Updates from Mbeya-Ziara ya Waziri mkuu Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Updates from Mbeya-Ziara ya Waziri mkuu Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by G.MWAKASEGE, Oct 17, 2007.

 1. G.MWAKASEGE

  G.MWAKASEGE Senior Member

  #1
  Oct 17, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na Christopher Nyenyembe  JARIBIO la Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kutaka kumsafisha na kumkingia kifua Waziri wa Nshati na Madini, Nazir Karamagi, kuhusu mkataba wa Buzwagi liliingia dosari jana baada ya wakazi wa Mbeya kupinga kwa sauti za juu utetezi wake kuhusu mkataba huo.
  Hali hiyo ilitokea baada ya mwananchi mmoja kumuuliza Lowassa sababu zinazomfanya Karamagi asijiuzulu wakati akikabiliwa na tuhuma za waziwazi za kusaini mkataba wenye utata wa madini huko London, Uingereza.

  Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Lowassa alianza kwa kuwasifu wakazi wa Mbeya kwa uelewa wao wa mambo na akasema Karamagi alikuwa hajafanya kosa lolote la kimaadili au kisheria kwa kusaini mkataba huo.

  Hata baada ya wananchi kuanza kuguna wakionyesha dhahiri kutokubaliana na majibu hayo, Waziri Mkuu alisema hoja za wapinzani kupinga mkataba huo kusainiwa London Uingereza hazijitoshelezi.

  Aidha, aliwataka wananchi wa Mbeya kutambua kuwa mkataba wa Buzwagi hauna matatizo yoyote kisheria kwani uliandaliwa na kuboreshwa kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete.

  “Mkataba wa Buzwagi ni mzuri, isipokuwa umepigwa maneno mengi ya kisiasa na sijaona kosa la Buzwagi hata kama ungesainiwa Sumbawanga au Kamachumu, bado ungekuwa vile vile. Kwa nini hili hamtaki kuliona?” alihoji Lowassa.

  Lowassa alikutana na zahama hiyo ya kisiasa katika uwanja ule ule wa Shule ya Msingi ya Ruanda Nzovwe, ambao mawaziri na makada kadhaa wa CCM walikutwa na tukio la kuzomewa siku chache tu zilizopita.

  Wakati hilo likitokea, hali ilikuwa tete kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, aliyejikuta akikabiliwa na wakati mgumu kujibu maswali ya wananchi mbele ya Waziri Mkuu.

  Kikubwa kilichomtia matatizoni Mwakipesile kilikuwa ni utata katika majibu aliyokuwa akiyatoa, hatua ambayo ilimfanya awaombe wananchi waache kumsulubu mbele ya kiongozi wake.

  Swali lililoonekana mwiba kwa mkuu huyo wa mkoa ni juu ya mabilioni ya Rais Kikwete, yaliyogawiwa kwa wananchi, ambao wengi hazijawafikia, na kinyume chake akijikuta akitoa mchanganuo tofauti wa fedha zilizokopeshwa kutoka benki mbili, ya CRDB na NMB, tofauti na sh bilioni moja zilizoahidiwa.

  Huku watu wakiguna, mkuu huyo wa mkoa alisema wazi kuwa mkoa huo umepokea kiasi cha sh milioni 500 tu za Rais Kikwete na si bilioni moja, na kwamba mkoa huo umeweza kukopeshwa kiasi cha sh bilioni 4.7 kwenye SACCOS na mtu mmoja mmoja kutoka kwenye benki hizo.

  “Mimi ndiye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Nawaomba wananchi msinisulubu sana mbele ya Waziri Mkuu, najua kuwa mahitaji ya mbolea ya ruzuku kwa mkoa wetu ni makubwa kuliko kiasi tulichotengewa, na mkoa wetu unaoongoza kwa kukopeshwa benki kuliko mikoa yote Tanzania,” alisema Mwakipesile.

  Kauli hiyo ilisababisha watu waendelee kuguna zaidi kutokana na utofauti wa maelezo kuhusu mbolea ya ruzuku na bilioni za Kikwete kama ilivyoelezwa awali na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika kuwa mkoa huo umepatiwa mbolea ya ruzuku tani 18,000 kwa mwaka huu, huku mkuu wa mkoa huo akidai kuwa umepokea tani 16,000 tu.

  Katika kujibu hoja na maswali ya wananchi ambao hawakuwa na mwelekeo wowote wa kufurahia majibu hayo na kuendelea kuguna, ulifika wakati ambao waziri mkuu aliwaomba watu wamshangilie kwa majibu yake na yale yaliyotolewa na watendaji wengine wa serikali na kuonekana kundi dogo tu ndilo lililoweza kutii.

  Maeneo mengine yaliyoonekana kero kwa wakazi wa mkoa huo na kuzusha maswali ni umilikaji wa viwanja, bei ya saruji na barabara ya Mbeya hadi Chunya, ambayo kwa kiasi kikubwa kulisababisha Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, aitwe na waziri mkuu ili kutolea maelezo kufuatia madai ya wazi kuwa tenda nyingi za ujenzi zinatolewa kwa makandarasi wa nje.

  Waziri mwingine aliyejikuta akikumbwa na wakati mgumu ni Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi, Ludovick Mwananzila, aliyeulizwa swali na mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Mbeya, aliyehoji upungufu wa walimu, huku wengi wakiwa wamejikita kwenye usimamiaji wa mitihani ya kidato cha nne na kusababisha wengine wakose masomo.

