Update Liyumba's case | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Update Liyumba's case

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, May 6, 2009.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mods, hii inaweza kuunganishwa na main thread baadaye.

  waendesha mashitaka leo wamekiri mahakamani Kisutu kuwa mashitaka waliyomfungulia Liyumba na mwenzake yana makosa. Kwa hiyo wameiomba mahakama kui-dismiss kesi hiyo. Lakini wamekataa Liyumba na mwenzake kuwa aquitted.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Source mkuu?

  Assuming this is true,

  Usanii mwingine bwana? Sasa wameiomba mahakama kudismiss kesi......then wanakatalia kuwaaquit watuhumiwa....siwamalizie hilo sinema lao tu!...arrrggghh
   
 3. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  shame....
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,942
  Trophy Points: 280
  Kumbe ndio maana kule mtaani wana hukumu wenyewe wahalifu eeh? maana wamechoka na usanii wa aina hiyo.
  Nadhani bado na zingine
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  comedians
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280
  ijumaa/sani ??
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Yeye Mwenyewe MN!
   
 8. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kama hii habari ni ya kweli, basi the so called "learned brazas" (lawyers) of tz are as good as makanjanja waliovamia taaluma ya habari. Inanipa shaka kuamini uwezo wa kiakili wa wanasheria wa serikali coz mwaka mzima walikuwa wanaanndaa mashtaka ya kina Liyumba kabla ya kuwapeleka mahakamani, ghafla leo wanakiri yanamakosa!

  Jamani huku ni kuchezea kodi za wananchi, ni "bora hizi pesa" zingetumika kuileta timu ya mpira ya Real Madrid mwaka jana kama rais wetu alivyoenda kuiomba ije tz! Potelea mbali hata kama rais wetu hajui vipaumbele vya nchi hii ya wadanganyika!!!!
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Drama still continue............
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  bangi tupu walah
   
 11. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  if true this's shit
   
 12. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  JK "kukumbatia maji kama jiwe ni UJIINGA" Mrisho Mpoto
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  i knew this was coming sasa bado akina YONA & CO

  safi sana kilichobaki sasa yeye anatakiwa kuisue JAMHURI kwa kumpakazia na kumpotezea income na kumsababishia matatizo ya kisaikolojia etc

  litigation lawyers wakati wenu ndio huuu
   
 14. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Duh!
  I'm sure there are still more to come...
  watch this space.......
   
 15. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  huu ni usanii wa kisheria...na kutufanya wajinga waTZ...
  kama ni kweli...inawezekana hiyo ikawa ndio dalili za muelekeo wa kesi za EPA...
   
 16. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Si usaniii. Suala la kufanya kazi kwa 'emotions' zinazoambatana na ku-please 'wanene' bila kujali 'Etiquette Rules'. Unategemea nini hapo? FBI wanaweza kukuchunguza miaka bila kukurupuka na siku wakikuweka kati hutoki kwa sababu wanakuwa wananondoz zote za kuweza kukufunga. Sisi ukihisi tu unakimbia Kisutu kufungua mashtaka mwisho wa siku unakuja kusoma vifungu vya sheria unakuta hujajenga hoja.

  Upande wa pili wa shilingi, unaweza kukuta ni hujuma zinazoendeshwa kutokana na 'scenario' niliohitaja hapo. I wish tungekuwa na Kikosi kama cha 'Scorpion' cha South Africa ambacho kilikuwa mwiba kwenye utawala wa ANC. Bosi wao sasa hivi yupo hapa DC kwenye office za WB - Integrity Office kwa sababu ya utendaji wake uliotukuka na si ufisadi bin majungu.
   
 17. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mnashangaa nini wakati ili ni jamo la kawaida bado mafisadi wote watatoka na kudai fidia, kesi zitakwenda mbio na watalipwa fidia yao halafu watachangia CCM ili iweze kuendelea kuwa madarakani na CCM kwa upande wake itakuwa imepata pesa za kampeni.

  Tulipiga kelele wakamatwe walipokamatwa nilito angalizo kuwa kukamatwa hakuna maana tumeshinda ila tunatengeneza sources ya pesa ya uchaguzi kwa CCM kwani njia nyingine zote zimeshindikana.

  Hata kama sheria ya kueleza pesa ya uchaguzi imetoka wapi, bado hapo hatuwakamata hata kidogo kwani watu walilipwa fidia ya kukamatwa bila makosa na kusoteshwa keko halafu wakatoa kwa moyo mmoja bila kinyongo kwa CCM.

  The commedy nafikiri ndio imeanza sasa tukae vizuri kwenye viti vyetu na pop corn kuangalia nchi yetu ikiteketea mikononi mwa wachache waliopewa madara na baba zao, ili kulinda madara wakakalibisha wageni wenye nazo.
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapo umenena, na hicho ndicho kinachotokea. mashitaka hayaku-base kwenye sheria yoyote na mawakiliw a Liyumba wameeleza hilo wazi wazi kuwa mashitaka yapo yanaelea hewani
   
 19. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hi habari ni kweli au sio kweli....???
   
 20. M

  Mwakaleli Member

  #20
  May 6, 2009
  Joined: Sep 23, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UPANDE wa mashitaka umekiri katika kesi inayowakabili mkurugenzi wa zamani wa Utawala na Utumishi Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na Meneja Miradi wa benki hiyo, Deograthias Kweka kuwa hati ya mashtaka inayowakabili washitakiwa hao ina makosa.

  Hayo yalifahamika jana mara baada ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema kutupilia mbali pingamizi lilotolewa na upande wa mashitaka na kuunga mkono maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa utetezi ya kutaka hati ya mashtaka ifutwe na washtakiwa waachiwe huru.

  Pingamizi lililotupwa ni madai kuwa vifungu vya sheria vilivyotumiwa na upande wa utetezi kuwasilisha maombi yao mahakamani kutaka kesi hiyo ifutwe vina makosa.

  Akitoa uamuzi huo Hakimu Lema alisema anakubaliana na maombi yaliyowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi kuwa hati ya mashitaka inayowakabili wateja wao ina makosa.

  Uamuzi huo ulifuata baada ya Jopo la Mawakili wa upande wa utetezi kuwasilisha maombi ya kutaka hati hiyo ya mashitaka ifutwe kabisa na wateja wao waachiwe huru kwa sababu ina makosa kisheria.

  Mawakili hao wanataka wateja wao kwa kuwa uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) wa kuwashitaki wateja wao una dosari za kisheria, hivyo wanataka ifutwe kabisa.

  Pia mawakili hao wanataka shitaka la tatu linalowakabili wateja wao la kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh 221 bilioni liondolewe kwani halijawekwa wazi kwamba washitakiwa wamefanya kosa gani.

  Baada ya kuwasilisha maombi hayo, Wakili wa Serikali, Boniface Stanslaus alikiri kuwa hati yao ya mashitaka ina mapungufu na kuomba washitakiwa wasiachiwe huru kama hawana hatia, bali kwa sababu hati ya mashitaka yanayowakabili ina makosa.
  Stanslaus alifafanua kuwa washitakiwa wangeweza kuachiwa huru kabisa iwapo mahakama ingekuwa imesikiliza ushahidi na kuthibitisha kama washitakiwa wana hatia au la lakini katika shauri hili halijafikia hatua hiyo.
  Source: Mwananchi
   
Loading...