Upanga, Dar: Yaliyojiri kutoka Ukumbi wa JWTZ, Mkutano na Waandishi wa Habari

Aisee hivi ni kweli hakunaga upendeleo wa kijiunga huko, 😀😃😃😃
Salaam Wakuu,

Leo Jeshi la Wananchi Tanzania, linafanya Mkutano na Waandishi wa habari. Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) kutoa Tamko Maalumu 30 Novemba, 2021

Nipo Nimefika kwenye Ukumbi huu kuwajuza kila kitakachojiri.

=====

UPDATES: 1022hrs

======
View attachment 2027879
Waandishi wameshafika eneo la tukio

1034 hrs: Mkurugenzi wa Habari wa JWTZ, Luteni Kanali Gervas Ilonda
View attachment 2027914
Wengi tumekutana hapa kujua ni nini hasa tunataka kuzungumza. Siji kutoa tamko bali nimekuja kutoa ufafanuzi wa mambo ambayo jeshi limeona yanaendelea. Hatuwezi kuyafumbia macho.

Naomba nitoe ufafanuzi kwa Vijana wanaojiandikisha kujiunga na Jeshi.

Hapo nyuma Viongozi wamekuwa wakitembelea Miradi ya Kimkakati. Wakiwa kule, wamekuwa wakilizishwa na Vija wa kujenga taifa wanavyojituma na kuwa Wazalendo.

Viongozi baada ya kuona uzalendo na umahili wa hali ya Juu wamekuwa wakiwaahidi kwamba nafasi za jeshi zikitka watapata.

Hivi karibu zimetoka nafasi kwa vijana wa Makambi ya JKT sio wote. Zimetoka chache lakini si haba.

Nimelazimika kuongea na vyombo vya habari ili tufahamishe umma kwamba kwa sasa kumeanza kuibuka kwa vitendo cya baadhi ya watu kutumia hizi nafasi za hawa vijana kujinufaisha. Vitendo vya Rushwa na Udanganyifu katika nafasi hizi. Matapeli hao wamekwenda mbali zaidi kwa kusingizia viongozi kwamba wametumwa wamewe hela ili vijana waandikishwe. Wanadai Mkuu wa majeshi ndo amewatuma. Jambo hilo sio kweli. Hatiwezi kulifumbia macho kuona viongozi wetu wanasumbuliwa. Mbaya zaidi wanachukua nyumba za kulala wageni wanaingiza vijana na kuwaambia subiri tunaenda kuwatafutia kazi, matokeo yake wanaanza kuwafuata wakuu wa Majeshi kudai nafasi zao. Kupitia kwenu nawaomba muwapuuze na msidanganyike kutoa fesha kwa nafasi za kuingia jeshini.

Natoa rai kwa wanaofanya Vitendo hivyo kwamba sio vya busara wala kiungwana. Waache mara moja.

Baadhi ya Wazazi wameanza kuwafuata viongozi waliopo Jishini kwenye ngazi mbalimbali kuwaomba wawasaidie kuwaingiza vijana wao Jeshini. Jeshi la Tanzania, lina taratibu na kanuni za kuingiza Vijana Jeshini sio kwa fedha wala kuoneana huruma.

Kijana anatakiwa awe

1). Raia wa Tanzania wa kuzaliwa

2). Umri awe na miaka 18 hadi 28

3) Awe na afya njema ya mwili na akili

4). Lazima awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri, asiwe amepatikana na hatia ya kijinai

5) Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vya shule na chuo.

Kwa Upande wa Madaktari

Awe amemaliza mafunzo kwa vitendo na pamoja na kusaidiwa na bodi ya madaktari.

Hizi ndizo sifa zitatumika kuwachuja vijana Walioandikishwa kuingia Jeshi la wananchi wa Tanzania. Sio wote walioandikishwa watapita.

Kazi ya jeshi ni kazi ngumu, ukiingia kwa hela bila kuwa na utimu wa akili na mwili atapoteza uhai au atakuwa mlemavu

Kazi anayojiandikisha kufanya, wengi wanasema ni ajira. Hakuna mwanajeshi mwenye ajira. Wote wameandikishwa. Mwanajeshi halipwi Mshahara bali malipo. Huwezi kuajiriwa kutoa uhai wako bali unajiandikisha. Unatoa uhai kwa kulinda nchi. Ndo maana hatutoi ajira kwa upendeleo wala Rushwa.

