UPDATE: Zitto, Bwege na wenzake wasafirishwa usiku kutoka Kilwa hadi Lindi. Waachiwa kwa dhamana

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,510
2,000
Huyo bwege mitero tuu haumwi kumbe na zile mbwwmbwe namwonaga nazo kule bungeni ni mweupe hivyo
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,732
2,000
Hahaha kunawatu huwa nawasikia eti wakimkemea shetani tokaaa, shetani hawezi kutoka kwa kukemewa.
Mungu alimfukuza shetani mbinguni akamtupa duniani, eti binadamu bado tunamtafuta shetani aliko. Wakati tuna tenda matendo ya kishetani.
Dawa ya nyoka ni kumponda kichwa siyo kumkimbia.
Ndio maana warundi hawakuomboleza msiba wao eti tukaenda sisi kuomboleza.
 

Gia kubwa

JF-Expert Member
May 28, 2020
474
1,000
mbinu za kibabe kuua upinzani zinavijenga zaidi vyama hivyo badala ya kuvibomoa, kila mtu nchini anasikia matukio hayo ya polisi kuwasumbua wapinzani na kuona wanaonewa na wananchi kuichukia serikali!
watu wa nje pia wanasikia na kuona video za matukio hayo na kuharibu taswira ya nchi na utoaji wao misaada na utalii, watalii wengi wa ulaya na marekani wanachukia nchi zenye ukandamizaji na pia matukio haya wapinzani wanayaandikia funding proposals na kupewa mabilioni kutoka nje kuja kuvuruga juhudi mfano hai ni tshirt alizogawa Zzk mji mzima Kilwa pesa hizo katoa wapi? aulizwe na Takukuru!

hapa ujanja ni kuwaruhusu wapinzani wafanye kwa amani vikao vya ndani na hata kwenye majukwaa ya siasa wasibugudhiwe sheria ya vyama vingi inawapa uhuru huo!

1. cha kufanya ni kuhakikisha wagombea wa ubunge wa upinzani hatari kwa kijani wanakosa form za ubunge kwa kukosa vigezo au wanapewa masharti kila wakileta form zirudishwe wakarekebishe vipengele hadi muda wa kurudisha form upite
2. kesi za uchochezi ziwepo za kumwaga hata wagombea hatari wa upinzani wakose muda wa kampeni wawe wanashinda mahakamani, kesi zao zisiishe kosa moja wapewe kesi kumi na kila wiki wapewe tarehe kurudi mahakamani hadi uchaguzi upite na wengine wapewe kesi za kutakatisha pesa na uchochezi na uhaini na waambiwe sio raia!!
3.kutumia makada mitaani kuhamasisha watu kujiunga na kijani, tshirt na kofia na vitenge na vilemba vigaiwe kwa wingi hali ni ngumu wengine watumie nguo hizo kufanya mtoko! hii ni takrima muhimu! isipuuzwe wapinzani wameanza kuitumia na itawapaisha!
4. kuhakikisha miradi mingi ya maendeleo inakamilika kila mji au wilaya na kuondoa wakandarasi wazembe na kuwashitaki na kuwatupa jela maafisa wanaofisadi miradi
5. Wakurugenzi kutumia magoli ya mkono kama last resort kwa majimbo yote tunayojua wabunge wake ni waropokaji na mawakala wa mabeberu!
6. kuendelea kupiga vichwa vya nyoka kule Dom, wakikaa hosp au mahabusu nchi inatulia miradi inaenda kwa kasi
7. kuunda kamati ya ufundi na bajeti ya kutosha kuhakikisha wale wabunge hatari kumi hatari kwa kijani hawarudi bungeni!

hakuna haja ya mabomu ya machozi siasa ni akili tu, si mchezo unaohitaji hasira, Bia Yetu uko wapi? ushaamka na kuzimua? nakuwakilisha!m
nani anasema nimeharibu uzi?
 

