“Upatikanaji wa matangazo ya TV katika vijiji elfu 10” wawezesha watu wa Afrika kutazama mechi nyumbani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
b64543a98226cffccd0eee40431f8599f703eac1.jpeg

Tarehe 6 Februari ni siku muhimu kwa shabiki mkubwa wa soka Jackson Ndongo. Yeye na wanakijiji wenzake walitazama fainali ya Kombe la Afrika 2022 iliyofanyika Yaounde, mji mkuu wa Cameroon mbele ya televisheni kijijini, wakinywa mvinyo wa mawese. Katika mwezi uliopita, kutazama mechi ulikuwa wakati muhimu zaidi na Ndongo baada ya kumaliza shughuli za kilimo shambani kila siku.

Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mjini Jonannesburg mwaka 2015, na kutoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili katika sekta ya utamaduni, na moja ya hatua ni kuzindua huduma za matangazo ya TV ya kidigitali kwenye vijiji elfu 10 barani Afrika, kikiwemo kijiji cha Djounyat anachoishi Ndongo, umbali wa kilomita 70 kaskazini mwa mji mkuu wa Cameroon. "Hapo awali ilikuwa ngumu kutazama mechi," Ndongo alimwambia mwaandishi wa habari, "kwa sababu nyumbani hakuna TV, kila mechi ilipochezwa, lazima niende kutazama kwenye baa ya mji umbali wa kilomita moja kutoka nyumbani kwangu. Wakati mwingine tulichelewa na kukosa ufunguzi au kipindi cha mwanzo cha mechi."

Kwenye chaneli za TV zinazopatikana, mbali na mechi za soka, pia kuna habari za kimataifa na za ndani, elimu ya kujikinga na maradhi, na hata tamthilia za Kichina. Na Sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya 2022 iliyofanyika siku chache zilizopita pia imetazamwa kupitia jukwaa hili. Pamoja na kustawisha maisha ya watu wa Afrika, huduma hiyo imewaletea dirisha la kuona dunia, kuwasaidia kuvunja mitazamo yenye upendeleo na kupanua upeo wao. Vijana wengi wa vijijini wameanza kugundua kuwa kuna fursa nyingi zaidi nje na wanapanga kushuhudia wenyewe.

Si hivyo tu, takwimu zinaonyesha kuwa mradi huo pia umeandaa zaidi ya wataalam 600 wa Afrika. Laurent Bella, 32, ni mmoja wao. Akiwa meneja wa kanda ya Afrika ya Kati wa kampuni ya startimes ya China, inayotekeleza mradi huo, Bella alisema kuwa uzoefu wake wa kikazi katika kampuni ya China umemsaidia yeye na vijana wengine kupata mengi. "Sio tu kwamba tumetengeneza pesa, na kuboresha maisha, pia tumejifunza mambo mapya."

Hapo awali, ushirikiano kati ya China na Afrika ulijikita kwenye kujenga madaraja na barabara. Leo China inatumia teknolojia ya hali ya juu kuzisaidia nchi za Afrika kujenga mitandao ya mawimbi ya televisheni ya kidijitali, kuhamisha teknolojia na kuboresha uwezo wa nchi za Afrika kuzalisha bidhaa za kidijitali. Kwa mujibu wa takwimu zisizokamilika, kuanzia Januari 2019, huduma ya upatikanaji wa TV ya kidigitali ilizinduliwa nchini Uganda hadi mwisho wa 2020, kutokana na mradi huu, TV za kidigital zimeingia katika zaidi ya vijiji 8,000 barani Afrika, na kunufaisha zaidi ya familia laki 1.72.

Likiwa ni jambo la uvumbuzi katika maendeleo ya zama za leo, katika Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Novemba mwaka jana, "uvumbuzi wa kidijitali" uliandikwa kuwa moja ya "miradi tisa" inayotekelezwa kwa pamoja kati ya China na Afrika katika miaka mitatu ijayo. Kuanzia "upatikanaji wa TV ya kidigitali" hadi ushirikiano wa kidijitali, China itaendelea kutoa uzoefu na msaada katika ujenzi wa "Digital Africa", ili "Smart Africa" itimizwe haraka iwezekanavyo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom