upatikanaji wa nyumba NHC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

upatikanaji wa nyumba NHC

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kalunguine, Jul 29, 2011.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwa aliye na taarifa au uzoefu wa jinsi ya kuweza pata nyumba ya NHC dar es salaam maeneo yeyote yale naomba anijuze.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  je umefanya application kunakohusika?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,421
  Likes Received: 19,731
  Trophy Points: 280
  je wewe ni mhindi?
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sijui kama znapatikana.Maana kuna watu waliozikamata na wao wanapangisha tena.Na kama unataka city center uwe na mamilioni.Otherwise tafuta ndugu NHC tena awe na cheo.
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kupata nyumba ya NHC ni ndoto kabisa siku hizi, kuna urasimu na ukiritimba wa hali ya juu....
  hizi nyumba karibu zooote zina wapangaji (wanarithishana bila kufuata utaratibu). utakuta mpangaji halali nyuma yake kuna wapangaji hata watatu. Kodi ya pango inakuwa ghali kupindukia.

  na ukiipata ambayo inataka kupangishwa ni lazima 'uwe mtu fulani' na hao wakina fulani mara nyingi hawaishi hump wanazipangisha tena kwa kodi ya juu zaidi. ni mzunguko unaokera sasa.

  NHC ni moja ya mashirika yanayoendeshwa kipuuzi kabisa. na haya yote nina uhakika wahusika wanayafahamu na wengine pengine wanahusika kwenye huu mchezo mchafu.
   
 6. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  je, wewe ni kada mwandamizi wa chama fulani??? Kama jibu ni hapana, basi huna nafasi ya kupata nyumba ya nhc!!!
   
 7. D

  Danniair JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa habari za jana, andika maombi yako kwa Mkurugenzi Mkuu (Maka makuu yako barabara Mandela, mkabala na uwanja wa taifa), yapeleke kwa mkono. Ukifika pale utaonyeshwa umuine nani, yeye atakupatia fomu ambazo utajaza. Mambo ya kodi SIKUAMBII kwani si biashara yangu. Mambo yooote waliyoyasema hapo juu yalikuwa ni utaratibu mbaya wa zamani ambao sasa wameufuta ni historia.
   
Loading...