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,378
2,000
Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe na viongozi wenzake 6 walisafirishwa jana usiku kwa gari la wazi kutoka Kilwa hadi Lindi

Magari ya Chama hicho yalifuata nyuma msafara wa Polisi ili kuhakikisha Usalama wa Viongozi wao ambapo walifanikiwa kufikia Kituo cha Polisi Lindi saa 7 usiku

Aidha, Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara (Bwege), aliyeugua jana ghafla wakiwa Kituo cha #Polisi Kilwa na kukimbizwa Hospitali ya Kilwa Masoko, amefikishwa Lindi na Polisi

Hali ya Bwege imetengemaa leo na yupo kituoni hapo pamoja na Zitto na Viongozi wengine huku Mawakili wa ACT wa Lindi na waliotoka Dar wakiwasili Kituo cha Polisi #Lindi ili kushughulikia dhamana

Pia, soma: Lindi: Zitto Kabwe na Sulemani Bungara (Bwege) wakamatwa na Polisi
Kesi uchwara za kubuni hizi tushazizoea.
Watumie ile kasi yao bambikizi kwa wakosoaji wa serikali ijulikanayo kama,
Uhujumu uchumi au
Katakatisha fedha.
 

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,148
2,000
Kosa lililopelekea kukamatwa ni nini?

Kosa kubwa ni uoga wa CCM dhidi ya ACT. Juzi niliandika kuwa CCM ilitumia nguvu kubwa kuisambalatisha CHADEMA. Haikuwa na wakati wa kupoteza na chama chenye mbunge mmoja tu- ACT. Hivyo haikuona tishio toka ACT na hivyo haikuwa na plan wala mbinu ya kukabiliana na ACT.

Leo ACT imewashtukizia pabaya, na bado Pole Pole hajapata mbinu ya kupambana na hiki chama hivyo shughuli zote wameachiwa polisi ambao nao wamepanik.

Uchaguzi mwaka huu si rahisi kama watu wanavyofikiria. Ni mabavu tu yatayomuhakikishia ushindi mgombea wa CCM (sitaji jina kwani sijui kama atakuwa Magu au Membe au mwingine). Kwa sababu mara hii wanachama CCM wamedhamiria kuvunja utamaduni na kufuata katiba ya CCM.
 

Gia kubwa

JF-Expert Member
May 28, 2020
474
1,000
Kosa kubwa ni uoga wa CCM dhidi ya ACT. Juzi niliandika kuwa CCM ilitumia nguvu kubwa kuisambalatisha CHADEMA. Haikuwa na wakati wa kupoteza na chama chenye mbunge mmoja tu- ACT. Hivyo haikuona tishio toka ACT na hivyo haikuwa na plan wala mbinu ya kukabiliana na ACT.

Leo ACT imewashtukizia pabaya, na bado Pole Pole hajapata mbinu ya kupambana na hiki chama hivyo shughuli zote wameachiwa polisi ambao nao wamepanik.

Uchaguzi mwaka huu si rahisi kama watu wanavyofikiria. Ni mabavu tu yatayomuhakikishia ushindi mgombea wa CCM (staji jina kwani sijuin kama atakuwa Magu au Membe au mwingine). Kwa sababu mara hii wna CCM wamedhamiria kuvunja utamaduni na kufuata katiba ya CCM.
utamaduni upi boss? hao wana CCM ni kina nani? wataje basi!
 

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,148
2,000
utamaduni upi boss? hao wana CCM ni kina nani? wataje basi!

Utamaduni: Rais kupitia tiketi ya CCM, baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha urais huwa ni pekee automatically anachaguliwa kugombea tena japokuwa katiba ya CCM inaruhusu wengine kuchukua fomu. Safari hii wapo wanaotaka kuchukua fomu na kupitia mchakato mzima - aka kuvunja utamaduni.

Pili unauliza "hao wana ccm ni akina nani?" jibu lipo katika maandishi yangu nanukuu " (sitaji jina kwani sijui kama atakuwa Magu au Membe au mwingine). Na kwa ufafanuzi zaidi sikiliza Klip ya Membe aliyoitoa akiwa Lindi na kueleza nia yake ya kuchukua fomu.
 

Mozwaa

Member
Mar 31, 2020
10
45
Write your reply...Hivi wale wanaosemaga tukutane october huu msemo waliutoa wapi? Wanaogopa kivuli chao wenyewe. 🚮
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom