Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mussolin5, Aug 15, 2015.

 1. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 17,578
  Likes Received: 61,877
  Trophy Points: 280
  Habari Wanajamvi,

  Leo ndio ile siku inayosubiriwa kwa hamu hapa Mkoani Arusha, pale ambapo mgombea wa Urais kwa tiketi ya Ukawa Ndugu Edward Lowassa atakapotambulishwa rasmi mkoani hapa.

  Hakika maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100%, Mkutano huu pia utashuhudia maelfu ya wanachama wa ccm mkoani hapa wakirudisha kadi zao na kuhamia rasmi Chadema.

  Makamanda karibuni ili tupeane updates na kujulishana kile kinachoendelea.

  Mkutano Unafanyika viwanja vya Tindigani, Kimandolu.
  cc: Timu mahiri ya wanahabari ya Chadema Chadema kwanza Molemo Tumaini Makene
  =======================================================================================

  Updates:
  Baadhi ya wanachama wamepiga kambi karibia na KIA ili kupata fursa ya kujumuika vizuri hapo baadae.

  Wananchi mamia kwa maelfu wanazidi kushuka toka mjini kwenda KIA hakika hapatoshi, picha zitakuja punde tuu.


  Edward Lowassa kashatua KIA, muda wowote msafara wa kuelekea Kimandolu utaanza.

  Polisi wametanda MTO Nduruma kuzuia magari yenye Bendera za chadema na pikipiki zote zinazolekea KIA...

  View attachment 276596
  Arusha.jpg

  SAM_0009.JPG
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  ============================================================
  Tunaomba radhi Makamanda, kuna tatizo la Network leo hapa Arusha, hivyo inasababisha zoezi la uwekaji picha kuwa mgumu. Tunajitahidi kupambana wakuu.
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]
  Wanafunzi nao wakifuatilia mkutano kupitia madirisha ya shule
  [​IMG]

  View attachment 276986
  Lowassa na mama Lowassa wakifanyiwa matambiko ya Kimasai

  11896027_769560393154937_3304267978777158586_n.png
  Lowassa akihutubia wananchi Arusha.
  ==========================================================================================

  Breaking news from Arusha

  Waliojiunga na CHADEMA:
  Laurence Masha anakabidhiwa kadi na Mbowe
  Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara
  Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha
  Sioi Sumari
  Yona Nko aliyekuwa mkiti ccm mkoa Arusha
  Mgombea ubunge Simanjiro
  Goodluck Sipira katibu wa ccm Arusha anatokea Longido
  Wazee wa kimila wa kimasai nchi nzima
  Wazee wa kimila wa kimeru wote wakiongozwa na Mshili Mkuu.


  Ole Medeye:
  Anaimba kuwa Mwambie Kikwete nimezinduka, ccm sirudi tena.
  Nimejitoa ccm kwa sababu mbili kuu, ya kwanza dhuluma imezidi ndani ya ccm, wanaapa kinafiki kuwa watailinda katiba ya nchi wakati wanaivunga, pili rushwa imekithiri katika taifa hili, nilifikiri kupitia ccm ningeshiriki kupiga vita rushwa, lakini matokeo yake kumbe niliowaamini kupiga vita rushwa ndiyo wanaotoa rushwa.
  Hivyo nimejiondoa ccm ili tuweze kurudisha maadili ya nchi.


  Mzee Mtei:
  Ninaambiwa kuwa muasisi wa hiki chama, roho yangu inadunda, nikiona umati huu na jinsi vyama hivi vimeungana nasikia furaha sana. Nashukuru kutuunga mkono, nawatakia kila la kheri katika safari hii ya ukombozi.
  Ninashukuru sasa kwakuwa chama nilichokiasisi kimempata mtu wa kutupeleka ikulu


  M/kiti wa ccm mkoa wa shinyanga Mgeja:
  Nataka niseme maneno machache,
  Kwanza juzi mpaka saa nne na dk 59 nilikuwa mwenyekiti wa ccm, saa tano na dk nikajitoa ccm, baada ya kugundua ndani ya ccm hakuna hakuna haki, nami nikaona nijiunge na chadema chama chenye haki.
  Jana mmemsikia vuvuzela ikipiga kelele kuwa tunamfuata Lowassa, ningekuwa namfuata Lowassa ningeenda Monduli nyumbani kwake.
  Nashangaa vuvuzela Nape eti nimehama chama kisa mtoto wangu ameangushwa ubunge, nataka nimwambie Nape kuwa nina uzefu wa kushindwa, nampa Salamu kuwa tutakutana Mtama.
  Nimepigiwa simu zaidi ya 800 zote zinanipongeza, simu sita tu zilikuwa zinanisikitia.
  Niseme tu nyumba ya ccm inaungua unasubiri nini kuaga?
  Nataka niwaambie Nape na wenye akili kama ya Nape kuwa waeleze wale vigogo wanaojihusisha na ujangili(Kinana) Waeleze fedha za escrow ziko wapi, ccm ni kichaka cha waizi, ccm waeleze kwanini shilingi inashuka, ccm mwulizeni Kikwete unatuachaje? Ataacha umaskini, chuki, husda na rushwa.
  Pombe mwisho kaunta, mtaani ni Lowassa

