Upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa umekuwa dili Kinondoni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,667
30,584
Sasa ni rasmi hata hawa tuliowathamini watutengeneze vyeti vya kuzaliwa watoto wetu wameanza kufanya dili. Ni wiki ya pili sasa watu wanaambiwa nenda rudi nenda rudi. Tunaomba mamlaka husika, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni pitia uone uhuni unaoendelea. Wapo watu hawakai kwenye foleni na wanapiga simu jamaa wanatoka wanarudi ndani gafla wanatoka na vyeti.

Sio mara ya kwanza bahati waziri aliiingilia walipokuwa Muhimbili. Urasimu kila kona wakaacha na kuanza kunyenyekea wananchi. Sasa naona hapa wilaya ya Kinondoni embu mh pitia angalia wamama wanavyoteseka na kulalamika.

Hivi hawajui wengi wanaokuja wameacha watoto wanaonyonyesha jamani, kwani wao hawazai mpaka wawatese watoto wa wanawake wenzao hivi!

Tunaomba uongozi husika msimamie hili else tutaleta jambo leo mda si mrefu.
 
Fafanua mada yako vizuri, maana inafamika kabisa baada ya kukamiliza vielelezo vya msingi ajiri ya kuomba cheti inapaswa ukae ndani ya siku zisizozidi 30 ndio uende kuchukua cheti , kwaiyo ebu tueleze wewe unambiwa uende urudi kiaje, hao unao sema wanakuja wanachukua vyeti na kuondoka wanachukua kwa utaratibu upi tuambie
 
Back
Top Bottom