Watanzania tuungane kupinga vitendo hivi viovu vya rushwa, udanganyifu Wizi, halafu akishakuibia analala mbele.

Nawaomba watanzania wote kwa moyo mmoja mkunjufu, tuungane kufichua vitendo hivi. Mkisikia mtu anataka apewe hela, toeni taarifa, jeshini, Polisi na TAKUKURU.

Watanzania tuendelee kuliunga mkono jeshi letu lililo imara. Tupo imara kuilinda katiba ya jamhuru ya Muungano wa Tanzania.

Asanteni sana
View attachment 2027914
View attachment 2027953
View attachment 2027959
View attachment 2027960
 
Kuwaweka watu hapo kumbe ni hilo tu wangesema wamewakamataa wahusika itakuwa bora.....jeshiiiiii buana naliheshimu lakina leo EMPTY kabisa
Hapa wamechemsha. Unless kama watakuwa wamebadili mawazo. Si wangetoa tu kapress release badala ya kuweka nchi kihoro.... Unless wanatuandaa kisaikolojia...!!
 
haya mambo si yalipaswa yasemwe na wizara ya ulinzi na is jeshi lenyewe? huko nyuma yalikuwa yanasemwa na waziri wa ulinzi au ye yote kwa niaba yake, huyu mabeyo ameamua kufanya hivi kwa kuwa rais na waziri wa ulinzi ni wanawake?
Aisee khaa wabongo noma!
 
Sasa hivi jeshi la wananchi limeanza tena kutumika kama toilet paper kwa manufaa ya wanasiasa wa CCM.Hatujawahi kuwa na Tanzania ya hovyo kama hii tokea uhuru.
Wasio miliki nyumba nao wanalipishwa kodi ya majengo ili makusanyo yanone. Hata 'Zakayo' hakufanya hivyo.
 
Mabeho angekemea hawa watawala uchwara waliobuni kesi za ugaini kwa matakwa yao ya kiuchwara kwani yanalipaka matope Taifa.
Free Freeman Mbowe
 
Aliyowaitia waandishi wa habari amekatazwa kuyasema dakika za mwisho! Utajua tu katika ufunguzi wa speech yake. Si siyo mbumbmbu!
 
Salaam Wakuu,

Leo Jeshi la Wananchi Tanzania, linafanya Mkutano na Waandishi wa habari. Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) kutoa Tamko Maalumu 30 Novemba, 2021

Nipo Nimefika kwenye Ukumbi huu kuwajuza kila kitakachojiri.

=====

UPDATES: 1022hrs

======
View attachment 2027879
Waandishi wameshafika eneo la tukio

1034 hrs: Mkurugenzi wa Habari wa JWTZ, Luteni Kanali Gervas Ilonda
View attachment 2027914
Wengi tumekutana hapa kujua ni nini hasa tunataka kuzungumza. Siji kutoa tamko bali nimekuja kutoa ufafanuzi wa mambo ambayo jeshi limeona yanaendelea. Hatuwezi kuyafumbia macho.

Naomba nitoe ufafanuzi kwa Vijana wanaojiandikisha kujiunga na Jeshi.

Hapo nyuma Viongozi wamekuwa wakitembelea Miradi ya Kimkakati. Wakiwa kule, wamekuwa wakilizishwa na Vija wa kujenga taifa wanavyojituma na kuwa Wazalendo.

Viongozi baada ya kuona uzalendo na umahili wa hali ya Juu wamekuwa wakiwaahidi kwamba nafasi za jeshi zikitka watapata.

Hivi karibu zimetoka nafasi kwa vijana wa Makambi ya JKT sio wote. Zimetoka chache lakini si haba.

