UPDATE: Zitto, Bwege na wenzake wasafirishwa usiku kutoka Kilwa hadi Lindi. Waachiwa kwa dhamana

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,303
2,000
Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe na viongozi wenzake 6 walisafirishwa jana usiku kwa gari la wazi kutoka Kilwa hadi Lindi

Magari ya Chama hicho yalifuata nyuma msafara wa Polisi ili kuhakikisha Usalama wa Viongozi wao ambapo walifanikiwa kufikia Kituo cha Polisi Lindi saa 7 usiku

Aidha, Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara (Bwege), aliyeugua jana ghafla wakiwa Kituo cha #Polisi Kilwa na kukimbizwa Hospitali ya Kilwa Masoko, amefikishwa Lindi na Polisi

Hali ya Bwege imetengemaa leo na yupo kituoni hapo pamoja na Zitto na Viongozi wengine huku Mawakili wa ACT wa Lindi na waliotoka Dar wakiwasili Kituo cha Polisi #Lindi ili kushughulikia dhamana

Pia, soma: Lindi: Zitto Kabwe na Sulemani Bungara (Bwege) wakamatwa na Polisi

----UPDATE----

LINDI: ZITTO KABWE NA VIONGOZI WENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na wenzake 7 wameachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja na kutakiwa kuripoti Polisi Lindi Julai 01, 2020

Kwa mujibu wa ACT hakuna masharti mengine ya dhamana kwa viongozi hao waliokamatwa jana Wilayani Kilwa na kusafirishwa hadi Kituo cha Polisi jana usiku

Awali, walikuwa wanashtakiwa kwa kufanya maandamano bila kibali cha Polisi lakini baadaye shtaka likageuzwa na kuwa kutishia uvunjivu wa amani

Zito.jpg
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,606
2,000
Wanatendewa kama wahalifu sijui kosa lao ni kuwa wanasiasa wa upinzani Tanzania?

Bora wafute hiyo sheria ya vyama vingi wabaki peke yao, msiwatese wengine.

Jana nimeona picha makamu wa Rais alikuwa na kikao cha ndani na nguo zao za kijani, kwani polisi hawakuwa na taarifa za "mhalifu" yule?
 
Rudeboytz

Member
Jun 23, 2020
80
225
Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe na viongozi wenzake 6 walisafirishwa jana usiku kwa gari la wazi kutoka Kilwa hadi Lindi

Magari ya Chama hicho yalifuata nyuma msafara wa Polisi ili kuhakikisha Usalama wa Viongozi wao ambapo walifanikiwa kufikia Kituo cha Polisi Lindi saa 7 usiku

Aidha, Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara (Bwege), aliyeugua jana ghafla wakiwa Kituo cha #Polisi Kilwa na kukimbizwa Hospitali ya Kilwa Masoko, amefikishwa Lindi na Polisi

Hali ya Bwege imetengemaa leo na yupo kituoni hapo pamoja na Zitto na Viongozi wengine huku Mawakili wa ACT wa Lindi na waliotoka Dar wakiwasili Kituo cha Polisi #Lindi ili kushughulikia dhamana

Pia, soma: Lindi: Zitto Kabwe na Sulemani Bungara (Bwege) wakamatwa na Polisi
Hawajui siasa zinazotumika (labda pride international milele)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom