Upatikanaji wa dawa kwenye Zahanati na Hospitali za Serikali, ukweli ni upi?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,452
215,249
Awamu ya 5 tuliambiwa upatikanaji wa dawa kwenye maeneo hayo umefikia hadi 94% hii likuwa 2018 , lakini watu walewale kwenye awamu ya 6 mwaka 2021 tunaambiwa upatikanaji wa dawa kwenye Zahanati na Hospitali zilezile umepanda hadi 61% kutoka 21% ilivyokuwa awali .

Anayeelewa hizi Takwimu atufafanulie

Nakala imfikie Mtaalamu wa Namba Tanzania Humphrey Polepole

 
  • Nzuri
Reactions: BAK
hivi kauli za awamu ya tano kuna mtu timamu alikua anaziamini? uongo wa kupitiliza ule ulipumbaza watu
 
Juzi kuna mwana JF humu ndani alimuonya Gerson Msigwa kwamba asiende kichwa kichwa hayajui madudu ya ile taasisi watu hawakumuelewa member!

Sasa naona mmeuona mkanganyiko, maana kuna watu wanasema afande ndo kasababisha ile taasisi i under perform, we don't know which is which!!
 
images (3).jpeg
 
hivi kauli za awamu ya tano kuna mtu timamu alikua anaziamini? uongo wa kupitiliza ule ulipumbaza watu
Msigwa alikuwa msemaji wa Rais , huyu kila uongo aliupamba , kulikoni leo ?
 
Kuna siku mama alisema uchumi umeshuka Sana, ikapita kama wiki akasema uchumi umekua Sana.
Aisee CCM ni Kama mitambo flani hivii
 
Sifahamu takwimu hizi wanazi toa wapi au mbinu zilizo tumiwa kufikia taarifa hizo lakini dawa ambazo zinatoka MSD kwenda kwenye hospitali za serikali hazi toshi kwa namna ya idadi na namna ya kutibu magonjwa tofauti tofauti.

Matibabu ya watoto chini ya miaka mitano, wazee waliozidi miaka 60 na wenye presha na kisukari huwa ni bure lakini ukiangalia dawa zilizopo kwa wagonjwa hawa na ulinganishe na wanaotibiwa kwa bima ya afya (NHIF), utagundua kwamba tofauti ipo kubwa sana.

Siamini kwamba afya inaweza kuwa bure kwa wananchi wote. Bima ya afya iboreshwe na wananchi wawezeshwe kuwa na bima.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom