Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA | Page 66 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mussolin5, Aug 15, 2015.

 1. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 17,578
  Likes Received: 61,877
  Trophy Points: 280
  Habari Wanajamvi,

  Leo ndio ile siku inayosubiriwa kwa hamu hapa Mkoani Arusha, pale ambapo mgombea wa Urais kwa tiketi ya Ukawa Ndugu Edward Lowassa atakapotambulishwa rasmi mkoani hapa.

  Hakika maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100%, Mkutano huu pia utashuhudia maelfu ya wanachama wa ccm mkoani hapa wakirudisha kadi zao na kuhamia rasmi Chadema.

  Makamanda karibuni ili tupeane updates na kujulishana kile kinachoendelea.

  Mkutano Unafanyika viwanja vya Tindigani, Kimandolu.
  cc: Timu mahiri ya wanahabari ya Chadema Chadema kwanza Molemo Tumaini Makene
  =======================================================================================

  Updates:
  Baadhi ya wanachama wamepiga kambi karibia na KIA ili kupata fursa ya kujumuika vizuri hapo baadae.

  Wananchi mamia kwa maelfu wanazidi kushuka toka mjini kwenda KIA hakika hapatoshi, picha zitakuja punde tuu.


  Edward Lowassa kashatua KIA, muda wowote msafara wa kuelekea Kimandolu utaanza.

  Polisi wametanda MTO Nduruma kuzuia magari yenye Bendera za chadema na pikipiki zote zinazolekea KIA...

  View attachment 276596
  Arusha.jpg

  SAM_0009.JPG
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  ============================================================
  Tunaomba radhi Makamanda, kuna tatizo la Network leo hapa Arusha, hivyo inasababisha zoezi la uwekaji picha kuwa mgumu. Tunajitahidi kupambana wakuu.
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]
  Wanafunzi nao wakifuatilia mkutano kupitia madirisha ya shule
  [​IMG]

  View attachment 276986
  Lowassa na mama Lowassa wakifanyiwa matambiko ya Kimasai

  11896027_769560393154937_3304267978777158586_n.png
  Lowassa akihutubia wananchi Arusha.
  ==========================================================================================

  Breaking news from Arusha

  Waliojiunga na CHADEMA:
  Laurence Masha anakabidhiwa kadi na Mbowe
  Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara
  Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha
  Sioi Sumari
  Yona Nko aliyekuwa mkiti ccm mkoa Arusha
  Mgombea ubunge Simanjiro
  Goodluck Sipira katibu wa ccm Arusha anatokea Longido
  Wazee wa kimila wa kimasai nchi nzima
  Wazee wa kimila wa kimeru wote wakiongozwa na Mshili Mkuu.


  Ole Medeye:
  Anaimba kuwa Mwambie Kikwete nimezinduka, ccm sirudi tena.
  Nimejitoa ccm kwa sababu mbili kuu, ya kwanza dhuluma imezidi ndani ya ccm, wanaapa kinafiki kuwa watailinda katiba ya nchi wakati wanaivunga, pili rushwa imekithiri katika taifa hili, nilifikiri kupitia ccm ningeshiriki kupiga vita rushwa, lakini matokeo yake kumbe niliowaamini kupiga vita rushwa ndiyo wanaotoa rushwa.
  Hivyo nimejiondoa ccm ili tuweze kurudisha maadili ya nchi.


  Mzee Mtei:
  Ninaambiwa kuwa muasisi wa hiki chama, roho yangu inadunda, nikiona umati huu na jinsi vyama hivi vimeungana nasikia furaha sana. Nashukuru kutuunga mkono, nawatakia kila la kheri katika safari hii ya ukombozi.
  Ninashukuru sasa kwakuwa chama nilichokiasisi kimempata mtu wa kutupeleka ikulu


