Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA | Page 65 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mussolin5, Aug 15, 2015.

 1. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 17,578
  Likes Received: 61,877
  Trophy Points: 280
  Habari Wanajamvi,

  Leo ndio ile siku inayosubiriwa kwa hamu hapa Mkoani Arusha, pale ambapo mgombea wa Urais kwa tiketi ya Ukawa Ndugu Edward Lowassa atakapotambulishwa rasmi mkoani hapa.

  Hakika maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100%, Mkutano huu pia utashuhudia maelfu ya wanachama wa ccm mkoani hapa wakirudisha kadi zao na kuhamia rasmi Chadema.

  Makamanda karibuni ili tupeane updates na kujulishana kile kinachoendelea.

  Mkutano Unafanyika viwanja vya Tindigani, Kimandolu.
  cc: Timu mahiri ya wanahabari ya Chadema Chadema kwanza Molemo Tumaini Makene
  =======================================================================================

  Updates:
  Baadhi ya wanachama wamepiga kambi karibia na KIA ili kupata fursa ya kujumuika vizuri hapo baadae.

  Wananchi mamia kwa maelfu wanazidi kushuka toka mjini kwenda KIA hakika hapatoshi, picha zitakuja punde tuu.


  Edward Lowassa kashatua KIA, muda wowote msafara wa kuelekea Kimandolu utaanza.

  Polisi wametanda MTO Nduruma kuzuia magari yenye Bendera za chadema na pikipiki zote zinazolekea KIA...

  View attachment 276596
  Arusha.jpg

  SAM_0009.JPG
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  ============================================================
  Tunaomba radhi Makamanda, kuna tatizo la Network leo hapa Arusha, hivyo inasababisha zoezi la uwekaji picha kuwa mgumu. Tunajitahidi kupambana wakuu.
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]
  Wanafunzi nao wakifuatilia mkutano kupitia madirisha ya shule
  [​IMG]

  View attachment 276986
  Lowassa na mama Lowassa wakifanyiwa matambiko ya Kimasai

  11896027_769560393154937_3304267978777158586_n.png
  Lowassa akihutubia wananchi Arusha.
  ==========================================================================================

  Breaking news from Arusha

  Waliojiunga na CHADEMA:
  Laurence Masha anakabidhiwa kadi na Mbowe
  Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara
  Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha
  Sioi Sumari
  Yona Nko aliyekuwa mkiti ccm mkoa Arusha
  Mgombea ubunge Simanjiro
  Goodluck Sipira katibu wa ccm Arusha anatokea Longido
  Wazee wa kimila wa kimasai nchi nzima
  Wazee wa kimila wa kimeru wote wakiongozwa na Mshili Mkuu.


  Ole Medeye:
  Anaimba kuwa Mwambie Kikwete nimezinduka, ccm sirudi tena.
  Nimejitoa ccm kwa sababu mbili kuu, ya kwanza dhuluma imezidi ndani ya ccm, wanaapa kinafiki kuwa watailinda katiba ya nchi wakati wanaivunga, pili rushwa imekithiri katika taifa hili, nilifikiri kupitia ccm ningeshiriki kupiga vita rushwa, lakini matokeo yake kumbe niliowaamini kupiga vita rushwa ndiyo wanaotoa rushwa.
  Hivyo nimejiondoa ccm ili tuweze kurudisha maadili ya nchi.


  Mzee Mtei:
  Ninaambiwa kuwa muasisi wa hiki chama, roho yangu inadunda, nikiona umati huu na jinsi vyama hivi vimeungana nasikia furaha sana. Nashukuru kutuunga mkono, nawatakia kila la kheri katika safari hii ya ukombozi.
  Ninashukuru sasa kwakuwa chama nilichokiasisi kimempata mtu wa kutupeleka ikulu