  James Mbatia:
  Sauti ya umma ni sauti ya Mungu, Mungu akiamua kitu inakuwa. Naanza na hili kwasababu mm ni mjumbe wa kamati ya bajeti ya bunge, najua mateso wanayopata polisi, najua Arusha damu za watu zimemwagika kwa ubabe wa jeshi la polisi.
  Polisi leo wanadiriki kumkaribisha Rais nyumbani kwake kwa mabomu. Namwambia Kikwete nchi hii siyo ya utawala wa kijeshi. Duniani huwezi kutumia nguvu ya dola kutawala raia.
  CCM wamelifikisha deni la taifa ambalo kila mtanzania anadaiwa laki nane na 55,000.
  Namtahadharisha Mkuu wa polisi na rpc wa Arusha nawatahadharisha kuwa wao ndiyo wanaohatarisha amani ya nchi yetu, sasa tumechoka. Polisi constebo mshahara wako haufiki hata laki tano, unatumwa na mtu anayelipwa mil 3 na shangingi una akili kweli wewe?
  Polisi wamekuwa kama panya mama sharubu baba sharubu na mtoto sharubu, kila moja lwake.
  Tanzania bila ccm inawezekana


  Godbless Lema:
  Nasikitika Rais wetu amepokelewa na mabomu, vijana wamezuiwa.
  Wanachokifanya hivi sasa ni kutengeneza mazingira ya kuiba kura kutufundisha uwoga.

  Nampa taarifa IGP kuwa kama wamezoea kuua sisi tumezoea kuwa maiti.

  Dhambi mbaya kuliko zote duniani ni uwoga.

  Polisi wanamzuia Rais wetu asishiriki msiba wa rafiki yake kwa hofu tu akienda atamfunika kikwete.

  Namuahidi Rais Lowassa kuwa kura yake Haitaibiwa.

  Watu wakiamini kuwa hatuwezi kushinda kwa njia ya demokrasia, watatafuta mbinu nyingine kushinda.

  Usalama mwambieni Kikwete yeye sasa ni rais, lkn hii nchi siyo ya mama yake wala ya baba yake
   

  Attached Files:

 2. KIMBWANGAI

  KIMBWANGAI Member

  #2
  Aug 15, 2015
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kambi saivi
  duuuh. me ntaenda asubuhi tu.
   
 3. steven mdoe

  steven mdoe Member

  #3
  Aug 15, 2015
  Joined: Jun 27, 2015
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja mkuu tunasubiri zaid hapa
   
 4. L

  Lotakajaki Member

  #4
  Aug 15, 2015
  Joined: Aug 8, 2013
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pamoja sana .........ukawa juu.........mwaka huu ....tanzania lazima iwe mpya....!!!!!!!!!
   
 5. T

  Tanzania Njema Yaja JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2015
  Joined: Jul 15, 2015
  Messages: 3,059
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  Picha kwa sana mkuu na yanayo jiri maana tv zimeisha nunuliwa... JF ndo kila kitu...
   
 6. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 17,578
  Likes Received: 61,877
  Trophy Points: 280


  watu wanahisi watazuiwa na polisi, hivyo wameamua kuwahi mapema.
   
 7. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 17,578
  Likes Received: 61,877
  Trophy Points: 280


  Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu. Ukawa Magogoni jioni ya Oktoba 25
   
 8. Victor wa happy

  Victor wa happy JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 24, 2013
  Messages: 9,444
  Likes Received: 6,775
  Trophy Points: 280
  hahaha hatupumui.n.kesho wangepumzka mbeya tu
  maana loo
   
 9. m

  mangola JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2015
  Joined: Aug 27, 2014
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hahahahaha, hizi sasa sifa.
   
 10. Victor wa happy

  Victor wa happy JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 24, 2013
  Messages: 9,444
  Likes Received: 6,775
  Trophy Points: 280
  mkuu iyo avater ndo mfasim musolin mwenyewe?
   
 11. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2015
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,297
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hizi sasa sifa!
   
 12. KING MAZENGO

  KING MAZENGO JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2015
  Joined: Aug 5, 2015
  Messages: 755
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hakika vijana wa chadema na ukawa mnanifurahisha...khahahaa...!
   
 13. k

  kibenya JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2015
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  hii sasa balaa kweli hakuna kulala
   
 14. Chademakwanza

  Chademakwanza JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2015
  Joined: Jun 11, 2014
  Messages: 6,350
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Jopo la Wanahabari wa Chadema ndio tumeingia mda huu Arusha Tutariport moja kwa moja tukio hili
   
 15. Gogo la choo

  Gogo la choo JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2015
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 714
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu hawa vijana aisee..ile baridi ya pale KIA na vijana wameweka kambi!!?mwaka huu tutashuhudia mengi sana Mungu atupe uzima tu tuonane Oct 25
   
 16. s

  sensor JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2015
  Joined: Jan 27, 2015
  Messages: 2,472
  Likes Received: 837
  Trophy Points: 280
  Unaogopa baridi ya KIA ? Hujaonaga baridi nini na watu wanasonga
   
 17. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2015
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hapajakucha bado..
   
 18. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Teh teh teh alfajiri hii mmeshaanza tayari! Umoja ni nguvu si mchezo . Hiyo ni statement ya wananchi loud na clear kwamba wamechoka, sasa ni wazi kwamba mwenye tija ni yule anaye saidia kuondoka kwa ccm madarakani.
   
 19. MAWAZO UJENZI

  MAWAZO UJENZI JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2015
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Du hatari sana,mwaka huu kuna mengi ya kujifunza katika chaguzi zijazo tuombe uzima tufike 0kitoba ishirini na tano
   
 20. Querido

  Querido Senior Member

  #20
  Aug 15, 2015
  Joined: May 12, 2014
  Messages: 119
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  naanza sfr kwenda kwa lowassa mapema hii
  kamanda utakae hisi njaa na kiu nina mihogo ba maji ..

  tusonge mbele comrades
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...