Upatikanaji wa masoko ya mende hapa Tanzania

African Believer

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
358
Likes
324
Points
80

African Believer

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
358 324 80
Ndugu wana JF

Naomba msaada kwa yeyote anayefahamu lilipo soko la wanunuzi wa wadudu aina ya mende kwa matumizi ya chakula cha binadamu na wanyama.

Kwa kipindi cha nyuma nilibahatika kuona makala ya ufugaji wa mende katika televisioni ya kimataifa ya CNN ambapo mwandaaji alimtembelea mkulima mmoja aliyekua na shamba la kufugia mende. Katika mahojiano yao nilipata kutambua mende wana soko kubwa kwa sasa duniani kutokana na faida ambazo walizitaja. Na mwenye shamba lile ambaye ni Mchina alisema mende wanahitajika sana hasa na makampuni makubwa ya madawa (pharmaceutical companies)
wp_ss_20180528_0005-png.788157

Kwa sababu nilipendezwa na makala ile nilimfuata ndugu yangu na kumpa wazo lile, awali alikataa lakini baada ya kumshawishi sana alikubaliana nami na tukaanza shamba la majaribio. Matokeo ya majaribio yale tulizalisha mende wengi sana, lakini ilituwia vigumu kutafuta na kupata soko jambo lililotulazimu kusitisha mradi ule.

Lengo la uzi wangu ni kujua kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa za upatikanaji wa soko la hao wadudu wenye faida nyingi pindi watumikapo kama chakula kwa binadamu na hata wanyama kwani wana kiwango kikubwa cha protini.
 
Pyepyepye

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2017
Messages
753
Likes
1,063
Points
180

Pyepyepye

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2017
753 1,063 180
Lengo la uzi wangu ni kujua kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa za upatikanaji wa soko la hao wadudu wenye faida nyingi pindi watumikapo kama chakula kwa binadamu na hata wanyama kwani wana kiwango kikubwa cha protini.
Na huku kwetu wanaliwa?
Namna ya kuwpika ikoje?
 
Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
28,977
Likes
13,924
Points
280

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
28,977 13,924 280
Ndugu wana JF

Naomba msaada kwa yeyote anayefahamu lilipo soko la wanunuzi wa wadudu aina ya mende kwa matumizi ya chakula cha binadamu na wanyama.

Kwa kipindi cha nyuma nilibahatika kuona makala ya ufugaji wa mende katika televisioni ya kimataifa ya CNN ambapo mwandaaji alimtembelea mkulima mmoja aliyekua na shamba la kufugia mende. Katika mahojiano yao nilipata kutambua mende wana soko kubwa kwa sasa duniani kutokana na faida ambazo walizitaja. Na mwenye shamba lile ambaye ni Mchina alisema mende wanahitajika sana hasa na makampuni makubwa ya madawa (pharmaceutical companies) View attachment 788157

Kwa sababu nilipendezwa na makala ile nilimfuata ndugu yangu na kumpa wazo lile, awali alikataa lakini baada ya kumshawishi sana alikubaliana nami na tukaanza shamba la majaribio. Matokeo ya majaribio yale tulizalisha mende wengi sana, lakini ilituwia vigumu kutafuta na kupata soko jambo lililotulazimu kusitisha mradi ule.

Lengo la uzi wangu ni kujua kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa za upatikanaji wa soko la hao wadudu wenye faida nyingi pindi watumikapo kama chakula kwa binadamu na hata wanyama kwani wana kiwango kikubwa cha protini.
Aiseeee naomba nifundishe nikawalishe kuku wangu
 
Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Messages
11,310
Likes
18,381
Points
280
Age
25

Castr

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2014
11,310 18,381 280
Nimewaza.

Mlianzisha shamba.

Kutokana na soko kujificha mkasitisha mradi.

Umesema wana protini nyingi.

Wale mende wa shamba la majaribio mliwapeleka wapi?
 
African Believer

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
358
Likes
324
Points
80

African Believer

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
358 324 80
Aiseeee naomba nifundishe nikawalishe kuku wangu
Ni kazi rahisi sana kuwazalisha, kama ni kwa ajili ya kuku unahitaji tu maboksi ya mbao yenye kipenyo kidogo kisha weka masalia ya chakula kidogo na makaratasi kisha weka sehemu yenye hoto la wastani.

Kama huna mbegu za mende weka maboksi yako sehemu ambazo ulishawaona mende wakipita baada ya hapo hakikisha panya hawaingii kwani watawapunguza sana katika hatua za mwanzo na utachelewa kupata matokeo mazuri. Kumbuka mende wanapendwa sana na panya.
 
African Believer

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
358
Likes
324
Points
80

African Believer

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
358 324 80
Nimewaza.

Mlianzisha shamba.

Kutokana na soko kujificha mkasitisha mradi.

Umesema wana protini nyingi.

Wale mende wa shamba la majaribio mliwapeleka wapi?
Kwa bahati nzuri sisi ni wafugaji wa kuku pamoja na bata pia. Hivyo kwa kiwango kikubwa tuliwapa kuku na bata ambao wanawapenda sana na kiwango fulani niliwala mimi mwenyewe kwani mengine waligoma.

Na mpaka sasa bado tunafuga kienyeji kwa ajili ya kuku na bata.

Pindi tukipata soko la uhakika tutaurejelea tena mradi wetu kwa kuboresha changamoto zilizojitokeza hapo awali, kwani tayani mwanga wa ufugaji wa wadudu hao tunao kwa kiwango fulani kizuri.
 
Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Messages
11,310
Likes
18,381
Points
280
Age
25

Castr

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2014
11,310 18,381 280
Kwa bahati nzuri sisi ni wafugaji wa kuku pamoja na bata pia. Hivyo kwa kiwango kikubwa tuliwapa kuku na bata ambao wanawapenda sana na kiwango fulani niliwala mimi mwenyewe kwani mengine waligoma.

Na mpaka sasa bado tunafuga kienyeji kwa ajili ya kuku na bata.

Pindi tukipata soko la uhakika tutaurejelea tena mradi wetu kwa kuboresha changamoto zilizojitokeza hapo awali, kwani tayani mwanga wa ufugaji wa wadudu hao tunao kwa kiwango fulani kizuri.
Ule urojo wake mweupe mtamu eeh?
 
Forum statistics

Threads 1,203,545
Members 456,791
Posts 28,118,074