  M/kiti wa ccm mkoa wa shinyanga Mgeja:
  Nataka niseme maneno machache,
  Kwanza juzi mpaka saa nne na dk 59 nilikuwa mwenyekiti wa ccm, saa tano na dk nikajitoa ccm, baada ya kugundua ndani ya ccm hakuna hakuna haki, nami nikaona nijiunge na chadema chama chenye haki.
  Jana mmemsikia vuvuzela ikipiga kelele kuwa tunamfuata Lowassa, ningekuwa namfuata Lowassa ningeenda Monduli nyumbani kwake.
  Nashangaa vuvuzela Nape eti nimehama chama kisa mtoto wangu ameangushwa ubunge, nataka nimwambie Nape kuwa nina uzefu wa kushindwa, nampa Salamu kuwa tutakutana Mtama.
  Nimepigiwa simu zaidi ya 800 zote zinanipongeza, simu sita tu zilikuwa zinanisikitia.
  Niseme tu nyumba ya ccm inaungua unasubiri nini kuaga?
  Nataka niwaambie Nape na wenye akili kama ya Nape kuwa waeleze wale vigogo wanaojihusisha na ujangili(Kinana) Waeleze fedha za escrow ziko wapi, ccm ni kichaka cha waizi, ccm waeleze kwanini shilingi inashuka, ccm mwulizeni Kikwete unatuachaje? Ataacha umaskini, chuki, husda na rushwa.
  Pombe mwisho kaunta, mtaani ni Lowassa

  James Mbatia:
  Sauti ya umma ni sauti ya Mungu, Mungu akiamua kitu inakuwa. Naanza na hili kwasababu mm ni mjumbe wa kamati ya bajeti ya bunge, najua mateso wanayopata polisi, najua Arusha damu za watu zimemwagika kwa ubabe wa jeshi la polisi.
  Polisi leo wanadiriki kumkaribisha Rais nyumbani kwake kwa mabomu. Namwambia Kikwete nchi hii siyo ya utawala wa kijeshi. Duniani huwezi kutumia nguvu ya dola kutawala raia.
  CCM wamelifikisha deni la taifa ambalo kila mtanzania anadaiwa laki nane na 55,000.
  Namtahadharisha Mkuu wa polisi na rpc wa Arusha nawatahadharisha kuwa wao ndiyo wanaohatarisha amani ya nchi yetu, sasa tumechoka. Polisi constebo mshahara wako haufiki hata laki tano, unatumwa na mtu anayelipwa mil 3 na shangingi una akili kweli wewe?
  Polisi wamekuwa kama panya mama sharubu baba sharubu na mtoto sharubu, kila moja lwake.
  Tanzania bila ccm inawezekana


  Godbless Lema:
  Nasikitika Rais wetu amepokelewa na mabomu, vijana wamezuiwa.
  Wanachokifanya hivi sasa ni kutengeneza mazingira ya kuiba kura kutufundisha uwoga.

  Nampa taarifa IGP kuwa kama wamezoea kuua sisi tumezoea kuwa maiti.

  Dhambi mbaya kuliko zote duniani ni uwoga.

  Polisi wanamzuia Rais wetu asishiriki msiba wa rafiki yake kwa hofu tu akienda atamfunika kikwete.

  Namuahidi Rais Lowassa kuwa kura yake Haitaibiwa.

  Watu wakiamini kuwa hatuwezi kushinda kwa njia ya demokrasia, watatafuta mbinu nyingine kushinda.

  Usalama mwambieni Kikwete yeye sasa ni rais, lkn hii nchi siyo ya mama yake wala ya baba yake
   

  Attached Files:

 2. yanga bwana

  yanga bwana JF-Expert Member

  #1281
  Aug 16, 2015
  Joined: Aug 14, 2015
  Messages: 300
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu atasikia kilio cha Watanzania Wanyonge kwa miaka 50 ya CCM Mkombozi Wa Wanyonge ni LOWASSA .Semeni ngonjela zetu kina Nape mtalala mafuriko no makubwa
   
 3. yanga bwana

  yanga bwana JF-Expert Member

  #1282
  Aug 16, 2015
  Joined: Aug 14, 2015
  Messages: 300
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu safari hii in kukata kiganja
   
 4. yanga bwana

  yanga bwana JF-Expert Member

  #1283
  Aug 16, 2015
  Joined: Aug 14, 2015
  Messages: 300
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani eti MTU anawabeza watanzania umati huo in BALAA
   
 5. G

  Getstart JF-Expert Member

  #1284
  Aug 16, 2015
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 6,092
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280
  Tuwapongeze CCM kwani sasa hatutasikiatena ufisadi, na wale wotewaliobaki wakiwa na tuhuma hizo wametakasika!
   
 6. m

  mkalikali JF-Expert Member

  #1285
  Aug 16, 2015
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hongeren bhana.. hivi chenge, jeikei, tibaijuka nao washaondoka eeh?
   
 7. t

  tufe JF-Expert Member

  #1286
  Aug 16, 2015
  Joined: Apr 24, 2015
  Messages: 750
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inaonekana umeshakata Tamaa. Sasa jiandae kupata maendeleo ya kweli chini ya seriali ya UKAWA.
   
