Chiwaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 5,726
- 3,741
Habari ndgu jamaa na marafiki na hasa hasa wale ndugu zangu mliozaliwa au mliowahi kuishi wilayani Kilosa,iliyopo katika mkoa wa Morogoro. Najua si wote mliozaliwa kilosa mmefanikiwa kuishi, wapo wengi ambao ni wazaliwa wa wilaya hiyo lakini mko mbali na wilaya hiyo.
Hiyo inatokana na sababu kadhaa zikiwemo zile za kujitafutia ridhiki aka maisha. Pamoja na hayo kuna wakati unapenda sana kufahamu nini kinachoendelea huko kilosa, lakini huna njia ya kupata habari za huko.
Kutokana na jambo hilo, nimeona si mbaya kama tutatumia njia hii(thread hii), kwa ajili ya kupashana habari. Tuomba yeyote mwenye taarifa ya aina yoyote ile iwe ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, sherehe,msiba, ajali,majanga yanayohusu wilaya kilosa awe tayari kutufahamisha. Kwa kutumia njia hii wana kilosa wataweza kufahamu kinachoendelea huko wilayani Kilosa.
Kwa kuanzia naomba niwataarifu kuwa Hiza wa Senkubo(Abdallah Dogo) amefariki dunia juzi. Mazishi yake yanategemewa kufanyika mchana huku kilosa. Kifo cha marehemu Hiza kimesababishwa na ajali ya gari iliyotokea maeneo ya bwawani nje kidogo ya mji wa Morogoro. Inallillah wa innallillah rrajun.
Wengingine katika ajali hiyo ni Sultan(mdogo wake na Fadhiri). Yeye inasemekana amevunjika mbavu mbili na amepelekwa hospitali ya Muhimbili kwa matababu zaidi. Wote walikuwa ni watumishi wa Tanzania investment Bank ya jijini DSM