kweli nchi haina serikali
Watanzania bwana. Ila ni kawaida kwa wapiga majungu sishangai. Hivi kumbe kuna watu wanataka suluhu kati ya madaktari na Serikali isiwepo ili waendeleea kupiga majungu, mara Serikali haisikilizi matatizo, mara Serikali inacheza na afya za wananchi wake. ili iweje sasa ina maana kweli hilo nalo limekuwa siasa kweli, Eti Chadema wanasema watatoa takwimu za vifo vilivyotokana na athari za mgomo wa madaktari, kisa eti kiongozi wao kafariki huko Muhimbili. Hizi si siasa? Kumbe kuna kila sababu ya kuamini kwamba mgomo huu ulikuwa na mkono wa baadhi ya wanasiasa. Angalia hata contribution mbalimbali za watu humu zinazohusiana na mgomo huo, ni ushabiki tu, watu wanathamani mgomo uendelee ili wafurahi ili ionekane kwmba Serikali imeshindwa.
Serikali iendeleze mazungumzo na Madaktari nao wakubaliane na Serikali badala ya kusikiliza maneno ya uchochezi. wapo watu ambao kwa makusukdi tu hawaitakii mema Nchi yetu. Wengine walishatamka kwamba Serikali haitatawalika na kwa maana hiyo wanafikiri kauli zao zisipotimia basi wataonekana kama ni manabii wa uongo na kuanzisha vituko vya kushawishi watu kugoma , kufanya fujo n.k. Kamwe kwa akili zangu siwezi kuwaona wanasiasa wa aina hiyo kama watetea wanyonge. Ni wachochezi/wabinafsi/wenye chuki/husuda n.k. Tuwaepuke hao. Tuache Serikali ifikie muafaka na Wafanyakazi wake ili chi isonge mbele. Kama kuna watu wana damu ya kupenda shari waende somalia, na kwingineko.
kwa ujumla, serikali lazima iwajibike!
Hebu rudia kujisoma kwanza halafu urudi utuambie hapa mpenda majungu ni yupi hapa?
Mod tunaomba uunganisha hz POST PLZ!Katika kuhaha kwa serkali kujaribu kutafuta suluhu ya mgomo wa madaktari leo serikali imekwenda kuonana na madaktari wakiwa katika vikao vyao visivyo na kikomo (extended meetings) pale starlight hotel. Delegation ilikuwa na wajumbe wafuatao: Waziri wa Utumishi - Hawa Ghasia, Waziri wa Afya - Haji Mponda, Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa serikali - Deo Mtasiwa
Ujumbe wa serikali ambao kimsingi walisema wametumwa na Waziri Mkuu ulikuja kwa ajili ya kusikiliza madai ya madaktari na wao kujaribu kutoa utatuzi kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wao.
Hata hivyo madai ya madaktari kwa mara nyingine tena waliambiwa na wao kupewa nafasi ya kutoa majibu ambayo walisema mengi kati ya hayo yanazungumzika na kwamba suala la interns (madaktari waliopo katika mafunzo katika vitendo) serikali imekubali kuwarudisha Muhimbili bila masharti yeyote. Suala la nyumba, risk allowance na mengineyo wamekubali kukaa na madaktari kupitia viongozi wao ili kujaribu kupata suluhu.
Hata hivyo madaktari wameazimia kuendela na vikao vyoa visivyo na kikomo mpaka hapo madai yao yatakapopatiwa ufumbuzi na kwambwa wajumbe waliambiwa wamfikishie waziri mkuu madai yao
Nawasilisha