 8. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #1287
  Aug 16, 2015
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,371
  Likes Received: 4,004
  Trophy Points: 280
  Jk kweli kituko, hivi Masha si alikuwa waziri kwenye serikali yake? Ridhiwan si alikuwa kwenye kampuni yake????? mahoka!
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #1288
  Aug 16, 2015
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,411
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  DHAIFU took wananchi for garanted na kukifanya ccm chama cha watu wa Msoga; sasa ndio anazinduka na kugundua kuwa wenyewe wanataka nchi yao hivyo muda si mrefu yeye ndiye atakayeisoma namba!!
   
 10. mzee wa liver

  mzee wa liver JF-Expert Member

  #1289
  Aug 16, 2015
  Joined: Dec 14, 2014
  Messages: 62,843
  Likes Received: 341,952
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wana JF,

  jana nilikuwa nafuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka kiwanja cha tindigani kimandolo arusha ambapo mgombea urais na mgombea mwenza wa UKAWA wikitafuta wadhamini kwa taratibu za NEC lakini kuna matukio ambayo hata aliposimama mwenyekiti wa taifa CHADEMA mh Mbowe alilisema kwa mujibu wa taratibu na kanuni za uchaguzi.

  Embu tuweke ushabiki wetu pembeni na tusije kumuharibia mgombea wetu kwa kuvunja kanuni za uchaguzi kwa kumuita mh lowassa RAIS wakati bado ni mgombea.

  Jamani magamba wamechanganyikiwa watatumia kila kuhakikisha UKAWA hawashindi tuwe makini kwenye kila eneo wasije pata kisingizio cha kumkata mgombea wetu.

  Nawaomba wana UKAWA kwa siku hizi sabini tuendelee kumwita mgombea urais mh lowassa na mgombea mwenza babu duni ole laizer
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1290
  Aug 16, 2015
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,177
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Ahsanteni makamanda Wa Arusha Kwa ushirikiano Wa Jana.
   
 12. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #1291
  Aug 16, 2015
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Huo ushauri wako hawawezi kuufuata.
   
 13. ngajapo

  ngajapo JF-Expert Member

  #1292
  Aug 16, 2015
  Joined: Jun 3, 2012
  Messages: 500
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  sio tatizo kuitwa raisi (kuna raisi wa TFF, chama cha ngumi nk.......)
   
 14. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #1293
  Aug 16, 2015
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,100
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 280

  Si ndie Rais wa Kaskazini?
   
 15. M

  Malata Junior JF-Expert Member

  #1294
  Aug 16, 2015
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,874
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Bila kusahau Rais wa Manzese na Rais wa wasafi,teh teh!
   
 16. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #1295
  Aug 16, 2015
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,837
  Likes Received: 3,643
  Trophy Points: 280
  Wamezoea kuona marais wa Tff sasa bado wanahisi anayetafutwa ni wa Tff ..bora uwaambie wachunge ndimi zao na mbatia pia aka sivyo yakiwakuta wasiseme bao la mkono
   
 17. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #1296
  Aug 16, 2015
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,100
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 280
  Clock tower Arusha, wewe waijua clock tower ya nkurumah tu?
   
 18. M

  Mwera pekee New Member

  #1297
  Aug 16, 2015
  Joined: Aug 14, 2015
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbowe alishatoa hiyo tahadhari jana,kuwa kumwita Lowassa rais ni kufungua milango ya pingamizi.
   
 19. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #1298
  Aug 16, 2015
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,659
  Likes Received: 14,687
  Trophy Points: 280
  Rais wa mapedeshee!

  Kuna laigwanani feki naye alimwita rais!NEC ikemee la sivyo ccm wakianza tuwe kimya
   
 20. Kansigo

  Kansigo JF-Expert Member

  #1299
  Aug 16, 2015
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,664
  Likes Received: 1,471
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]

  [FONT=&quot]Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakifanyiwa matambiko na Wazee (Malaigwanani) ya Kimasai, wakati wa Mkutano wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.
  LO1.jpg

  [/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hapa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akipokea rungu kutoka kwa Mzee Nyinyajwangwa Laiza, mara baada ya Ibada ya kimila na Wazee (Malaigwanani) ya Kimasai, wakati wa Mkutano wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.
  LO2.jpg
  [/FONT]  [/TABLE]
   
 21. M

  MICHAEL JOSEPH93 Senior Member

  #1300
  Aug 16, 2015
  Joined: Aug 1, 2015
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  African culture
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...