UPDATE 4: Yafahamu mambo 10 yanayomuhusu Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden Mputa'.

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Katika kuelekea ile sikukuu yetu ya tarehe 01.10.2016, leo nawaletea kwenu Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden Mputa'.. Living Legend wa Simba SC.
Huyu kiumbe ni nani katika nchi hii??

1. Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden Mputa' alizaliwa Oktoba 11, 1949 katika mtaa wa Kiburugwa, Mbagala uliyopo jijini Dar es Salaam.

2. Akiwa na miaka 20 tu, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ alijiunga na Simba SC , iliyokuwa ikiitwa Sunderland.

3. Mnamo mwaka 1974, aliiongoza Simba SC kuwa klabu ya kwanza na pekee Tanzania kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika, ambapo ilitolewa kwa mikwaju ya penalti nchini Misri na Mehalla El Kubra.

4. Mnamo Julai 19, 1977 ndipo aliingia katika vitabu vya kumbukumbu na hii ilikua ni katika mechi dhidi ya watani wetu Yanga.. Ambapo tulishinda goli 6. Katika mechi hiyo Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ alifunga magoli 3 na mpaka leo rekodi hii haijavunjwa.

5. Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘Kingn Kibadeni’ anaitwa King kutokana na yeye kucheza namba 10 kipindi kile na wakati ule mfalme wa dunia kwenye mpira alikuwa ni [B[Pele[/B], na yeye alikuwa anavaa jezi namba 10. Kutokana na umahiri wake kwenye soka basi watu wengi wakawa wanamfananisha nae na hapo ndipo jina la King lilipoanza.

6. Aliitwa jina la Kibadeni na watoto wenzake kutokana na kucheza soka la nguvu akiwa umri mdogo uliochagizwa na ufupi wake. Kibadeni maana yake ni kitu cha baadae.. Na hii ilikua ni Mwaka 1959 [akiwa na miaka 10 tu].

7. Jina Chifu Mputa ni jina la Chifu wa Songea. Baada ya kustaafu kucheza soka Simba SC, mwaka 1979 alikwenda Majimaji Songea kama kocha na kule napo kutokana na kuipatia mafanikio timu hiyo ndipo wakampatia jina la Chifu Mputa na mpaka leo navyoandika haya bado Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni Mputa’ anaheshimika kama Chifu Mputa katika mji wa Songea. Ikumbukwe huyu "living legend" ni Mzaramo.

8. Mnamo mwaka 1993, aliiwezesha Simba SC kufika Fainali Kombe la Shirikisho akiwa kama Kocha. Mnyama alifungwa kwenye mechi ya fainali ya pili jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0 dhidi ya Stella Abidjan, baada ya sare ya bila kufungana ugenini. Rekodi hiyo haijavunjwa hadi leo ikiwa ni miaka 23 baadaye.

9. Mwaka 2011 Abdallah Athumani Seif alikwenda Hijja.

10. Mwaka 2013 Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni Mputa’ alirejea tena Simba SC akiwa kama kocha, japo hakudumu sana. Sasa hivi King anatumia mda wake mwingi katika Academy yake ya kukuza vipaji vya soka ambayo inaitwa Kibadeni Soccer Academy [KISA].

Kwa jinsi navyoiona tarehe 01.10.2016.. Kuna Bunduki ya Mnyama inaenda kuivunja rekodi ya Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni Mputa’ aliyoiweka Julai 19, 1977.. TUKUTANE OCTOBA.

SIMBA SPORTS CLUB, NGUVU MOJA
 
Wazee wa 6-0.. Kibadeni ni wa tatu toka kushoto.

1473681089388.jpg
 
Back
Top Bottom