonjwa ni mizaha na kukosa umakini. Hatuna takwimu rasmi zozote mpaka sasa za chochote kuhusiana na huu ugonjwa. Hatujaona umakini wowote kwenye maandalizi ya dharura. Chukulia mfano mkoa wa Pwani kutoka Mkuranga mpaka Bagamoyo utenge kituo kimoja tu cha ukaguzi wa corona, inawezekana kweli!?
Kinachopigiwa chepuo sasa ni kusalimiana bila kushikana mikono, eti kugongesha miguu. Mmh! Tumeiona kwa viongozi, lakini nyie msioshikana mikono sasa si mlikaa chumba kimoja kwa madakika mengi tu? Je, mlitumia viziba midomo na pua?
Hivi kwani corona ni ugonjwa wa ngozi? Iweje wachezaji uwanjani wazuiwe kusalimiana kwa kushikana mikono eti ni mojawapo ya kampeni ya kupambana na corona wakati huo huo wachezaji haohao watakuwa pamoja uwanjani kwa dakika 90+ wakishikana, wakivutana, wakiangukiana wakipumuliana? Vipi na wale mashabiki watazamani kwa maelfu walio majukwaani? Tuna abiria kwa maelfu wanasongana kwenye vyombo vya usafiri. Kwenye masoko. Kila mahali.
Bado hatuko serious na mizaha ndio imetawala kupitia siasa. Mungu pekee ndio anatubeba. Kitengo cha dharura kitaifa hakijasema chochote. Kipo kimya kabisa. Vyombo vyetu vya habari ni siasa na wanasiasa mwanzo mwisho. Viziba pua na midomo vimepanda bei maradufu. Box lilikokuwa linauzwa elfu 10 piece 50 sasa hivi linauzwa elfu 40 na hapo ugonjwa haujachanganya. Ukithibitika upo nchini na tukatakiwa kutumia hivyo vifaa tutafanyaje?
Jr