Elections 2015 Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,783
66,962
Habari Wanajamvi,

Leo ndio ile siku inayosubiriwa kwa hamu hapa Mkoani Arusha, pale ambapo mgombea wa Urais kwa tiketi ya Ukawa Ndugu Edward Lowassa atakapotambulishwa rasmi mkoani hapa.

Hakika maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100%, Mkutano huu pia utashuhudia maelfu ya wanachama wa ccm mkoani hapa wakirudisha kadi zao na kuhamia rasmi Chadema.

Makamanda karibuni ili tupeane updates na kujulishana kile kinachoendelea.

Mkutano Unafanyika viwanja vya Tindigani, Kimandolu.
cc: Timu mahiri ya wanahabari ya Chadema Chadema kwanza Molemo Tumaini Makene
=======================================================================================

Updates:
Baadhi ya wanachama wamepiga kambi karibia na KIA ili kupata fursa ya kujumuika vizuri hapo baadae.

Wananchi mamia kwa maelfu wanazidi kushuka toka mjini kwenda KIA hakika hapatoshi, picha zitakuja punde tuu.


Edward Lowassa kashatua KIA, muda wowote msafara wa kuelekea Kimandolu utaanza.

Polisi wametanda MTO Nduruma kuzuia magari yenye Bendera za chadema na pikipiki zote zinazolekea KIA...

View attachment 276596
Arusha.jpg

SAM_0009.JPG
attachment.php


attachment.php






11899749_1011063825613128_6401811854898484674_n.jpg
attachment.php


============================================================
Tunaomba radhi Makamanda, kuna tatizo la Network leo hapa Arusha, hivyo inasababisha zoezi la uwekaji picha kuwa mgumu. Tunajitahidi kupambana wakuu.
11181090_844000892387032_6036706536539975914_n.jpg
attachment.php

IMG-20150815-WA0127.jpg

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php


11902572_844032525717202_2088289352271060428_n.jpg

attachment.php

Wanafunzi nao wakifuatilia mkutano kupitia madirisha ya shule
11898541_844026842384437_3521145624124665587_n.jpg


View attachment 276986
Lowassa na mama Lowassa wakifanyiwa matambiko ya Kimasai

11896027_769560393154937_3304267978777158586_n.png
Lowassa akihutubia wananchi Arusha.
==========================================================================================

Breaking news from Arusha

Waliojiunga na CHADEMA:
Laurence Masha anakabidhiwa kadi na Mbowe
Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara
Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha
Sioi Sumari
Yona Nko aliyekuwa mkiti ccm mkoa Arusha
Mgombea ubunge Simanjiro
Goodluck Sipira katibu wa ccm Arusha anatokea Longido
Wazee wa kimila wa kimasai nchi nzima
Wazee wa kimila wa kimeru wote wakiongozwa na Mshili Mkuu.


Ole Medeye:
Anaimba kuwa Mwambie Kikwete nimezinduka, ccm sirudi tena.
Nimejitoa ccm kwa sababu mbili kuu, ya kwanza dhuluma imezidi ndani ya ccm, wanaapa kinafiki kuwa watailinda katiba ya nchi wakati wanaivunga, pili rushwa imekithiri katika taifa hili, nilifikiri kupitia ccm ningeshiriki kupiga vita rushwa, lakini matokeo yake kumbe niliowaamini kupiga vita rushwa ndiyo wanaotoa rushwa.
Hivyo nimejiondoa ccm ili tuweze kurudisha maadili ya nchi.