Nimelazimika kuongea na vyombo vya habari ili tufahamishe umma kwamba kwa sasa kumeanza kuibuka kwa vitendo cya baadhi ya watu kutumia hizi nafasi za hawa vijana kujinufaisha. Vitendo vya Rushwa na Udanganyifu katika nafasi hizi. Matapeli hao wamekwenda mbali zaidi kwa kusingizia viongozi kwamba wametumwa wamewe hela ili vijana waandikishwe. Wanadai Mkuu wa majeshi ndo amewatuma. Jambo hilo sio kweli. Hatiwezi kulifumbia macho kuona viongozi wetu wanasumbuliwa. Mbaya zaidi wanachukua nyumba za kulala wageni wanaingiza vijana na kuwaambia subiri tunaenda kuwatafutia kazi, matokeo yake wanaanza kuwafuata wakuu wa Majeshi kudai nafasi zao. Kupitia kwenu nawaomba muwapuuze na msidanganyike kutoa fesha kwa nafasi za kuingia jeshini.

Natoa rai kwa wanaofanya Vitendo hivyo kwamba sio vya busara wala kiungwana. Waache mara moja.

Baadhi ya Wazazi wameanza kuwafuata viongozi waliopo Jishini kwenye ngazi mbalimbali kuwaomba wawasaidie kuwaingiza vijana wao Jeshini. Jeshi la Tanzania, lina taratibu na kanuni za kuingiza Vijana Jeshini sio kwa fedha wala kuoneana huruma.

Kijana anatakiwa awe

1). Raia wa Tanzania wa kuzaliwa

2). Umri awe na miaka 18 hadi 28

3) Awe na afya njema ya mwili na akili

4). Lazima awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri, asiwe amepatikana na hatia ya kijinai

5) Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vya shule na chuo.

Kwa Upande wa Madaktari

Awe amemaliza mafunzo kwa vitendo na pamoja na kusaidiwa na bodi ya madaktari.

Hizi ndizo sifa zitatumika kuwachuja vijana Walioandikishwa kuingia Jeshi la wananchi wa Tanzania. Sio wote walioandikishwa watapita.

Kazi ya jeshi ni kazi ngumu, ukiingia kwa hela bila kuwa na utimu wa akili na mwili atapoteza uhai au atakuwa mlemavu

Kazi anayojiandikisha kufanya, wengi wanasema ni ajira. Hakuna mwanajeshi mwenye ajira. Wote wameandikishwa. Mwanajeshi halipwi Mshahara bali malipo. Huwezi kuajiriwa kutoa uhai wako bali unajiandikisha. Unatoa uhai kwa kulinda nchi. Ndo maana hatutoi ajira kwa upendeleo wala Rushwa.

Watanzania tuungane kupinga vitendo hivi viovu vya rushwa, udanganyifu Wizi, halafu akishakuibia analala mbele.

Nawaomba watanzania wote kwa moyo mmoja mkunjufu, tuungane kufichua vitendo hivi. Mkisikia mtu anataka apewe hela, toeni taarifa, jeshini, Polisi na TAKUKURU.

Watanzania tuendelee kuliunga mkono jeshi letu lililo imara. Tupo imara kuilinda katiba ya jamhuru ya Muungano wa Tanzania.

Asanteni sana
View attachment 2027914
View attachment 2027953
View attachment 2027959
View attachment 2027960
Kwa msingi huu unaweza kufikiria au kuwaza, kwani wao kama kitengo muhimu hawana utawala nora wa kuwaajiri au kuwatahini wanaohitajika hadi waletewe vijana. Inadhihirish wazi ule mtindo wa vikaratasi bado upo na ndio maaana hatuendi mbele.
Nadhani kitenho cha uajiri kinahitaji kujiongeza zaidi.
 
haya sasa wale mbumbumbu walokuwa wanamponda mama na uongozi wake wakisubiri kwa hamu tamko la jeshi wamejinyea tyari.

mama ni mzr, mchapakazi anashaurika, na hekima anayo hata hao wafanyakazi wake JW wanalijua hilo na dunia nzima tunalitambua hilo.
 
JWTZ ni Jeshi la kizalendo, lenye utii, weledi na uadilifu. Limesukwa kimfumo tangu enzi za Mwalimu. Mnaofanya utapeli ili kuchafua Jeshi acheni. Na hayo mawazo mengine ya kipori pori kamwe hayawezi kutokea Tanzania.
 
Back
Top Bottom