  M/kiti wa ccm mkoa wa shinyanga Mgeja:
  Nataka niseme maneno machache,
  Kwanza juzi mpaka saa nne na dk 59 nilikuwa mwenyekiti wa ccm, saa tano na dk nikajitoa ccm, baada ya kugundua ndani ya ccm hakuna hakuna haki, nami nikaona nijiunge na chadema chama chenye haki.
  Jana mmemsikia vuvuzela ikipiga kelele kuwa tunamfuata Lowassa, ningekuwa namfuata Lowassa ningeenda Monduli nyumbani kwake.
  Nashangaa vuvuzela Nape eti nimehama chama kisa mtoto wangu ameangushwa ubunge, nataka nimwambie Nape kuwa nina uzefu wa kushindwa, nampa Salamu kuwa tutakutana Mtama.
  Nimepigiwa simu zaidi ya 800 zote zinanipongeza, simu sita tu zilikuwa zinanisikitia.
  Niseme tu nyumba ya ccm inaungua unasubiri nini kuaga?
  Nataka niwaambie Nape na wenye akili kama ya Nape kuwa waeleze wale vigogo wanaojihusisha na ujangili(Kinana) Waeleze fedha za escrow ziko wapi, ccm ni kichaka cha waizi, ccm waeleze kwanini shilingi inashuka, ccm mwulizeni Kikwete unatuachaje? Ataacha umaskini, chuki, husda na rushwa.
  Pombe mwisho kaunta, mtaani ni Lowassa

  James Mbatia:
  Sauti ya umma ni sauti ya Mungu, Mungu akiamua kitu inakuwa. Naanza na hili kwasababu mm ni mjumbe wa kamati ya bajeti ya bunge, najua mateso wanayopata polisi, najua Arusha damu za watu zimemwagika kwa ubabe wa jeshi la polisi.
  Polisi leo wanadiriki kumkaribisha Rais nyumbani kwake kwa mabomu. Namwambia Kikwete nchi hii siyo ya utawala wa kijeshi. Duniani huwezi kutumia nguvu ya dola kutawala raia.
  CCM wamelifikisha deni la taifa ambalo kila mtanzania anadaiwa laki nane na 55,000.
  Namtahadharisha Mkuu wa polisi na rpc wa Arusha nawatahadharisha kuwa wao ndiyo wanaohatarisha amani ya nchi yetu, sasa tumechoka. Polisi constebo mshahara wako haufiki hata laki tano, unatumwa na mtu anayelipwa mil 3 na shangingi una akili kweli wewe?
  Polisi wamekuwa kama panya mama sharubu baba sharubu na mtoto sharubu, kila moja lwake.
  Tanzania bila ccm inawezekana


  Godbless Lema:
  Nasikitika Rais wetu amepokelewa na mabomu, vijana wamezuiwa.
  Wanachokifanya hivi sasa ni kutengeneza mazingira ya kuiba kura kutufundisha uwoga.

  Nampa taarifa IGP kuwa kama wamezoea kuua sisi tumezoea kuwa maiti.

  Dhambi mbaya kuliko zote duniani ni uwoga.

  Polisi wanamzuia Rais wetu asishiriki msiba wa rafiki yake kwa hofu tu akienda atamfunika kikwete.

  Namuahidi Rais Lowassa kuwa kura yake Haitaibiwa.

  Watu wakiamini kuwa hatuwezi kushinda kwa njia ya demokrasia, watatafuta mbinu nyingine kushinda.

  Usalama mwambieni Kikwete yeye sasa ni rais, lkn hii nchi siyo ya mama yake wala ya baba yake
   

  Attached Files:

 2. nkulikwa

  nkulikwa JF-Expert Member

  #1301
  Aug 16, 2015
  Joined: Jul 21, 2015
  Messages: 723
  Likes Received: 794
  Trophy Points: 180
  Safi sana
   
 3. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #1302
  Aug 16, 2015
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,100
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  Safi hiyoooo
   
 4. Chumchang Changchum

  Chumchang Changchum JF-Expert Member

  #1303
  Aug 16, 2015
  Joined: Nov 1, 2013
  Messages: 2,701
  Likes Received: 925
  Trophy Points: 280
  Mimi sio Team Lowasa lkn kwa hili mbona jambo la kawaida kwa Mwafrica kutambikiwa aidha akiwa nyumbani kwao au hata ugenini....
   
 5. M

  Mssassou JF-Expert Member

  #1304
  Aug 16, 2015
  Joined: Jun 17, 2015
  Messages: 1,540
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Lowassa ni mwiba kwa kila mwana CCM
   
 6. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #1305
  Aug 16, 2015
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 23,866
  Likes Received: 20,218
  Trophy Points: 280
  Mnamnadi mda gani Magufuli?
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1306
  Aug 16, 2015
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 8,374
  Likes Received: 2,418
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1307
  Aug 16, 2015
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 8,374
  Likes Received: 2,418
  Trophy Points: 280
  Tofauti ya hiyo ya Lowassa na hii chini ya JK ni nini?

