Upasuaji wa ubongo mgonjwa akiwa macho wafanyika kwa mara ya kwanza Kenya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,872
Nchini Kenya umefanyika upasuaji wa kwanza wa ubongo huku mgonjwa akiwa macho.

Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya-Nairobi Hospital, mjini Nairobi Kenya ambapo mgonjwa huyo alikuwa macho na kuweza kuzungumza wakati wote wa upasuaji huo.

Madaktari wa upasuaji wanategemea mchakato wa kipekee a upasuaji unaomfanya mgonjwa awe macho, ambao bado ni hatari, lakini unaweza kuleta matokeo bora na kupunguza hatari ya jeraha katika ubongo.

Katika aina hii ya tiba, madaktari bingwa wa upasuaji wa fuvu la kichwa wanaweza pia kufuatilia hali ya mgonjwa wakati wa upasuaji, hii ikimaanisha kuwa wanaweza kuondoa uvimbe ambao kwa kawaida usingeweza kutolewa salama.

Upasuaji huo wa kufungua fuvu la kichwa au 'brain craniotomy', kwa lugha ya kitaalamu unaangaliwa kama mafanikio makubwa katika sekta ya tiba kuweza kufanyika nchini Kenya.
 

Attachments

  • 1606394239774.gif
    1606394239774.gif
    42 bytes · Views: 1
Habari haijajitosheleza vizuri, Surgeons na wakina nani? Hakuna usaidizi kutoka mataifa mengine?
 
Mbona utaalam wa kawaida sana huo hapa kwetu!?? Wataalamu sasa hivi wanachangamkia misheni ya kulink & kuhifadhi kumbukumbu za ubongo kwenye external hard devices (drives) halafu na kuextend maisha indefinetely plus kumrudishia uhai marehemu na kumfanya mzee awe kijana au mtoto tena --- "incarnomorphogenology"
 
Unauhakika hata hospitali yahaydom manyara wanafanya upasuaji wa ubongo
Hatuongei kuhusu upasuaji wa ubongo tu maana hata Somalia wanaweza kufanya upasuaji huo. Hapa tunaongea kuhusu upasuaji wa ubongo huku mgonjwa akiwa na fahamu zake zote ila anapewa dawa ya kuzuia uchungu.

Sasa daktari anamuuliza mgonjwa maswali na mgonjwa anajibu. Akishindwa kujibu au akiongea kwa kigugumizi basi daktari anajua kwamba amegusa mahali pabaya. Hii neurosurgery ya aina hii nyie hamfanyi.
 
Hatuongei kuhusu upasuaji wa ubongo tu maana hata Somalia wanaweza kufanya upasuaji huo. Hapa tunaongea kuhusu upasuaji wa ubongo huku mgonjwa akiwa na fahamu zake zote ila anapewa dawa ya kuzuia uchungu. Sasa daktari anamuuliza mgonjwa maswali na mgonjwa anajibu. Akishindwa kujibu au akiongea kwa kigugumizi basi daktari anajua kwamba amegusa mahali pabaya. Hii neurosurgery ya aina hii nyie hamfanyi.
Una uhakika?
 
Back
Top Bottom