Update: Usaili wa TRA Matokeo kutoka ndani ya siku 10 wasailiwa waendelee kujiandaa vitu si rahisi.

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi waliofanya usaili wa mchujo kwa nafasi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa matokeo ya usaili huo, yanatarajiwa kutolewa katika kipindi kisichozidi siku kumi (10) kuanzia siku ya tangazo hili.

Amesema kuwa kutokana na muitikio mkubwa wa waombaji kazi waliojitokeza kwenye usaili huo, kwa sasa zoezi linaloendelea ni kusahihisha mitihani hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika ndani ya muda huo, kwa kuwa usaili wa ana kwa ana (oral Interview) unategemewa kufanyika kuanzia tarehe 18 Septemba, 2017.

Aidha, amesisitiza waombaji kazi wote waliofanya usaili huo kuendelea kujiandaa kwa ajili ya usaili unaofuata kwa wale watakaochaguliwa, ili kujiweka katika nafasi ya kufanya vizuri kutokana na ujuzi na weledi walionao katika taaluma zao na hatimae kuwa miongoni mwa watakaofanikiwa kuajiriwa katika Utumishi wa Umma kupitia mamlaka hiyo.

Amewataka wasailiwa watakaoitwa kwenye usaili wa mahojiano watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, cheti cha kidato cha nne, kidato cha sita, Astashahada, Stashahada ya juu, Shahada na kuendelea kulingana na kiwango cha elimu waliyonayo. Aidha kwa wale waliosoma nje ya Nchi wafike na cheti cha uhakiki toka Mamlaka zenye dhamana ambazo ni TCU, NACTE na NECTA.

Sambamba na hayo, anawakumbusha wasailiwa hao kuendelea kuitunza namba zao za usaili kwa kuwa matokeo yote yatatolewa kupitia namba walizopewa wakati wa usaili.

Usaili huo wa mchujo ulifanyika kwa muda wa siku tatu katika kanda kumi ambazo ni Zanzibar, Mbeya, Dodoma, Arusha, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Tabora, Iringa na Dar es Salaam kulikokuwa na vituo viwili vya usaili ambavyo ni Chuo cha Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma tarehe 6 Septemba, 2017.
 
mhhh ile pepa ilikua maji tegemea kuaona 90 marks za kwanza
 
Yakitoka msinicheke naomba

Maana nahisi nitakua wa kwanza kufeli sijui, ila tumuachie Mwenyezi Mungu
 
Back
Top Bottom