Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli atazikwa nyumbani kwao Chato Machi 26, tofauti na tarehe iliyotajwa awali ambayo ilikuwa Machi 25.
Mwili wa Rais Magufuli utaagwa na wananchi wa Dar, Machi 20 na 21 Uwanja wa Uhuru kabla ya kusafirishwa kwenda Dodoma ambapo utaagwa Machi 22.
Baada ya Dodoma mwili utapelekwa Zanzibar ambao watapata nafasi ya kuaga Machi 23. Kisha utaelekea Mwanza ambapo wataaga Machi 24.
Ukitoka Mwanza, mwili wa Rais Magufuli utapelekwa Chato ambapo utaagwa Machi 25. Kisha Machi 26 itakuwa siku ya Mazishi huko Chato Mkoani Geita.