Updates: Kukamatwa kwa Wanachama wa CHADEMA Kanisani Mwanza

Wakuu, nimepata hii updates ila kwa kweli hata kama Polisi wetu wanatumwa basi at least watumie hata akili. Why wanalazimisha kujenga chuki isiyomithilika kwenye jamii?? Was it necessary?

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi na baadhi ya Askari Wanyama pori wanaozea gerezani kwa kufanya mauwaji Kanisani. anyways wacha niwape updates


Updates


Makamanda, habari za muda huu. Mpaka sasa hivi tunaendelea kushughulikia sakata la kukamatwa kwa viongozi na wanachama walipokuwa kwenye misa jana Kawekamo.

Walioko lock up ni Katibu wa kanda ya Victoria, Mwenyekiti wa Ilemela, Katibu wa Nyamagana na wanachama wengine jumla yao ni 20.

Baada ya kumuona OCD asubuhi ya leo, alitwambia kuwa wanatuhumiwa kwa kufanya vurugu kanisani na kwamba alipigiwa simu na viongozi wa kanisa.

Ilibidi tukauone uongozi wa kanisa Katoliki jimbo la Mwanza, tumeonana na msaidizi wa baba Askofu na akatuwezesha kuongea na askofu Mkuu Renatus Kwande.

Askofu Nkwande amesikitishwa sana na uongo wa jeshi la polisi na kuthibitisha kwamba hakukuwa na vurugu yoyote kwenye misa hiyo. Na alipokea matoleo ya Wana Chadema na kusali pamoja nao. Akawakaribisha wale chakula.

Wakati wanakwenda kunawa polisi wakavamia eneo hilo na kuanza kukamata kila aliyekuwa na sare za Chadema.

Awali asubuhi, walikwishakamata wanachama watano akiwemo mama Pambalu ambaye naye alikuwa anaigia kanisani.

Baba askofu katupa msaidizi wake tukaenda naye Kirumba na ameongea na OCD, sasa ocd kageuza kwa si kanisa lilimpigia simu bali ni waumini wawili mmojawapo anaitwa Gerlad Joseph. Msaidizi wa Askofu kawasiliana naye na sasa Askofu amemtuma katibu wake Padre Nyanda, tunaendelea kumsubiri hapa kirumba.

Msimamo wetu ni:
1. Wawaachie wote bila masharti ya dhamana.

2. Au baba Askofu akawadhamini waumini wake.

Wanzagi
Wale waliokuwa wakishangilia salamu mpya kwa jina la JMT, sasa ndiyo wanapaswa kutambua ya kwamba ilikuwa ni ya kishetani ambayo ipo kinyume na Jina lile kuu kuliko majina yote mbinguni na duniani.
 
Huo utaratibu umeanza lini?
Mnaombewa nini?
Maombi yenu hadi yafanyikie kanisani, sehemu ya ibada?

Siku mkijua mnachokitaka, kwanjia gani, kwa wakati gani na kwakiongozi gani mtakuwa wapinzani sahii lakni sahivi tunawaona kama upepo tu.
Umesahau mwendazake alikuwa anafanya nini kanisani?
 
Kwa akili zangu za kubumba , Kuna kitu kinatengenezwa ili mtu achafuke haswa na anuke kila Aina ya uozo na harufu asifae Tena kwa kazi bali arudi kwao kuogelea ama kwa maksudi kabisa anayafanya yeye ili atimue watu kwa kupata kusingizio.

Sitaki uniamini Ila ni akili zangu zinanituma hivyo sijui ni uchovu wa safari hata sielewi 😢😢😢😢😢
 
Umuhimu wa Polisi ni Mkubwa sana Duniani. Lkn nitamlaani Mtoto wangu akijiunga na Polisi Tanzania.
 
uliwai kumuona kavaa kijani kanisani? Leta evidence
Lakini pia yeye alikuwa na nyazifa gani?

Kijana haya unayoyaona yanatokea ninmatokeo ya ujinga na umaskini.
 
Ujinga mwingi sn Tanzania. Hivi mpaka ya Taleban yatokee ndo upuuzi huu utaisha?
 
Mbowe sio gaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Amen

IMG_20210812_123915.jpg


IMG_20210815_123259.jpg
 
Back
Top Bottom