Kikao changu na makampuni ya simu kuhusu kesi ya kuibiwa vifurushi

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
KIKAO CHANGU NA MAKAMPUNI YA SIMU KUHUSU KESI YA KUIBIWA VIFURUSHI.

Bashir Yakub, WAKILI
0714047241.


Ndugu wapendwa mnakumbuka wiki iliyopita niliwapa taarifa kuwa baada ya kutangaza na kuanza utaratibu wa kuyashitaki makampuni manne ya simu Tigo,Vodacom,Airtel na Halotel nilipata ujumbe kutoka TCRA-CCC wakiniomba kukutana na kufanya kikao cha pamoja wao TCRA-CCC,upande wangu, na kampuni hizo za simu kuhusu yale mambo ninayotaka kushitaki.

Kwa lengo la kumbukumbu nilisema nazishitaki kampuni hizo nne katika mambo matano, Kwanza vifurushi vyote visiwe na muda wa kuexpire,Pili iwepo ruhusa ya kuhamishiana vifurushi kama ilivyo muda wa maongezi, Tatu kutochanganya vifurushi na muda wa kawaida wa maongezi pale unapokuwa unaongea au kutumia data bila ruhusa ya mtumiaji, Nne vifurushi vya watu kuliwa hovyo wakati mtu hajatumia au ametumia kidogo, na Tano kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa kifurushi kinapokaribia kuisha na si kinapoisha.

Basi, wiki iliyopita kuanzia jumatano na alhamisi tulifanya kikao hicho ambapo jumatano saa nne asubuhi hadi saa sita tulianza na Vodacom, saa sita hadi saa nane mchana tulikuwa na Airtel. Wakati alhamisi saa nne mpaka saa sita ilikuwa Tigo na saa sita mpaka saa nane mchana ilikuwa TTCL. Halotel hawakutokea labda waje baadae.

Kwa ujumla kuhusu mambo haya matano wamekubali kuyapokea na kuahidi kuyafanyia kazi.

Airtel wao wamesema moja wameshalifanyia kazi tangu tarehe 4 mwezi huu wa 11/2019 ambapo sasa kifurushi cha data kikiisha muda wa kawaida wa maongezi hauwezi kuunganishwa moja kwa moja bali utaulizwa iwapo uendelee au ujiunge upya.Haitoshi wafanye hivyo hata kwenye kuongea.

Aidha, kwa pamoja hoja yao kuu ni kuwa malalamiko mengi ya wateja yanasababishwa na kutokua na elimu ya kutosha kuhusu mitandao.

Hoja hii nimeikataa kwa nguvu zangu zote. Kwanza, watanzania ni waelewa na si washamba wa huduma. Si washamba wa huduma kwasababu kabla ya kuja huduma zao za simu Watanzania tayari walikuwa wakitumia huduma nyingine nyingi tu zikiwemo za maji, umeme, simu za mezani na huduma nyingine nyingi.

Mbona hawakuwahi kulalamikia huduma hizi kwa kiwango zinacholalamikiwa kampuni za simu za sasa. Kwahiyo wasitake kujifanya huduma yao ni ya kwanza kwetu, hapana, kabla yao tumetumia huduma nyingi na bado tunaendelea kutumia huduma nyingine nyingi nje ya huduma yao na kwa msingi huu sisi si wajinga wa huduma bali tu waelevu mno.

Pili, kwani inahitaji elimu ya kiasi gani kujua kuwa nimepewa dakika 50 au MB 1000 lakini kwa namna nilivyotumia hizi dakika 50 au MB 100 hazipaswi kuwa zimeisha kwasasa. Hili nalo linahitaji degree ngapi jamani. Mbona hatulalamikii Units za umeme kuisha haraka, mbona hatulalamikii mafuta kwenye magari kuisha haraka, nk,nk.

Watanzania ni maprofesa, ni madk wanatengeneza mabarabara, wanajenga majengo marefu,wanaendesha madege na viwanda halafu washindwe kuhesabu vifurushi,ujinga mtupu.

Tatu, Malalamiko haya hayawezi kupuuzwa au kujibiwa kwa hoja dhaifu kama hizo ati watumiaji hawana elimu ya mtandao. Hii ni kwasababu ya wingi wa walalamikaji ambapo karibia 90% ya watumiaji wote wa simu wanalalamika na malalamiko yanatoka kada zote.

Watu maskini wanalalamika, wa uchumi wa kati wanalalamika, matajiri wanalalamika, viongozi hadi wa ngazi za juu wanalalamika, makampuni na taasisi zinalalamika hadi wafanyakazi wao wenyewe baadhi wanalalamika. Katu hili haliwezi kuwa jambo dogo.

Niliwapa chalenji kuwa kama wanataka kuujua ukubwa wa malalamiko haya watangaze kuwa wanaokerwa na mambo haya waje kwenye ofisi zao siku fulani. Nimewaambia barabara zote zilizo katika maofisi yao siku hiyo zitafungwa kwa mafuriko ya watu. Halafu mtu apuuze.

Zaidi, wamesema hata kama watafanya mabadiliko katika mambo haya halitakuwa jambo la siku moja kwakuwa mabadiliko yanahitaji kubadilisha mfumo pia(system). Ni hivi, sisi tunachohitaji ni mabadiliko tena ya haraka kwasababu tumechoka.

Mwisho ni kuhusu utaratibu wa kesi. Sijasitisha utaratibu wa kesi dhidi yao kwasababu ya vikao. Kesi iko palepale tunasubiri tu zile siku 30 ziishe. Kama mabadiliko yatakuja wakati kesi ikiendelea tutafuta kesi wala hakuna kinachoharibika.

Zaidi, tutahitaji sahihi za wale wote wanaokerwa na mambo haya kujiorodhesha ili jambo hili lisiwe la mtu mmoja. Utaratibu nitawafamisheni badae. Asanteni na tushirikiane.
 
Kwa kuongezea, unapopigiwa simu na mtu data zako zisitumike kwasababu sio wewe uliyepiga, lakini huwa nashangaa nampigia mtu simu tunaongea baada ya muda, Simu yake inakata. Anaweza kukutumia ujumbe kwa simu nyingine DATA ZIMEISHA.

Mimi ndiye nimepiga sasa hiyo mitandao yao inatumia data mara mbili kwa mpigaji na aliyepigiwa?!

Na kwanini ukiwa na voda uka mpigia mtu wa tigo dakika zinaliwa sana?! Nchi moja hii connection fee inatoka wapi?!
 
Back
Top Bottom