Uzalishaji wa mende kwa matumizi ya binadamu na mifugo pamoja na masoko yake

Lengo la uzi wangu ni kujua kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa za upatikanaji wa soko la hao wadudu wenye faida nyingi pindi watumikapo kama chakula kwa binadamu na hata wanyama kwani wana kiwango kikubwa cha protini.

Na huku kwetu wanaliwa?
Namna ya kuwpika ikoje?
 
Ndugu wana JF

Naomba msaada kwa yeyote anayefahamu lilipo soko la wanunuzi wa wadudu aina ya mende kwa matumizi ya chakula cha binadamu na wanyama.

Kwa kipindi cha nyuma nilibahatika kuona makala ya ufugaji wa mende katika televisioni ya kimataifa ya CNN ambapo mwandaaji alimtembelea mkulima mmoja aliyekua na shamba la kufugia mende. Katika mahojiano yao nilipata kutambua mende wana soko kubwa kwa sasa duniani kutokana na faida ambazo walizitaja. Na mwenye shamba lile ambaye ni Mchina alisema mende wanahitajika sana hasa na makampuni makubwa ya madawa (pharmaceutical companies)View attachment 788157

Kwa sababu nilipendezwa na makala ile nilimfuata ndugu yangu na kumpa wazo lile, awali alikataa lakini baada ya kumshawishi sana alikubaliana nami na tukaanza shamba la majaribio. Matokeo ya majaribio yale tulizalisha mende wengi sana, lakini ilituwia vigumu kutafuta na kupata soko jambo lililotulazimu kusitisha mradi ule.

Lengo la uzi wangu ni kujua kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa za upatikanaji wa soko la hao wadudu wenye faida nyingi pindi watumikapo kama chakula kwa binadamu na hata wanyama kwani wana kiwango kikubwa cha protini.
Aiseeee naomba nifundishe nikawalishe kuku wangu
 
Nimewaza.

Mlianzisha shamba.

Kutokana na soko kujificha mkasitisha mradi.

Umesema wana protini nyingi.

Wale mende wa shamba la majaribio mliwapeleka wapi?
 
Ni kazi rahisi sana kuwazalisha, kama ni kwa ajili ya kuku unahitaji tu maboksi ya mbao yenye kipenyo kidogo kisha weka masalia ya chakula kidogo na makaratasi kisha weka sehemu yenye hoto la wastani.

Kama huna mbegu za mende weka maboksi yako sehemu ambazo ulishawaona mende wakipita baada ya hapo hakikisha panya hawaingii kwani watawapunguza sana katika hatua za mwanzo na utachelewa kupata matokeo mazuri. Kumbuka mende wanapendwa sana na panya.
 
Naona MTU anaanzisha maada na kujijibu mwenyewe kwa Multiple ID ili kuvuna wajinga
 
Nimewaza.

Mlianzisha shamba.

Kutokana na soko kujificha mkasitisha mradi.

Umesema wana protini nyingi.

Wale mende wa shamba la majaribio mliwapeleka wapi?
Kwa bahati nzuri sisi ni wafugaji wa kuku pamoja na bata pia. Hivyo kwa kiwango kikubwa tuliwapa kuku na bata ambao wanawapenda sana na kiwango fulani niliwala mimi mwenyewe kwani mengine waligoma.

Na mpaka sasa bado tunafuga kienyeji kwa ajili ya kuku na bata.

Pindi tukipata soko la uhakika tutaurejelea tena mradi wetu kwa kuboresha changamoto zilizojitokeza hapo awali, kwani tayani mwanga wa ufugaji wa wadudu hao tunao kwa kiwango fulani kizuri.
 
Ule urojo wake mweupe mtamu eeh?
 
Ha ha ha naona mate yanajaa mdomoni, sijui ni ishara ya uchu au kichefuchefu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom