Update :Mama mzazi wa mtoto aliyekatwa mkono awashukuru wakazi wa Mbeya na majirani waliotoa taarifa

Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,459
4,748
MAMA MZAZI WA MTOTO ALIYEKATWA MKONO AWASHUKURU WAKAZI WA MBEYA NA MAJIRANI WALIOTOA TAARIFA YA KUTESWA KWA MTOTO WAKE

20121117_135117.jpg

MAMA MZAZI WA ANETH ASERA MKANDARA

20121118_132220.jpg
20121117_135109.jpg



ANETH SASA ANAEDELEA VIZURI
20121118_130121%231.jpg
UMATI WA WAKAZI WA MBEYA WANAOENDA KUMWONA MTOTO ANETH HOSPITALINI HAPO
MAMA wa mtoto Aneth Johanes aliyefanyiwa unyama na hatimaye kukatwa mkono Asera Mkandara ametoa shukurani kwa wananchi wa Mbeya na majirani waliosaidia kutoa taarifa na hatimaye kuokoa maisha ya mwanaye aliyekuwa akiishi kwa mateso.


Bi. Mkandara alizungumza hayo alipotembelewa na wanahabari waliofika wodi namba 8 kumjulia hali mtoto Aneth na kusema kuwa alipewa taarifa za kutokea kwa matatizo ya mwanaye lakini hakufafanuliwa ni tatizo gani alilopata.


Anasema kuwa amewasili Jijini Mbeya akitokea kwao Muleba Bukoba na kumkuta mwanaye Aneth ambaye ni mtoto wake wa pili baada ya mwanaye wa kwanza mwenye umri wa miaka 7 anayelelewa na bibi yake mjini Bukoba.


Anasema kuwa hata hivyo yeye hana shughuli maalumu zinazomuendeshea maisha yake isipokuwa biashara ndogo ndogo hivyo kuchukuliwa kwa mtoto wake na kaka yake aliyemtambulisha kwa jina moja la Mkandara ilikuwa ni sehemu ya msaada kwake.


Mama huyo anafafanua kuwa anashukuru kukuta mwanaye ni mzima na anawashukuru madaktari waliompa msaada kwani inawezekana huduma za matibabu zingechelewa angeweza kupata madhara makubwa.


Anasema kuwa kwa sasa anasaidiwa na ndugu na majirani na baadhi ya watu wanaomiminika hospitalini hapo kutoa msaada.


YEYOTE MWENYE MAPENZI MEMA ANAWEZA KUTOA MSAADA KUPITIA NAMBA YA SIMU YA MKONONI YA MAMA HUYO 0756-293784
source mbeya yetu blog .haya jamani wapendwa kutoa ni moyo kwa yeyote aliyeguswa na hili unaweza fikisha mchango wako kwa huyo mama.kuna wengi waliotaka kumsaidia mtoto huyu ikakosekana jinsi Thanda sosoliso na wengine wengi na mimi pia nivea ndio sababu nuilifuatia sakata hili mpaka hapa.​
 
dah

imenisikitisha sana hii habari dada nivea
ngoja tujitafute tafute mana kutoa ni moyo
watu wamekua hawana utu siku hizi.
 
Mi ningemsaidia, lakini tatizo nina pepo anayetaka kila msaada ninaoutoa malipo yawe ngono zembe
YEYOTE MWENYE MAPENZI MEMA ANAWEZA KUTOA MSAADA KUPITIA NAMBA YA SIMU YA MKONONI YA MAMA HUYO 0756-293784
 

YEYOTE MWENYE MAPENZI MEMA ANAWEZA KUTOA MSAADA KUPITIA NAMBA YA SIMU YA MKONONI YA MAMA HUYO 0756-293784
source mbeya yetu blog .haya jamani wapendwa kutoa ni moyo kwa yeyote aliyeguswa na hili unaweza fikisha mchango wako kwa huyo mama.kuna wengi waliotaka kumsaidia mtoto huyu ikakosekana jinsi Thanda sosoliso na wengine wengi na mimi pia nivea ndio sababu nuilifuatia sakata hili mpaka hapa.

Nivea Nashukuru sana mwitikio wa watu umekuwa mzuri.. Nitatuma mchango wangu kwenda namba hiyo mwishoni mwa mwezi huu.. Mungu amsaidie huyo mtoto na ampe moyo wa ujaciri.. Tukemee kwa nguvu zetu zote ukatili kama huu kwa watoto..
 
hii habari imenisikitisha sana yaani kila nikisoma machozi yananitoka nashindwa hata kumalizia kuisoma
 
Mdogo wangi nivea nimeguswa mno na hili tatizo, sijui binadamu kwa nini tumeanza kuwa na mioyo ya kikatili hivi siku hizi?! Mungu atusaidie.
 
Last edited by a moderator:
Mdogo wangi nivea nimeguswa mno na hili tatizo, sijui binadamu kwa nini tumeanza kuwa na mioyo ya kikatili hivi siku hizi?! Mungu atusaidie.
Hii habari imenigusa sana na imeniumiza sana kwa asilimia kubwa ilibidi shemeji yako anipe cancelling maan kila sekunde nisikitika niko naisoma yaaani nalia ikafika mahali its too much na ndio sababu nikaifuatilia sana ,nilijitolea kuliko aishi ktk mikono ya watu wasio salama mimi niko radhi nimchukue ila nashukuru ana mama mwenye nguvu,wasiwasi wangu n pale in absence of her mama maisha yatakuwa magumu sana kwake ee mungu mtie nguvu
 
hii habari imenisikitisha sana yaani kila nikisoma machozi yananitoka nashindwa hata kumalizia kuisoma

Nikweli inasikitisha sana sana tu ndugu yangu,ila huyo mama nae kazidi nimesoma kwa gazeti la mwanainchi mwanae wakwanza nae analelewa pia,hajui majira?anawazaa watoto wanini kma hawezi kukaa nao jamani,ningekuwa karibu nae ningemshauri afunge kizazi chake tu.
 
Back
Top Bottom