Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,372
Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe na viongozi wenzake 6 walisafirishwa jana usiku kwa gari la wazi kutoka Kilwa hadi Lindi
Magari ya Chama hicho yalifuata nyuma msafara wa Polisi ili kuhakikisha Usalama wa Viongozi wao ambapo walifanikiwa kufikia Kituo cha Polisi Lindi saa 7 usiku
Aidha, Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara (Bwege), aliyeugua jana ghafla wakiwa Kituo cha #Polisi Kilwa na kukimbizwa Hospitali ya Kilwa Masoko, amefikishwa Lindi na Polisi
Hali ya Bwege imetengemaa leo na yupo kituoni hapo pamoja na Zitto na Viongozi wengine huku Mawakili wa ACT wa Lindi na waliotoka Dar wakiwasili Kituo cha Polisi #Lindi ili kushughulikia dhamana
Pia, soma: Lindi: Zitto Kabwe na Sulemani Bungara (Bwege) wakamatwa na Polisi
----UPDATE----
LINDI: ZITTO KABWE NA VIONGOZI WENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na wenzake 7 wameachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja na kutakiwa kuripoti Polisi Lindi Julai 01, 2020
Kwa mujibu wa ACT hakuna masharti mengine ya dhamana kwa viongozi hao waliokamatwa jana Wilayani Kilwa na kusafirishwa hadi Kituo cha Polisi jana usiku
Awali, walikuwa wanashtakiwa kwa kufanya maandamano bila kibali cha Polisi lakini baadaye shtaka likageuzwa na kuwa kutishia uvunjivu wa amani