  [​IMG]
   
 9. n

  nkongu ndasu JF-Expert Member

  #1308
  Aug 16, 2015
  Joined: Jan 19, 2013
  Messages: 22,520
  Likes Received: 3,764
  Trophy Points: 280
  kwa hili mtoa mada umejishushia heshima...
   
 10. N

  Njema kabisa JF-Expert Member

  #1309
  Aug 16, 2015
  Joined: May 25, 2015
  Messages: 702
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mkuu wanashindwa kuelewa huu si wakati wa hila kabisa..ndo ule msemo kunya anye kuku akinya bata kaharisha!!
   
 11. MAFUNGUO KUFULI

  MAFUNGUO KUFULI Senior Member

  #1310
  Aug 16, 2015
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 138
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wamasai hawana matambiko,bali huo ni utaratibu wa kumpa cheo kikubwa cha kijamii juu ya laigwnani wote wa tanzania.
   
 12. mkorinto

  mkorinto JF-Expert Member

  #1311
  Aug 16, 2015
  Joined: Jun 11, 2014
  Messages: 8,109
  Likes Received: 4,538
  Trophy Points: 280
  Umechanganyikiwa mpaka umeamua kugoma kufikiri.

  Hivi.kakodisha magari mangapi kwa shilingi ngapi ili ajaze watu wote hapo!!!???????
   
 13. Chademakwanza

  Chademakwanza JF-Expert Member

  #1312
  Aug 16, 2015
  Joined: Jun 11, 2014
  Messages: 6,350
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Jana Arusha ilisimama
   
 14. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #1313
  Aug 16, 2015
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 3,072
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Chadema na viongoz wake napinga maneno yenu ya kejeli na matusi kwa Rais wa jamuhur ya muungano wa Tz na Rais wa mapinduz Zanzibar. Huna chakusema ktk sera zako kaa kimya ikumbukwe wao ni viongoz na kama kunajambo walienda kinyume na taratibu jamuhuri yenyewe itaamua sawa sawa na sheria zetu. Tuwaache viongoz hawa wamalize kwa amani maana watabaki kuwa viongoz nakulindwa mpaka mauti usijesema ukujuwa. Asante
   
 15. Simolunda

  Simolunda JF-Expert Member

  #1314
  Aug 16, 2015
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 452
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wakumbushe tu ikulu imewachanganya
   
 16. H

  Haika JF-Expert Member

  #1315
  Aug 16, 2015
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,319
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kejeli ni jadi ya siasa ya Tanzania. Ukiwa upande wa kukejeli inafurahisha sana ila ukiwa upande wa kukejeliwa huuma sana.

  Ila ikiweza kubadilika itakuwa poa sana. Tukiweza kulist statements za kejeli from both sides itasaidia. Mradi uwe fair.
   
 17. maramia

  maramia JF-Expert Member

  #1316
  Aug 16, 2015
  Joined: Jul 17, 2015
  Messages: 1,915
  Likes Received: 1,092
  Trophy Points: 280
  Ukitaka Rais asisemwe majukwaani mwambie naye akiwa ikulu kwenye ofisi ya umma inayobeba nembo ya utaifa wa watanzania wote asifanye vitendo vya kibaguzi vya kumpigia kampeni mgombea wa chama chake. Kama anayafanya kama m/kiti wa chama chake basi na wapinzani watamsema kama Rais wa chama chake
   
 18. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #1317
  Aug 16, 2015
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,598
  Trophy Points: 280
  Ametuita wapinzania MABUA,sasa nenda kamwambie nyumba yake inaungua moto,kosa ni yale mabua matano aliyowasha mwanae akichoma Mchwa,halafu mwambia Nape Oil Chafu ni dawa ya Mchwa....

  Akitaka kuheshimiwa aheshimu wenzake.............
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #1318
  Aug 16, 2015
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,140
  Likes Received: 22,410
  Trophy Points: 280
  Chadomo hawana sera kabisa, sera yao ni maji taka.
   
 20. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #1319
  Aug 16, 2015
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,837
  Likes Received: 3,643
  Trophy Points: 280
  Endelezeni ushindani wenu eti kisa kafanya acha na mie nifanye ...usije pasuka msamba
   
 21. fundi25

  fundi25 JF-Expert Member

  #1320
  Aug 16, 2015
  Joined: Apr 16, 2013
  Messages: 5,839
  Likes Received: 2,836
  Trophy Points: 280
  Mama sikuhizi unamaneno machache kweli yakujiliwaza!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...