Mzee Mtei:
Ninaambiwa kuwa muasisi wa hiki chama, roho yangu inadunda, nikiona umati huu na jinsi vyama hivi vimeungana nasikia furaha sana. Nashukuru kutuunga mkono, nawatakia kila la kheri katika safari hii ya ukombozi.
Ninashukuru sasa kwakuwa chama nilichokiasisi kimempata mtu wa kutupeleka ikulu


M/kiti wa ccm mkoa wa shinyanga Mgeja:
Nataka niseme maneno machache,
Kwanza juzi mpaka saa nne na dk 59 nilikuwa mwenyekiti wa ccm, saa tano na dk nikajitoa ccm, baada ya kugundua ndani ya ccm hakuna hakuna haki, nami nikaona nijiunge na chadema chama chenye haki.
Jana mmemsikia vuvuzela ikipiga kelele kuwa tunamfuata Lowassa, ningekuwa namfuata Lowassa ningeenda Monduli nyumbani kwake.
Nashangaa vuvuzela Nape eti nimehama chama kisa mtoto wangu ameangushwa ubunge, nataka nimwambie Nape kuwa nina uzefu wa kushindwa, nampa Salamu kuwa tutakutana Mtama.
Nimepigiwa simu zaidi ya 800 zote zinanipongeza, simu sita tu zilikuwa zinanisikitia.
Niseme tu nyumba ya ccm inaungua unasubiri nini kuaga?
Nataka niwaambie Nape na wenye akili kama ya Nape kuwa waeleze wale vigogo wanaojihusisha na ujangili(Kinana) Waeleze fedha za escrow ziko wapi, ccm ni kichaka cha waizi, ccm waeleze kwanini shilingi inashuka, ccm mwulizeni Kikwete unatuachaje? Ataacha umaskini, chuki, husda na rushwa.
Pombe mwisho kaunta, mtaani ni Lowassa

James Mbatia:
Sauti ya umma ni sauti ya Mungu, Mungu akiamua kitu inakuwa. Naanza na hili kwasababu mm ni mjumbe wa kamati ya bajeti ya bunge, najua mateso wanayopata polisi, najua Arusha damu za watu zimemwagika kwa ubabe wa jeshi la polisi.
Polisi leo wanadiriki kumkaribisha Rais nyumbani kwake kwa mabomu. Namwambia Kikwete nchi hii siyo ya utawala wa kijeshi. Duniani huwezi kutumia nguvu ya dola kutawala raia.
CCM wamelifikisha deni la taifa ambalo kila mtanzania anadaiwa laki nane na 55,000.
Namtahadharisha Mkuu wa polisi na rpc wa Arusha nawatahadharisha kuwa wao ndiyo wanaohatarisha amani ya nchi yetu, sasa tumechoka. Polisi constebo mshahara wako haufiki hata laki tano, unatumwa na mtu anayelipwa mil 3 na shangingi una akili kweli wewe?
Polisi wamekuwa kama panya mama sharubu baba sharubu na mtoto sharubu, kila moja lwake.
Tanzania bila ccm inawezekana


Godbless Lema:
Nasikitika Rais wetu amepokelewa na mabomu, vijana wamezuiwa.
Wanachokifanya hivi sasa ni kutengeneza mazingira ya kuiba kura kutufundisha uwoga.

Nampa taarifa IGP kuwa kama wamezoea kuua sisi tumezoea kuwa maiti.

Dhambi mbaya kuliko zote duniani ni uwoga.

Polisi wanamzuia Rais wetu asishiriki msiba wa rafiki yake kwa hofu tu akienda atamfunika kikwete.

Namuahidi Rais Lowassa kuwa kura yake Haitaibiwa.

Watu wakiamini kuwa hatuwezi kushinda kwa njia ya demokrasia, watatafuta mbinu nyingine kushinda.

Usalama mwambieni Kikwete yeye sasa ni rais, lkn hii nchi siyo ya mama yake wala ya baba yake
 

Attachments

  • SAM_0019.JPG
    SAM_0019.JPG
    758 KB · Views: 46,459
Du hatari sana,mwaka huu kuna mengi ya kujifunza katika chaguzi zijazo tuombe uzima tufike 0kitoba ishirini na tano
 
naanza sfr kwenda kwa lowassa mapema hii
kamanda utakae hisi njaa na kiu nina mihogo ba maji ..

tusonge mbele comrades
 
Back
Top Bottom