  Akijibu swali la mwanafunzi huyo, Tito Benny, alikubali na kukiri mapungufu hayo kuwa mkoa huo una upungufu wa walimu zaidi ya 476 wanaopaswa kufundisha katika shule mbalimbali za sekondari zilizofunguliwa, huku mahitaji ya walimu wapya ni zaidi ya 7,000 wanaotakiwa kusambazwa kwenye shule zaidi ya 1,090 zilizofunguliwa nchi nzima.

  Akihitimisha kipindi cha maswali na majibu katika mkutano huo, Lowassa aliwaasa wananchi kuwa yule mtu anayeitwa ‘bure’ alikwisha zikwa muda mrefu na matanga yakaanuliwa, akiwataka wananchi waache kukaa vijiweni, wafanye kazi, na hivyo kusababisha watu wengi wanune.
   
 2. Zee la shamba

  Zee la shamba Member

  #2
  Oct 17, 2007
  Joined: Oct 17, 2007
  Messages: 55
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wapinzani walitoa photocopy wakaficha original copy, CCM wanajaribu kutafuta spelling errors kwenye photocopy badala ya original.
  Kazi ipo.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Niko Mnadani hapa Buturi , Jimbo la Rorya sasa na nimepata habari za Magufuli kuwa Musoma mjini Uwanja wa Mukendo nami naelekeo huko kujua yatakayo jiri . Ila CCM kwa kweli wanajuta sana na nadhani ile tabia ya CCM mbele na tanzania na watanzania nyuma itawatoka kama wanaweza kujiuliza na kusoma alama za nyakati .
   
 4. data

  data JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2017
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,775
  Likes Received: 6,540
  Trophy Points: 280
  Duh!! Lowassa ni Don kitambo...
   
 5. Countrywide

  Countrywide JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2017
  Joined: Mar 2, 2015
  Messages: 2,518
  Likes Received: 1,839
  Trophy Points: 280
  duh
   
 6. Heavy Weight

  Heavy Weight JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2017
  Joined: Mar 1, 2014
  Messages: 539
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 80
  Sawa
   
 7. T

  TRUVADA JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2017
  Joined: Jan 6, 2014
  Messages: 4,529
  Likes Received: 1,178
  Trophy Points: 280
  Karamgh aliwahi kwenda kusaini mkatabaa landon kwa kuwa alitaka kurudisha pesa yake ya kampeni na ndo maana alimuaga lowsa tu kwenda london
   
 8. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2017
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,394
  Likes Received: 6,577
  Trophy Points: 280
  siasa siasani ; ningependa sana kujua msimamo wa lowasa kwa sasa kuhusiana na hili! Je, atakana kauli yake mwenyewe kuwa hakukua na kosa lolote katika issue ya buzwagi??
   
 9. data

  data JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2017
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,775
  Likes Received: 6,540
  Trophy Points: 280
  Mbona kashasema hapo......

  Hata ingesainiwa Sumbawanga kusingekuwa na tofauti...Jakaya Kikwete alishaipitisha....

  Rais hapingwi.
  Antachabo.
   
 10. cocochanel

  cocochanel JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2017
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 18,453
  Likes Received: 59,403
  Trophy Points: 280

  Enzi za habari kuwa habari tunasoma kama hatujui mengi na kiundani, tunanyamaza huku tukisubiri threads zingine... hatukuchafua uzi kwa kuandika maajabu au kutunga kama ilivyo siku hizi, ambaoo mtu unasoma unakuta 85% walioandika ni wameandika majanga au niseme sifwuli.
   
 11. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2017
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,138
  Likes Received: 9,022
  Trophy Points: 280
  Inaonekana ulikula sana utumbo wa kuku utotoni mwako hasa wa broiler ukakutoa akili....

  Ukisoma mstari kwa mstari utaona Lowassa akijibu kuwa mkataba ulifuata hatua zote kwa maelekezo ya Rais Kikwete!!
   
 12. data

  data JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2017
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,775
  Likes Received: 6,540
  Trophy Points: 280
  "Tuwaache wazee hawa wapumzikee...wamelifanyia taifa hili meengiii"
   
 13. Zawadi B Lupelo

  Zawadi B Lupelo JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2017
  Joined: Jul 19, 2015
  Messages: 1,865
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Kweli wazee wapumzike kumbe ulisainiwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete
   
 14. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2017
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,394
  Likes Received: 6,577
  Trophy Points: 280
  “Mkataba wa Buzwagi ni mzuri, isipokuwa umepigwa maneno mengi ya kisiasa na sijaona kosa la Buzwagi hata kama ungesainiwa Sumbawanga au Kamachumu, bado ungekuwa vile vile. Kwa nini hili hamtaki kuliona?” alihoji Lowassa.
   
 15. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2017
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,394
  Likes Received: 6,577
  Trophy Points: 280
  Hayo mengine umesema wewe, msome hapa kauli yake mwenyewe;

  “Mkataba wa Buzwagi ni mzuri, isipokuwa umepigwa maneno mengi ya kisiasa na sijaona kosa la Buzwagi hata kama ungesainiwa Sumbawanga au Kamachumu, bado ungekuwa vile vile. Kwa nini hili hamtaki kuliona?” alihoji Lowassa.
   
 16. data

  data JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2017
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,775
  Likes Received: 6,540
  Trophy Points: 280
  Gongo imeshakupofua macho wewe....
   
 17. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2017
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,481
  Likes Received: 2,144
  Trophy Points: 280
  Leo ndo anatetea eti mali zetu wakati alishindwa akiwa na mamlaka!!!!!!
   
Loading...