Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Jimbo la kibakwe simbachawene anagawa fedha kama njugu Jana hapa kwenye kitongoji cha msangambuya Kata ya mtera mnapanga foleni unapewa 10000/_ unaambiwa chagua simbachawene kwakweli mkoa wa Dodoma takukuru imelala kuliko mkoa wowote walikuwa wameuchuna tu naamini hata wao walipoozwa kwani simbachawene na mawakala wake wamegawa fedha mchana kweupe.binafsi nimepewa 10000 na kula simpi.
 
kila kituo kina projection ya wapiga kura,wakikamilika wanaweza hesabu lakini kanuni za chama hicho kuhesabu ni kuanzia saa 10 jioni

Imekuwa uchaguzi mkuu? kwa nini wahesabu jioni kama sio magoli ya mikono, leo watachinja wakikatwa waliotoa pesa nyingi
 
Mathias Byabato

Umefanya vyema kutuwekea live updates, kuna watia nia hapo sioni kama wana sifa...mfano Karamagi,Kamala alitutukana kuwa tule nkende kama wanatusumbua shambani.

Dr. Aman na Kagasheki nao wapumzishwe walau siasa za Bukoba zirudi katika mstari.
 
Last edited by a moderator:
Kata ya Stakishari Kipawa jimbo la Segerea Dar es Salaam uchaguzi umeahirishwa, baada ya sintofahamu kubwa kutokana na wanachama wengi wenye kadi za CCM kuibuka na majina yao kutokuwepo kwenye ledger book, hivyo kukosa sifa ya kupiga kura...ngumi na matusi yakaanza..kati ya watia nia udiwani na ubunge.....
 
Huko jimbo Chemba kwa Mzee wa kuongea na mwenye mbwaa vipi????? Nitanunua kinana baridi akiangukia pua
 
Kwa hali niliyoiona kwa jimbo LA Segerea na jimbo LA Ukonga Dar es Salaam, CCM wana mpasuko mkubwa sana, wanapigana wenyewe kwa wenyewe mchana kweupe huku wengine wakitamka wazi wazi kuwa hiki chama bora kife, hivyo UKAWA wakiweka watu makini katika majimbo haya ushindi ni wao asubuhi na mapema...Ujio wa Lowasa upinzani umepelekea wengi CCM kujiamini kuwa kama haki haitendeki bora twende upinzani ili chama dola CCM Kijifie zake
 
Hivi kwa nini wanatakiwa kwenda na kadi za kupigia kura na kadi za CCM kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.
 
Kukiwa na matukio lukuki ya rushwa ambayo yametikisa ngoma za masikio za watanzania,matukio hayo yanazidi kuota mizizi katika vitongoji na kata mbalimbali jijini Dar es salaam.

Nikiwa katika kata ya Mbagala sabasaba Mtaa wa Kizinga kunaonekana kukiwa na shughuli mbalimbali za chama tawala zinaendelea huku wajumbe na wagombea mbalimbali wa viti vya udiwani na ubunge wakihaha kutetea nyadhifa zao kwa kutoa kiasi cha shilingi 5,000/= mpaka 2,000/= kwa mwanachama mwenye kadi ya Kijani (ccm) Je mamlaka husika mko wapi?
 
jimbo la kibakwe simbachawene anagawa fedha kama njugu Jana hapa kwenye kitongoji cha msangambuya Kata ya mtera mnapanga foleni unapewa 10000/_ unaambiwa chagua simbachawene kwakweli mkoa wa Dodoma takukuru imelala kuliko mkoa wowote walikuwa wameuchuna tu naamini hata wao walipoozwa kwani simbachawene na mawakala wake wamegawa fedha mchana kweupe.binafsi nimepewa 10000 na kula simpi.

Huku kata ya Luhundwa Simbachawene na diwani aliyeko madarakani wameiba fomu za kupigia kura kutoka kijiji cha ikuyu kupeleka vijiji wanapokubalika, hata hivyo baadhi ya matawi wanachama wamegoma kupiga kura hadi fomu 400 zilizoibwa zirudi
 
Back
Top Bottom