Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Nimepokea simu kuwa Waziri mtarajiwa wa Nishati na Madini, ndg yetu mpendwa Prof. Sospter Mhongo kashinda Musoma Vijijini (Butiama) japo sija ambiwa idadi ya kura.
 
Wakati vyama vikiwa kwenye mchakato wa kuwachagua watia nia wao ili kuwasimamisha kugombea nafasi za ubunge na udiwani katika majimbo ya chaguzi, chama cha Mapinduzi kipo katika hali mbaya zaidi. CCM ni chama kikongwe zaidi Tanzania ambacho historia yake inaanzia tangu Tanganyika African Association (1929) kisha Tanganyika African National Union (1954) na baadae chama cha Mapinduzi baada ya kuungana TANU na Afro-Shiraz Party 1977. Licha ya kuwa chama kikongwe, CCM haina jipya la kujivunia katika kuwaletea watanzania maendeleo.

Hii imepelekea watanzania wengi hasa wanaojitambua kuamua kutafuta vyama vingine kuviunga mkono ili vichukue dora na kuwaletea watanzania maendeleo yanayoendana na karne ya 21. Katika hili, ndipo Waziri mstaafu Edward Ngoyai Lowassa, Mzee wamatumaini alipoamua kuungana na CHADEMA katika mbio za kuchukua dora tarehe 25/10/2015.

Hali hii ya kuhama kwa Lawassa imepandisha homa ya uchaguzi kwa upande wa CCM baada ya kugundulika kuwa Lowassa amewaacha baadhi ya wana-CCM kuendelea kufanya kazi ndani ya chama kwa maslai ya upinzani (Lowassa). Wenyeviti na Makatibu wa kata wa CCM wanaofanya kazi kwa maslai ya Lowassa waliweka utaratibu wa kupiga kura za kuwachagua wagombea Ubunge na Udiwani. Utaratibu huu uliangalia zaidi majina yaliomdhamini Lowassa wakati anatafuta wadhamini CCM kugombea Urais ndiyo yalipewa kipaumbele kupiga kura kuchagua mgombea Ubunge na Udiwani ambaye tayari walishamuanda. Kitendo hiki kimepelekea kuchaguliwa wagombea Ubunge na Udiwani ambao hawakubaliki kwa wanainch ili washindwe na wapinzani (Team Lowassa & UKAWA) washinde kiurahisi uchaguzi. Hii imesababisha hata mmoja kati ya wagombea Udiwani kutoruhusiwa kuingia kupiga kura kwasababu jina lake halipo kwenye daftari.

Pia, wana-CCM wanadhihilisha kukumbwa na homa kali ya uchaguzi kwa kutumia mda wao mwingi kumjadili Lowassa (upinzani) badala ya kumjadili Magufuli (CCM)

Naomba kuwasilisha!
 
Mgombea nafasi ya Ubunge kupitia tiketi
ya chama cha mapinduzi Ndugu Devis
Mosha ameanza kupigania kulirudisha jimbo la moshi mikononi mwa c.c.m kwa udi na uvumba, baada ya style iliyozoeleka ya kutumia magari Jana tarehe 31/07/2015 zilianza harakati za kipekee kwa
kutumia helicopter huku ikipita maeneo ya moshi na kudondosha vikaratasi vyenye kuhimiza mabadiliko moshi,kila la heri Mkuu.

anajisumbua....
 
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, anaongoza katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Habari kutoka jimboni humo zinasema Nyalandu ambaye pia ni waziri wa maliasili na utalii, anaongoza katika vituo vya kata zote huku akiwaacha mbali wapinzani wake.

Update:

Katika kata ya Ilongero.
Nyalandu 667
Mpombo 88
Monko 60

Kata ya Maghojoa:
Nyalandu 743
Monko 72
Mpombo 26
Aron 16
Mungwe 15

Wengine wanazitiki kabla hazijapigwa, mmeyasikia ya Tarime Mjini na Tarime Vijijini?
 
Matokeo ya kura za maoni huko Arumeru Mashariki yamempitisha ndugu John D Pallangyo ambaye sasa atapambana na dogo janja!

Ikumbukwe kuwa Jon D alisemekana kuwa ni Team lowasssa na sasa lowasa yuko chadema na atatakiwa kumsupport Nassari.

Isitoshe John D alikuwa anapambanishwa na Sioyi ambaye ni baba mkwe wa lowassa nadhani anaweza kuingia chadema.

Challange ni moja tu je lowassa atamtosa John D waliyeanza naye safari ya matumaini?au atamtosa nassari mbunge wa Chadema?

Mbowe wakati anawalaghai wanachadema jui ya ujio wa lowassa hakuconsider dialema kama hizi ambazo zitajitokeza sehemu nyingi nchini.

lowassa kaja Chadema peke yake na kuwaacha wenzake wa safari ya matumaini ccm!!

Dr Slaa yuko sahihi kwamba Chadema ilihitaji kutafakari na sio kukurupuka tu!

Scenario kama hii itatokea Arusha mjini pia!!!


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Wewe hujui strategy ya EL na Ukawa. EL anataka Ukawa iwe na Wabunge wake wengi kutoka upande wa pili. EL ana akili sana!
 
Back
Top Bottom