Updates: Simba SC vs Yanga SC Uwanja wa Taifa

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Wanajamvi hasa wanaspoti

Ile siku hatimaye imewadia na muda mfupi ujao Simba na Yanga watashuka dimbani kutafuta mbabe baina yao ingawa Simba ni bingwa tayari wa ligi kuu. kama kawaida tupeane taarifa kwa wale mlioko uwanjani na wale mtakaokuwa mnasikiliza katika radio ili walio mbali wafaidike pia.

Sina hakika kama kuna TV itaonyesha. Nikipata taarifa nitawaarifu ama tuarifiane humu
updates: ft simba 5 yanga 0
 
mwenye updates za vikosi pia tunaomba atuwekee hapa

VIKOSI:
SIMBA: Juma Kaseja, Nassor Chollo, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kelvin Yondan, Patrick Mafisango, Uhuru Suleiman, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Emanuel Okwi.

BENCHI: Ally Barthez, Derrick Walullya, Obadia Mungusa, Victor Costa, Ramadhan Singano, Gervais Kago na Salum Machaku.

YANGA: Yaw Berko, Nsajigwa Shadrack, Oscar Joshua, Nadir Cannavaro, Athumani Iddi, Juma Seif, Shamte Ally, Haruna Nironzima, Davies Mwape, Kenneth Asamoah na Hamisi Kiiza.

BENCHI: Shaaban Kado, Omega Seme, Zuberi Ubwa, Job Ibrahim, Bakari Mbega, Nurdin Bakari, Idrisa Senga, Pius Kisambale na Geoffrey Bonny.

Kwa hisani ya Shaffi Dauda
 
Ripota wenu Masuke tayari niko uwanjani na watu ni wengi kwa upande wa jukwaa la Simba lakini kwa upande wa jukwaa la Yanga si wengi sana huenda wakaongezeka baadaye maana mechi inaanza saa kumi, Vikosi vinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:-Simba: Juma Kaseja, Said Chollo, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Patrick Mafisango, Uhuru Selemani, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Emmanuel Okwi; Yanga: Yaw Berko, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Chuji, Cannavaro, Juma Kijiko, Shamte Ali, Haruna Niyonzima, Davies Mwape, Asamoah na Hamis Kiiza. Hivyo ndo vikosi kwa timu zote mbili kama kutakuwa na mabadiliko nitawajulisheni wasomaji wote wa jukwaa hili la sports.
 
Simba tunaweka kikosi cha pili. Cha kwanza kina majukumu ya kupambana na wanaume wenzetu Sudan kule. Hatuwezi kuwachosha kwa mechi na watoto wa mitaa ya mafurikoni.
 
Simba tunaweka kikosi cha pili. Cha kwanza kina majukumu ya kupambana na wanaume wenzetu Sudan kule. Hatuwezi kuwachosha kwa mechi na watoto wa mitaa ya mafurikoni.
Kama yanga wataonyesha nidhamu basi tutawaachia maana ilivyo kama tukiwafunga jangwani hakuta kalika...lakini wakileta ujeuri tuna watandiaka vitatu kama kawaida yetu....
 
Wachezaji wa Yanga ndo wanatoka kwa ajili ya kupasha misuli na wameshangiliwa sana na mashabiki wao japo ni wachache.
 
Kila la heri Simba, mechi ya leo ni muhimu kushinda, ita-boost saikolojia ya wachezaji kwenye game zijazo za CAF,
achilia mbali mikogo ya kumfunga mtani.
 
Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania msimu huu Simba sports Club, wekundu wa Tanzania nao ndo wanatoka kwa ajili ya kuipa joto misuli yao.
 
Mungu ibariki SIMBA S S, ipate ushindi ili wapokee kombe la ubingwa kwa heshima KUU
 
Kwa mnaongalia ligi ya Uingereza msisahau kutupa updates za New Castle na Man City.
 
Lakini jamani hii tabia ya kuanzisha uzi halafu haupo eneo la tukio mbona naona inazido kuota mizizi!!!!

Kwani kuna ubaya ukasubiri walio eneo la tukio kuanzisha mada na wewe ukawa mfuagiliaji?

Mfano, mimi nipo Morogoro au Dodoma naanzisha uzi kama huu nasema,

Kwa wale mliopo uwanja wa Taifa naomba kupeane updates kwa mechi ya Simba na Yanga.

Kwa haraka huwezi kuona shida, lakini mnawapa kazi MoDs kuweka updates toka post za watu mbalimbali ili kukubeba tu kwa sababu umewahi kuanzisha uzi.

Tabia hii siipendi kabisa.
 
Wapenzi na Mashabiki wa Yanga naona leo wameamua kuhujumu mapato ya mechi ya leo, walioko uwanjani ni wachache sana labda kwa sababu wanajua mechi ya leo haiwaongezei chochote wao zaidi ya kulinda heshima endapo watawafunga wapinzani wao.
 
VIKOSI:
SIMBA: Juma Kaseja, Nassor Chollo, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kelvin Yondan, Patrick Mafisango, Uhuru Suleiman, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Emanuel Okwi.

BENCHI: Ally Barthez, Derrick Walullya, Obadia Mungusa, Victor Costa, Ramadhan Singano, Gervais Kago na Salum Machaku.

YANGA: Yaw Berko, Nsajigwa Shadrack, Oscar Joshua, Nadir Cannavaro, Athumani Iddi, Juma Seif, Shamte Ally, Haruna Nironzima, Davies Mwape, Kenneth Asamoah na Hamisi Kiiza.

BENCHI: Shaaban Kado, Omega Seme, Zuberi Ubwa, Job Ibrahim, Bakari Mbega, Nurdin Bakari, Idrisa Senga, Pius Kisambale na Geoffrey Bonny.

Kwa hisani ya Shaffi Dauda

Inaonekana unabahatisha vikosi; Omega Seme wa Yanga yuko na timu ya vijana sudan, au wamerudi leo? hata kama amerudi si rahisi apangwe leo.........
 
Timu zote mbili zinarudi vyumbani kwa ajili ya Maandalizi ya mwisho mwisho tayari kwa Mtanange unaotarajiwa kuanza saa kumi kamili.
 
Jamani update zikiwa za kusua sua msinilaumu, maana nataka niangalie mpambano kwa asilimia mia moja.
 
Vikosi vyote vinatoka vikiongozwa na watoto na bendera yao ya Fifa ya fair play, Simba kama kawaida wamepiga jezi Nyekundu kwa juu, bukta Nyeupe na soksi Nyekundu, Yanga nao juu ni kijani bukta njano na soksi ni njano.
 
Back
Top Bottom